Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Dada amtabiria mdogo wake Ballon d’Or

UTABIRI Pict

Muktasari:

  • Temwa kwenye mashindano ya WAFCON 2026 alionyesha kiwango bora akiibuka mfungaji bora akiweka kambani mabao matano na kuwapiku Barbra Banda wa Zambia, Marie Ngah Manga wa Cameroon na In’ Konan wa Ivory Coast.

NAHODHA wa timu ya Taifa ya Malawi, Tabitha Chawinga, anaamini mshambuliaji wa Kansas City, Temwa Chawinga ambaye ni mdogo wake ana nafasi kubwa ya kushinda tuzo ya Ballon d’Or ya Wanawake mwaka huu baada ya kuwa na msimu bora katika Ligi ya Wanawake Marekani na kwenye fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (WAFCON) 2026.

Temwa kwenye mashindano ya WAFCON 2026 alionyesha kiwango bora akiibuka mfungaji bora akiweka kambani mabao matano na kuwapiku Barbra Banda wa Zambia, Marie Ngah Manga wa Cameroon na In’ Konan wa Ivory Coast.

Mbali na mafanikio hayo akiwa na timu ya taifa, lakini pia kwenye klabu aliibuka mfungaji bora wa Ligi ya Wanawake Marekani akiweka kambani mabao 15 na asisti tatu kwenye mechi 23, takwimu zilizomfanya achukue Tuzo ya Mchezaji Bora wa msimu mara mbili mfululizo.

UTAB 01

Tabitha anayekipiga Lyon ya Ligi Kuu ya Wanawake nchini Ufaransa, amesema mafaniko ya mdogo wake huyo kuanzia ngazi ya klabu na timu ya taifa yanatosha kumpa tuzo ya Ballon d’Or.

“Ninaamini kwa mdogo wangu, yeye ni supastaa wangu. Ni mmoja wa wachezaji bora zaidi duniani,”  amesema Tabitha.

Ameongeza kuwa, Temwa hastahili kuishia kwenye tuzo ya Kiatu cha Dhahabu pekee, bali anaweza pia kutwaa tuzo kubwa zaidi barani Afrika na hata kufikia hatua ya kushinda Ballon d’Or.

“Sio Kiatu cha Dhahabu tu. Ninaamini atakuwa mchezaji bora Afrika na labda hata kushinda Ballon d’Or. Ni supastaa. Ukiangalia kipaji chake, bidii yake na namna alivyofanya, namheshimu sana,” amesema.

UTAB 02

Tabitha pia alieleza kuwa wakati yeye alipokuwa mdogo hakupata nafasi ya kufikia hatua ya kushindania Ballon d’Or, lakini sasa anatamani kuona mdogo wake akifikia mafanikio hayo.

“Nilipokuwa mdogo sikuwa na nafasi ya kushinda Ballon d’Or, lakini ninatamani mdogo wangu ashinde. Ninaamini kwake,”  amesema.

Nyota hao wawili wamechangia kwa kiasi kikubwa mafanikio ya Malawi kwenye mashindano ya WAFCON 2026 ambapo licha ya kushindwa kubeba taji hilo lakini ilionyesha kiwango bora.

Madada hao waliipeleka Malawi fainali ya WAFCON 2026 kwa mara ya kwanza katika historia ya mashindano hayo ambayo tangu yaanzishwe mwaka 1991 hakuna timu iliyowahi kushiriki mara ya kwanza ikafika hatua hiyo.

Licha ya kutokuwa na matarajio makubwa kutoka kwa wengi, Malawi ilifanya mambo makubwa kwa kushinda dhidi ya Nigeria bingwa mara nyingi wa mashindano hayo, Misri, Ghana na Algeria kabla ya kufika fainali. Temwa alikuwa mhimili wa safari hiyo, akifunga mabao mawili dhidi ya Nigeria, bao moja dhidi ya Misri, akasawazisha dhidi ya Ghana na kufunga bao la pili katika ushindi wa 3-1 dhidi ya Algeria kwenye nusu fainali. Tabitha amesema mafanikio hayo ni kama muujiza kwa Malawi, akidai hata waandishi wa habari hawakuipa nafasi kubwa ya kufika fainali. “Hii ilikuwa mara ya kwanza kwa Malawi kushiriki mashindano haya. Huu ni muujiza kwa Scorchers. Hata ninyi waandishi wa habari hamkutupa nafasi. Mlitupa asilimia mbili tu za kufika fainali, lakini Mungu aliwashangaza kila mtu,† amesema.

UTAB 03

Malawi ilianza kuonyesha dalili mapema baada ya kuichakaza Nigeria mabao 3-2 kwenye mechi ya kwanza ya kundi C. Ikashinda tena mabao 3-1 dhidi ya Misri na kupoteza mechi ya mwisho dhidi ya Zambia kwa bao 1-0 kisha ikamaliza kileleni mwa kundi hilo na kufuzu robo fainali.

Kilichoendeleza kuwashangaza mashabiki timu hiyo ikaitoa Ghana kwenye mechi ya robo fainali kwa mabao 2-1 kabla ya kufika nusu fainali ambako iliondoa Algeria na kushinda 3-1.

Ilipotinga fainali Malawi ilikumbana na kipigo cha mabao 3-0 kutoka kwa Cameroon katika fainali, ambapo Marie Ngah Manga alifunga mabao mawili huku Naomi Eto akifunga bao jingine kwa shuti zuri. Pamoja na kipigo hicho, Tabitha anaamini Malawi inapaswa kutamba kutokana na safari yake kwenye mashindano ikikutana na kundi gumu lenye timu kubwa lakini ikafanikiwa kutoboa.