Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Dah! Manchester United yaporomoka kiuchumi

MAN 01

Muktasari:

  • Licha ya mapato yao kuongezeka kwa Pauni 40 milioni, uongozi wa Sir Jim Ratcliffe na kundi la Ineos, umeshuhudia klabu hiyo ikishuka hadi nafasi ya chini zaidi kuwahi kufika kwenye jedwali la mapato.

MANCHESTER, ENGLAND: MANCHESTER UNITED imeshuka hadi nafasi ya nane kwenye orodha ya klabu zenye mapato makubwa zaidi duniani.

Licha ya mapato yao kuongezeka kwa Pauni 40 milioni, uongozi wa Sir Jim Ratcliffe na kundi la Ineos, umeshuhudia klabu hiyo ikishuka hadi nafasi ya chini zaidi kuwahi kufika kwenye jedwali la mapato.

Takwimu za hivi karibuni zilizokusanywa na wataalamu wa masuala ya fedha za soka wa Deloitte zinaonyesha Man United wako nyuma ya Liverpool, Manchester City na Arsenal, hivyo kushika nafasi ya nne kwenye orodha ya timu zenye mapato makubwa kwa upande wa  Ligi Kuu England.

Mapato ya jumla ya Man United kutokana na viingilio vya mashabiki uwanjani, haki za matangazo na mikataba ya kibiashara yaliongezeka kutoka Pauni 653 milioni msimu wa 2023-24 hadi Pauni 692 milioni msimu uliopita.

Hata hivyo, kumaliza ligi nafasi ya 15 kulichangia kupungua kwa mapato ya matangazo kwa Pauni 45 milioni.

Man United ambayo imewahi kuwa kileleni mwa orodha hiyo miaka ya nyuma, imeshuka nafasi nne ikilinganishwa na mwaka jana.

MAN 02

Hii ni mara ya kwanza kwa klabu hiyo yenye maskani yake Old Trafford kutoka nje ya tano bora katika miaka 29 tangu orodha ya Deloitte Money League ilipoanza kutolewa.

Kwa kuwa Man United imecheza mechi 20 tu za nyumbani msimu huu baada ya kutolewa mapema kwenye mashindano yote mawili ya vikombe vya ndani, inatarajiwa kupoteza takribani Pauni 85 milioni kutokana na kupungua kwa idadi ya mechi.

Tim Bridge wa Deloitte alisema: “Kama ungerudi nyuma miaka 10 au 15 na kuangalia mapato ya Manchester United siku za mechi, walikuwa ndio wanaongoza. Uwezo wao wa kuzalisha mapato makubwa, ulikuwa kipimo ambacho kila klabu ilikiangalia. Sidhani kama hali hiyo bado ipo."

“Fursa bado ipo kwa Manchester United. Bila shaka bado ni moja ya chapa kubwa zaidi za soka duniani na inaweza kutumika kikamilifu kuzalisha mapato makubwa."

MAN 03

Kwa upande mwingine, Liverpool baada ya msimu wao wa ubingwa chini ya Arne Slot, mapato yao yameongezeka kwa Pauni 106 milioni hadi Pauni 729 milioni na sasa imeshika nafasi ya tano kwenye orodha hiyo.

Manchester City pia ilipata pigo kidogo, mapato yao yakishuka kwa Pauni 7 milioni wakipata Pauni 723 milioni kutoka Pauni 730 milioni, hali iliyowafanya kushuka kutoka nafasi ya pili mwaka jana hadi ya sita kwa sasa.

Hiyo imetokea baada ya kumaliza ligi nafasi ya tatu na kutolewa kwenye hatua ya 16 bora ya Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu uliopita.

Arsenal, imepanda kutoka nafasi ya 10 hadi ya saba, mapato yao yakiongezeka karibu kwa asilimia 15 kutoka Pauni 624 milioni hadi Pauni 717 milioni ikiwa ni baada ya kufika nusu fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya na kupata takribani Pauni 99 milioni  kutokana na zawadi za Uefa.

Liverpool ndiyo klabu pekee ya Ligi Kuu England iliyo kwenye tano bora ya mapato, huku Real Madrid ikiwa ya kwanza kuvunja rekodi ya kufikisha zaidi ya Pauni 1 bilioni ikifuatiwa na Barcelona, Bayern Munich na PSG.

Takwimu hizo pia zinaonyesha baadhi ya timu zilifaidika na mfumo mpya wa Ligi ya Mabingwa Ulaya na mikataba mipya ya matangazo ya televisheni iliyoanzishwa msimu uliopita.

Tottenham Hotspur, ambayo bado wako nafasi ya tisa, iliona mapato yao yakiongezeka kwa Pauni  52 milioni kutoka Pauni 536 hadi Pauni 587 milioni, Chelsea ambayo imeshika nafasi ya 10, ilikusanya jumla ya mapato ya pauni 510 milioni.

MAN 04

Vilevile, Bridge aliongeza:"Matokeo ya uwanjani bado ndiyo sababu kuu inayofanya klabu kupanda hadi ngazi za juu za orodha hii."


MAPATO YA KLABU 20 MWAKA 2025

1. Real Madrid                            Pauni 1 bilioni

2. FC Barcelona                         Pauni 974.8 mil

3. Bayern Munich             Pauni 860.6 mil

4. Paris Saint-Germain              Pauni 837 mil

5. Liverpool                     Pauni 836.1 mil

6. Manchester City          Pauni 829.3 mil

7. Arsenal                       Pauni 821.7 mil

8. Manchester United                Pauni 793.1 mil

9. Tottenham Hotspur               Pauni 672.2 mil

10. Chelsea                      Pauni 584.1 mil

11. Inter Milan                            Pauni 537.5 mil

12. Borussia Dortmund              Pauni 531.3 mil

13. Atlético de Madrid                Pauni 454.5 mil

14. Aston Villa                            Pauni 450.2 mil

15. AC Milan                     Pauni 410.4 mil

16. Juventus                    Pauni 410.7 mil

17. Newcastle United                 Pauni 398.4 mil

18. VFB Stuttgart             Pauni 296.3 mil

19. SL Benfica                           Pauni 283.4 mil

20. West Ham United                Pauni 276 mil