Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

DEAR EX: Wamezikamua pesa nyingi timu za utotoni zilipowarudisha

Muktasari:

  • Hata hivyo, si kila mchezaji anayeibukia kwenye akademia ya timu anapanda na kupewa nafasi kubwa kwenye timu yake, badala yake anaondoka na kwenda kutamba kwingineko.

LONDON, ENGLAND: KWA mashabiki wa soka, hakuna kitu kitamu kwao kama kuona mchezaji wao akiibukia kutoka kwenye akademia zao kisha akapata namba kwenye kikosi cha timu ya wakubwa na kufanya vizuri akiwa panga pangua kikosini.

Hata hivyo, si kila mchezaji anayeibukia kwenye akademia ya timu anapanda na kupewa nafasi kubwa kwenye timu yake, badala yake anaondoka na kwenda kutamba kwingineko.

Kwa mfano kipa James Trafford, alijiunga na Manchester City mwaka 2015 akiwa na umri wa miaka 12, lakini aliuzwa Burnley miaka minane baadaye akiwa hajacheza mechi yoyote kwenye kikosi cha wakubwa.

Baada ya miaka miwili katika kikosi cha Burnley, Trafford anarudi Man City huku akiwa na uhakika wa kwenda kuwa kipa chaguo la kwanza.

Kwa mfano kama huo, hii hapa orodha ya mastaa wa maana kabisa ambao waliachwa na timu zilizowatengeneza kutokea kwenye akademia yao, kisha wakaondoka na baadaye kuwarudisha kwa pesa nyingi sana.


Cesc Fabregas Kutoka Arsenal kwenda Barcelona

Miaka ya 2000 ilishuhudia akademia ya La Masia ikitengeneza vijana matata kabisa. Akademia hiyo ya klabu ya Barcelona iliibua mastaa matata kabisa kama Andres Iniesta na Lionel Messi, ambao walienda kuungana na wahitimu wenzao Xavi na Carles Puyol kuifanya Barcelona kuwa hatari uwanjani.

Kabla ya muongo kumalizika, Gerard Pique naye akaungana nao. Pique awali aliondoka Catalonia kwenda Manchester United, lakini kitendo cha kushindwa kucheza huko Old Trafford kilimrudisha Camp Nou. Barca ililipa Pauni 5 milioni kumrudisha beki beki huyo wa kati Barcelona, wakati Cesc Fabregas alilipiwa pesa nyingi sana kurudi Barcelona, ambako ndiko alikoanzia.

Barca ilimrudisha Fabregas kutoka Arsenal kwa ada ya Pauni 25.4 milioni mwaka 2011. Alicheza hapo kwa miaka mitatu, akifunga mabao 42 na asisti 50 katika mechi 151 za michuano yote kabla ya kuondoka kwenda Chelsea.


Mats Hummels kutoka Borussia Dortmund kwenda Bayern Munich

Kwa namna fulani, Mats Hummels alitengeneza jina lake huko North Rhine-Westphalia, mahali ambako alizaliwa.

Kwa kusema hivyo, beki huyo wa kati alikuwa zao la akademia ya Bayern Munich. Na kabla ya kuonyesha ubora wake kwenye kikosi cha kwanza, alipelekwa kwa mkopo Borussia Dortmund, ambako alianza kucheza kwenye Bundesliga na kulifanya jina lake la Hummels kufahamika.

Baada ya msimu mmoja wa mkopo, akabeba jumla Dortmund. Bayern ikamfuatilia kwa karibu Hummels na kuamua kuvunja benki kumrudisha kwenye kikosi chao mwaka 2026 kwa ada ya Pauni 33.8 milioni.


