Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Dakika 444 bila bao, huyu ndiye Viktor Gyökeres

Muktasari:

  • Baada ya kufunga mabao matatu katika mechi zake nne za mwanzo, nyota huyo aliyesajili kwa pauni milioni 64, hajafunga katika mechi zilizofuata akitumika kwa dakika 444, huku kocha Mikel Arteta akisema alimkumbatia mshambuliaji huyo baada ya ushindi wa 2-0 dhidi ya West Ham kwa kupongeza juhudi zake.

Klabu ya Arsenal imeanza msimu kwa kiwango cha kuvutia, ikishinda mechi nane kati ya kumi za mwanzo, lakini mambo hayajawa mepesi sana kwa mshambuliaji mpya Viktor Gyökeres.

Baada ya kufunga mabao matatu katika mechi zake nne za mwanzo, nyota huyo aliyesajili kwa pauni milioni 64, hajafunga katika mechi zilizofuata akitumika kwa dakika 444, huku kocha Mikel Arteta akisema alimkumbatia mshambuliaji huyo baada ya ushindi wa 2-0 dhidi ya West Ham kwa kupongeza juhudi zake.

Gyökeres amecheza dakika 90 katika mechi sita kati ya kumi za mwanzo, zaidi ya vile Arteta alivyopanga, kutokana na jeraha la goti la Kai Havertz lililomnyima nafasi ya kumpumzisha mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 27.

Havertz ni miongoni mwa wachezaji wanaoaminika zaidi na Arteta, na kuna hoja kwamba Mjerumani huyo angeanza badala ya Gyökeres katika michezo mikubwa ya ugenini dhidi ya Liverpool ambayo ndiyo mechi pekee Arsenal imepoteza, pia dhidi ya Newcastle United na Manchester United ambazo zote imeshinda.

Pia, Gyökeres hakuwa na maandalizi kamili ya kabla ya msimu baada ya kukosa mazoezi na kikosi cha Sporting Lisbon akilazimisha uhamisho kwenda London Kaskazini.

Hata hivyo, Gyökeres ametua Arsenal akisajiliwa kwa mbwembwe kubwa baada ya kufunga mabao 97 katika michezo 102 akiwa na Sporting ndani ya misimu miwili.

Ukosefu wa mabao kwa sasa si tatizo kubwa kwani Arsenal inashinda, lakini ukweli ni kwamba alisajiliwa ili kusaidia timu kutwaa taji lao la kwanza tangu 2020.

Arteta ameonyesha kuthamini mchango wa Gyökeres katika michezo ya mwanzo na kumpongeza mara kadhaa kwa kazi yake ngumu, ambayo mara nyingi haionekani kwa urahisi.

Baada ya ushindi dhidi ya Olympiacos, Arteta alimwelezea mshambuliaji huyo kuwa mzuri sana na akaongeza kuwa anafanya kazi kwa bidii kubwa.

Wakati Arsenal ilipomsajili Gyökeres, kulikuwa na matumaini kwamba uwepo wake ungefungua nafasi zaidi kwa washambuliaji wanaocheza nyuma yake kama Martin Ødegaard, Bukayo Saka, Eberechi Eze na Gabriel Martinelli.

Kumekuwa na dalili chache za hivyo kutokea, lakini Gyökeres binafsi angependa kupata zaidi katika mechi zake kumi za kwanza akiwa mhimili wa safu ya ushambuliaji akifunga katika michezo miwili pekee ikiwa ni mara mbili katika ushindi wa 5-0 dhidi ya Leeds mwezi Agosti, na bao moja katika ushindi wa 3-0 dhidi ya Nottingham Forest mwezi Septemba.


TAKWIMU ZINAONYESHA NINI?

Arsenal imebadilisha mtindo wa uchezaji msimu huu ili kupeleka mipira haraka zaidi katikati ya uwanja na kucheza kwa njia ya moja kwa moja.

Mabadiliko haya yamekusudiwa kumsaidia Gyökeres, ambaye tofauti na Havertz, hapendi kushuka hadi chini kusaidia ujenzi wa mashambulizi. Nguvu yake kubwa ipo katika kukimbia kati ya mabeki wa kati na kutafuta nafasi nyuma yao.

