Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Carrick, Solskjaer kuunganisha nguvu Man United

MAN UTD Pict

Muktasari:

  • Makocha hao wawili, ambao tayari waliwahi kuinoa United, wamefanya mazungumzo ya awali yasiyo rasmi na viongozi wa klabu baada ya Ruben Amorim kufukuzwa kazi Jumatatu ya wiki hii.

MANCHESTER, ENGLAND: MANCHESTER United inafikiria  kuwaajiri kwa pamoja Ole Gunnar Solskjaer na Michael Carrick kama makocha wa mpito.

Makocha hao wawili, ambao tayari waliwahi kuinoa United, wamefanya mazungumzo ya awali yasiyo rasmi na viongozi wa klabu baada ya Ruben Amorim kufukuzwa kazi Jumatatu ya wiki hii.

Tovuti ya The Sun, inaeleza kuwa si jambo la kufikirika tena bali ni kweli mashetani wekundu wanaweza kuwachukua malejendi hao ndani ya siku chache zijazo.

Carrick alikuwa sehemu muhimu ya benchi la ufundi la Solskjaer wakati kocha huyo raia wa Norway alipomrithi Jose Mourinho Old Trafford Desemba 2018.

Carrick pamoja na aliyekuwa kocha wa klabu hiyo, Kieran McKenna walikuwa wakisimamia mazoezi mengi ya timu katika kipindi chote cha miaka mitatu ya Solskjaer madarakani, ambacho alianza kama kocha wa muda kabla ya kupewa ajira moja kwa moja.

MAN 01

Baada ya Solskjaer kufukuzwa, Carrick alichukua nafasi yake kama kocha wa mpito kwa siku 10 kati ya Novemba na Desemba 2021, ambapo alishinda mechi mbili na kutoka sare moja kati ya mechi tatu alizoiongoza.

Man United imeanza kufanya mazungumzo zaidi na Solskjaer pamoja na Carrick kabla ya kuamua nani atakuwa kocha wa mpito hadi mwisho wa msimu na ikiwezakana itawachukua wote.

Darren Fletcher, ambaye kwa sasa ni kocha wa kikosi cha vijana chini ya miaka 18 cha United, ataendelea kuiongoza timu kama kocha wa mpito hadi uamuzi wa mwisho utakapofanyika.

Vilevile, kuna uwezekano Fletcher akaruhusiwa kuendelea na nafasi hiyo hadi mwisho wa msimu iwapo matokeo ya mechi mbili zijazo yatakuwa mazuri.

MAN 02

Man United pia ina makocha wengine inaowatazama kwa ajili ya  kuwapa nafasi hiyo ya muda hadi mwisho wa msimu, akiwamo Ruud Van Nistelrooy.

Van Nistelrooy aliiongoza Man United kwa muda baada ya Erik Ten Hag kufukuzwa kazi Oktoba 2024, kabla ya Amorim kuchukua mikoba mwezi uliofuata.

Mshambuliaji huyo nguli wa zamani wa Man United aliteuliwa kuwa kocha msaidizi wa Ten Hag majira ya kiangazi mwaka 2024, kama sehemu ya mabadiliko ya benchi la ufundi.

Hata hivyo, Amorim baadaye alishindwa kumpatia nafasi Van Nistelrooy katika benchi lake la ufundi.

Baada ya kuondoka Man United, raia huyo wa Uholanzi aliifundisha Leicester City kuanzia Novemba 2024 hadi Juni 2025, kipindi ambacho klabu hiyo ilishuka daraja kutoka Ligi Kuu England. Kwa sasa hana timu,

MAN 03

Carrick amekuwa bila kazi tangu alipofukuzwa na klabu ya Championship, Middlesbrough, Juni mwaka jana baada ya kuitumikia kwa miaka miwili na nusu.

Solskjaer naye alifukuzwa na klabu ya Uturuki, Besiktas Agosti mwaka jana baada ya kuhudumu  kwa miezi minane tu.

Kocha wa Crystal Palace Oliver Glasner na aliyekuwa kocha wa Brighton Roberto De Zerbi  ambaye kwa sasa yupo Marseille wanatajwa kuwa miongoni mwa wale wanaoweza kupewa ajira ya kudumu na timu hiyo.