Dani Carvajal Kutoka Bayer Leverkusen kwenda Real Madrid

Kipindi cha Dani Carvajal kwenye Bundesliga akiwa na Bayer Leverkusen kilikuwa matata sana. Mhispaniola huyo alitengeneza jina lake kuwa huko huko Ujerumani katika msimu wa 2012-13 na kuwafanya Real Madrid kutaka kumrudisha kwenye kikosi chao mchezaji huyo. Carvajal aliibukia kutokea kwenye akademia ya Real Madrid, La Fabrica kabla ya kuanza kucheza kwenye kikosi cha Castilla.

Leverkusen ilipohitaji beki wa kulia, ilienda kumsajili mwaka 2012 na kwenda kumfanya kuwa bora, huku Real Madrid iliweka kipengele cha kumnunua upya staa huyo, kitu ambacho ilifanya kwa kutumia pesa nyingi.


Paul Pogba kutoka Juventus kwenda Man United

Paul Pogba aliibukia kwenye timu za watoto za Man United kabla ya kupewa mechi chache za kucheza kikosi cha kwanza chini ya kocha Sir Alex Ferguson.

Baada ya kuona hapati sana namba, aliamua kwenda kujiunga na Juventus bure kabisa na kwenda kuwa kiungo hodari huko kwenye soka la Italia.

Kiwango chake matata katika kikosi cha Juventus kiliwafanya Man United kutaka kumrudisha kiungo wao huo wa zamani kwenye timu yao na walifanya hivyo kwa kutumia pesa nyingi sana, Pauni 89 milioni.

Na wakati Pogba anarudi Man United walitumia maneno “Pogback”, kabla ya kudumu kwa miaka kadhaa na kurudi tena bure Juventus.


Alvaro Morata kutoka Chelsea kwenda Atletico Madrid

Mzaliwa wa Madrid, Alvaro Morata alikuwa akitalii kwenye klabu za jiji la Madrid huko Hispania. Alianzia Atletico kati ya mwaka 2005 na 2007, kabla ya kwenda kujiunga na Getafe na baadaye akaenda kujiunga La Fabrica. Morata aliibukia kwenye kikosi cha kwanza huko Bernabeu, akicheza mechi yake ya kwanza 2010 alipotokea benchini kuchukua nafasi ya Angel Di Maria.

Alicheza mechi 52 kwenye kikosi cha Los Blancos kabla ya kujiunga na Juventus.

Baada ya misimu miwili Juventus, Morata alirudi Real Madrid. Kisha aliuzwa Chelsea kwa ada ya Pauni 60 milioni, kabla ya kurudi Atletico Madrid na alilipiwa ada ya Pauni 58 milioni.


Rodri kutoka Villarreal kwenda Atletico Madrid

Kama ilivyotokea kwa Morata, Rodri alitumikia miaka michache kwenye akademia ya Atletico, ambayo ilimnasa wakati anamiaka 11 akitokea Rayo Majadahonda mwaka 2007.

Lakini, Rodri aliachwa mwaka 2013 kutokana na kuwa goigoi na hatimaye, Villarreal ikamnasa. Akiwa huko Villarreal, Rodri alitamba kwa kiwango bora kabisa na kuwafanya Atletico Madrid kuona makosa yao na kuamua kumrudisha kiungo huyo kwenye kikosi chao kwa ada ya Pauni 20 milioni mwaka 2018.

Kwa sasa, Rodri anakipiga Man City na alishinda tuzo ya Ballon d’Or mwaka jana.


Marco Reus kutoka Borussia Monchengladbach kwenda Borussia Dortmund

Mzaliwa huyo wa Dortmund, gwiji wa Dortmund aliibukia kwenye akademia za huko  Dortmund. Marco Reus alibaki Ruhr Valley kwa miaka 10 kabla ya kuachwa kwenye dirisha la majira ya kiangazi 2006 kabla ya kwenda kujiunga na timu ya daraja la tano, Rot Weiss Ahlen.

Huko Rot Weiss Ahlen na kuongeza kikosi chake na akiwa na miaka 19 alipanda viwango vyake.

