Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Arteta: Bado nina imani kubwa na Viktor Gyokeres

GYOKERES Pict

Muktasari:

  • Arteta amesema pamoja na kumshuhudia mdhambuliaji huyo wa Sweden akishindwa kufunga katika mechi ya jana Jumamosi, Oktoba 04, 2025 dhidi ya West ham United iliyokubali kubamizwa 2-0 kwenye Uwanja wa Emirates, lakini bado alionyesha uwezo na kujituma wakati wote.

KOCHA wa Arsenal, Mikel Arteta, amemwagia sifa Viktor Gyokeres kwa juhudi za kupambana tangu alipoanza kumpa nafasi ya kucheza kwenye kikosi cha Washika Bunduki hao wa jijini London.

Arteta amesema pamoja na kumshuhudia mdhambuliaji huyo wa Sweden akishindwa kufunga katika mechi ya jana Jumamosi, Oktoba 04, 2025 dhidi ya West ham United iliyokubali kubamizwa 2-0 kwenye Uwanja wa Emirates, lakini bado alionyesha uwezo na kujituma wakati wote.

Arsenal ilishinda mechi hiyo kupitia mabao ya Declan Rice dakika ya 38, kisha Bukayo Saka akafunga kwa penati dakika ya 67. 

Mikel Arteta amesema hana shaka na Gyokeres, kwani anaamini muda bado upo na ataweza kufanya vizuri na kuisaidia Arsenal kufikia malengo yake msimu huu 2025-2026.

GYO 01

Amesema baada ya mechi hiyo, alimkumbatia Gyokeres kwa kumshukuru kwa kazi nzuri aliyoifanya, huku akiamini alitoa ushirikiano mkubwa kwa wachezaji wenzake licha ya kukosa nafasi kadhaa za kufunga mabao. 

"Nilimkumbatia tu na kumshukuru kwa sababu juhudi anazionyesha ni za ajabu kwa timu.. Kweli, siwezi kuelewa kwanini hakufunga bao jana."  

Arsenal ilimsajili Gyokeres kutoka Sporting CP kwa ada ya pauni 63.5 milioni, wakati wa majira ya joto. Amefunga mabao matatu katika mechi 10 za mashindano yote msimu huu.  

GYO 02

Wakati huohuo, Arteta ameonyesha fahari yake baada ya ushindi wa wa 2-0 dhidi ya West Ham United iliyokuwa ugenini kaskazini mwa jijini London jana Jumamosi.

Arteta amesema: "Mechi mbili zilizopita zimekuwa muhimu sana kwetu. Mechi ya Newcastle ilikuwa na mambo mengi lakini tulipambana na tulishinda, kisha tumekutana na West Ham United, nao tumefanikiwa kuwafunga, hili ni jambo zuri sana na lenye umuhimu kwenye kikosi changu kuelekea mapengo tuliyojiwekea msimu huu."  

Ameongeza: "Niliwaambia wachezaji wangu mechi zote dhidi ya Newcastle United na West Ham United ilikuwa ni fursa kubwa, tumekuwa na mechi ngumu sana tangu mwanzo wa msimu. Bado timu inafanya vizuri, inacheza kwa ustadi, inashinda kwa kuonyesha ufanisi wa hali ya juu bila kupoteza. Limekuwa jambo jema sana kwa timu yetu kwenda mapumziko ya kimataifa ikiwa na hali kama hii."  

GYO 03

Arsenal inaingia kwenye mapumziko ya kimataifa ikiwa kwenye nafasi ya juu katika msimamo wa Ligi ya EPL ikiwa na pointi 16, ikifuatiwa na Liverpool yenye point 15.