Katika mechi za Arsenal msimu huu, mara nyingi imeonekana viungo wakitafuta pasi ya moja kwa moja inayoweza kumfungulia nafasi ya kufunga.

Takwimu zinaonyesha Gyökeres amepata nafasi 23 za kufunga, lakini amepiga mashuti saba pekee yaliyolenga goli katika mechi hizo kumi, moja kati ya hayo ikiwa penalti.

Msimu uliopita, Arsenal ilihangaika kuvunja ukuta wa timu zinazocheza kwa kujilinda sana, na hivyo sasa wameamua kucheza kwa kasi zaidi ili kuwaumiza wapinzani.

Aidha, Arsenal wameanza kutumia krosi mara nyingi zaidi ili kuongeza nafasi za kufunga.

Moja ya mabao matatu ya Gyökeres ilitokana na penalti lakini hilo lilitokea wakati Bukayo Saka tayari alikuwa ametolewa uwanjani kwenye ushindi wa 5-0 dhidi ya Leeds.

Ingawa Arteta aliwahi kusema katika mahojiano na ESPN Brazil kuwa Gyökeres ndiye mtaalamu bora wa penalti kwenye klabu, ni Saka aliyepiga penalti katika ushindi dhidi ya West Ham, jambo linaloonyesha kuwa huenda Mwingereza huyo ndiye chaguo la kwanza msimu huu.

Saka, aliyefikisha mechi 200 za Ligi Kuu akiwa na Arsenal katika ushindi huo, amempa Gyökeres sapoti kubwa.

“Nadhani Viktor anacheza vizuri sana,” amesema Saka baada ya mechi hiyo iliyochezwa Oktoba 4, 2025.

“Hakuna shaka kwamba atafunga mabao. Kile anachotuletea kama timu ni kikubwa sana hasa jinsi anavyoshikilia mpira, anakimbia, anavyotishia mabeki. Ni sehemu kubwa ya sababu kwa nini tunashinda mechi. Mabao yake yatakuja, tunajua hilo. Tunamwamini, na hakuna shaka yoyote.”


JE, HIZI NI DALILI ZA MATUMAINI KWA GYÖKERES?

Ni kweli kwamba mwanzo wa Gyökeres haukuwa rahisi, lakini kuna ishara kadhaa kwamba mambo yanaweza kuimarika.

Mshambuliaji huyo alianza msimu akiwa nyuma kwa kiwango cha utimamu wa mwili kutokana na maandalizi yaliyovurugika kabla ya msimu.

Jeraha la Havertz limefanya atumike zaidi ya ilivyopangwa, jambo lililoathiri uhusiano wake na viungo wanaocheza nyuma yake.

Gyökeres ni mchezaji anayependa kukimbia, kutafuta nafasi na pia kushikilia mpira wakati Arsenal inataka kushambulia kwa kasi.

Ni mchezaji mwenye mwili mkubwa, lakini vivyo hivyo mabeki wengi wa Ligi Kuu, hivyo atalazimika kuzoea changamoto za kimwili ili kuwashinda.

Kila mara maswali yanapoulizwa kuhusu Gyökeres, watu hurejelea tabia yake ya kupambana na kutoogopa changamoto sifa ambazo zitamsaidia kwenye mazingira magumu ya Ligi Kuu.

Wachezaji wenzake wanaonekana pia kutamani afanikiwe, mfano ni Martinelli aliyemruhusu mpira wa Gyökeres uingie wavuni dhidi ya Olympiacos kabla haujakosa goli na yeye kuumalizia.

Huenda mtindo wa Gyökeres usiwe wa kuvutia kama wa washambuliaji wapole wa Ligi Kuu, lakini dalili zinaonyesha anaweza kuwa na ufanisi mkubwa.

Kwa mtindo wa moja kwa moja zaidi wa Arsenal na safu ya kiungo iliyoundwa kumtengenezea nafasi, ana kila nyenzo ya kufanikiwa.

Swali lililosalia ni moja tu: Je, ataweza kuzitumia vyema nyenzo hizo?