Miamba ya Bundesliga katika msimu wa 2008-09, Borussia Monchengladbach ilinasa saini ya Reus kabla ya Dortmund kumsajili na kumrudisha kwenye kikosi chao, ikitumia Pauni 17 milioni mwaka 2012.


Aaron Ramsdale kutoka Bournemouth kwenda Sheffield United

Aaron Ramsdale anaonekana kuwa kwenye uhamisho tena akijaribu kuwa kipa namba moja kwenye Ligi Kuu England.

Staa huyo Mwingereza alikulia kwenye akademia ya Sheffield United kabla ya kusajiliwa na Bolton Wanderers mwaka 2013, akiwa mwanafunzi.

Mwaka 2016, Ramsdale alisaini mkataba wa soka la kulipwa Blades na kucheza mechi mbili kwenye Kombe la FA katika msimu wa 2016-17.

Lakini, kiwango chake huko Bramall Lane kilikuwa moto. Bournemouth ilimsajili Ramsdale mwaka 2017 kwa ada ya Pauni 1 milioni, kabla ya Sheffield United kumrudisha kwenye kikosi chao miaka mitatu baadaye kwa Pauni 18.5 milioni.


Danny Ings kutoka Liverpool kwenda Southampton

Southampton mara nyingi imekuwa wagumu kuachia mchezaji mwenye kipaji asinaswe na timu yao.

Miamba hiyo imekuwa na huduma za mastaa wengi akiwamo Danny Ings, ambaye ilimtengeneza yenyewe kutoka kwenye akademia yao kabla ya kuondoka na baadaye kumrudisha kwa pesa nyingi.

Southampton ililipa Pauni 18 milioni kumrudisha Ings kwenye kikosi chao akitokea Liverpool mwaka 2019. Hilo lilitokea baada ya kutamba Bournemouth na baadaye Burnley. Southampton ilipiga faida kubwa kwa Ings baada kumuuza Aston Villa kwa ada ya Pauni 25 milioni mwaka 2021.


Jordi Alba Kutoka Valencia Kwenda Barcelona

Akitokea kwenye akademia ya La Masia, alishindwa kupewa nafasi ya kucheza kwenye kikosi cha kwanza. Lakini, hiyo haina maana hakuwa na kiwango bora cha kupata nafasi. Jordi Alba aliachwa na Barca mwaka 2005 kwa madai alikuwa na umbo dogo sana. Kabla ya kuanza kuonyesha kiwango kikubwa akiwa beki, Alba kipindi hicho alikuwa akitumika kama winga wa kushoto.

Lakini, umbo lake halikuonekana shida mwaka 2012 wakati Barcelona ilipomrudisha kwenye kikosi chao kwa ada ya Pauni 14 milioni akitokea Valencia. Ni staa mwingine aliyerudi kwenye timu ya zamani kwa pesa nyingi.


Nicolas Anelka Kutoka Real Madrid kwenda PSG

Arsene Wenger alimsajili Nicolas Anelka akiwa kinda Februari 1997 kwa ada ya Pauni 500,000. Kwa kipindi hicho, alikuwa na umri wa miaka 17 na alichezeshwa mechi chache sana akiwa anatokea benchi huko PSG.

Lakini, mwaka mmoja baadaye baada ya kushinda taji la Ligi Kuu England na Kombe la FA akiwa na kikosi cha Arsenal, akifunga kwenye mechi ya fainali dhidi ya Newcastle United, Anelka alibadilika na kuonekana kuwa staa wa kiwango cha dunia huko Highbury.

Na hapo ndipo, Real Madrid ilipokwenda kumsajili kwa ada ya Pauni 22.3 milioni mwaka 1999. Alidumu kwa mwaka mmoja huko Bernabeu kabla ya klabu yake ya zamani aliyoibukia tangu utotoni, PSG ilipomrudisha kikosini kwa ada ya Pauni 22 milioni mwaka uliofuatia.