Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mitego ya Jux huko Nigeria ni marudio tu!

JUX Pict

Muktasari:

  • Jambo hilo limemfanya Jux kuwa karibu na hata kukutana mara kwa mara na mastaa wengi wakubwa wa muziki Nigeria, hatua inayoweza kuwa fursa kwake kwa kushirikiana nao katika nyimbo zao.

Kwa sasa Jux anachukuliwa kama mwanamuziki wa Bongo Fleva mwenye nguvu kubwa zaidi ya ushawishi katika soko la muziki la Nigeria kutokana na kumuoa binti maarufu nchini humo ambaye ni Priscilla.

Jambo hilo limemfanya Jux kuwa karibu na hata kukutana mara kwa mara na mastaa wengi wakubwa wa muziki Nigeria, hatua inayoweza kuwa fursa kwake kwa kushirikiana nao katika nyimbo zao.

Wikiendi iliyopita, Jux alitumbuiza jijini London, Uingereza katika show ya staa wa Nigeria, Stonebwoy iliyofanyika OVO Arena Wembley, huku ikipambwa na mastaa wengine wa nchi hiyo akiwemo Tiwa Savage.

Hata hivyo, ikiwa ni zaidi ya miaka miwili tangu Jux ajitambulishe katika tasnia hiyo Nigeria kupitia uhusiano wake na Priscilla, fursa alizokutana nazo na kuzitumia tayari kuna wasanii wengine wa Bongo Fleva walishazitumia pia!.

JU 01

Mathalan, wanamuziki wa huko aliyoshirikiana nao na hata ambao wanatajwa kuwa katika mipango yake, si wageni katika Bongo Fleva kwani walishapiga kolabo na wasanii wa hapa.

Jux alimshirikisha Phyno wa Nigeria katika wimbo wake maarufu, God Design (2025) uliotayarishwa na Foxx Made, huku katika video iliyosimamiwa na Director Fole X akiigiza pamoja na mkewe Priscilla.

Wimbo huo uliokuja kujumuishaa katika Extended Playlist (EP) yake ya kwanza, A Day To Remember (2025) yenye nyimbo saba, ndio ilikuwa kolabo ya kwanza kubwa ya Jux dhidi ya mwanamuziki wa Nigeria.

Hata hivyo, Phyno ambaye ni rapa, awali alishafanya kazi na staa wa Bongofleva kutokea Next Level Music (NLM), Rayvanny ambaye alimshirikisha katika wimbo wake, Slow (2019) uliotayarishwa na S2kizzy na Laizer.

Hivi karibuni Jux ameonekana akiwa pamoja na Tiwa Savage, Mr. P (Peter wa P-Square) na Davido, iwapo Jux ana mpango wa kushirikiana nao kimuziki, bado simulizi itasalia kuwa ile ile - anarudia kitu ambacho tayari wenzake wamefanya ingawa si jambo baya.

Je, ni kwa namna gani Jux atakuwa anafanya marudio kwa Tiwa Savage, Mr. P, na Davido?, tunaenda kuangazia hilo kwa ufupi.

JU 05

1. Tiwa Savage

Albamu ya tatu na ya mwisho kutoka kwa Diamond Platnumz, A Boy From Tandale (2018), ilishirikisha wanamuziki wengi wakubwa kutokea Afrika, na miongoni mwao ni Tiwa Savage ambaye ni msanii wa kwanza wa kike Afrika kushinda tuzo ya MTV EMAs.

Tiwa Savage alisikika katika wimbo wa Diamond uitwao Fire (2017) uliotayarishwa na Laizer, hivyo kama Jux atashirikiana na Tiwa Savage, basi atakuwa amerudia jambo ambalo Diamond alilifanya zaidi ya miaka tisa iliyopita.

Utakumbuka Tiwa Savage alivuma kimuziki baada ya kurejea Nigeria mwaka 2012 na kusaini Mavin Records, lebo inayomilikiwa na Don Jazzy na mwaka uliofuatia alitoa albamu ya kwanza, Once Upon a Time (2013) ikiwa na wimbo wake maarufu, Kele Kele Love.

JU 03

2. Mr. P (P-Square)

Mwanamuziki huyo amefanya kazi na mastaa wa Bongo Fleva akiwa ndani ya kundi la P-Square, na vilevile akiwa pekee yake kama solo (Mr. P) baada ya kundi lao kusambaratika kufuatia migogoro ya kibiashara na kifamilia ambayo imekosa suluhisho.

P-Square walishirikiana na AY katika ngoma yake, Freeze (2008) iliyotayarishwa na Hermy B kutokea B'Hitz, kisha baadaye wakasikika katika wimbo wa Diamond Platnumz, Kidogo (2016) uliotayarishwa na Shirko kutokea Kenya huku V-Teck wa Nigeria na Laizer wakifanya mixing.

Baada ya P-Square kuvunjika, Mr. P (Peter ) alisikika katika wimbo wa Vanessa Mdee, Kisela (2017) kutoka katika mikono ya EKelly wa Nigeria ambaye pia ndiye alitengeneza wimbo wa Vanessa, Cash Madame (2016).

Pacha mwenzake Mr. P, Paul (Rudeboy) alikuja kushirikishwa na Alikiba katika wimbo, Salute (2021) uliyotayarishwa na Yogo Beats, huku video yake ikifanyika Lagos na director wa huko, Paul Gambit.

Hivyo kutoka mwaka 2008 ambapo P-Square walisikika katika Bongofleva kwa mara ya kwanza hadi sasa, ni miaka 18, kwa hiyo endapo Jux atafanya kazi na msanii wa kundi hilo, ni sawa tu na kusema anarudia tukio la miaka 18 iliyopita!.

JU 02

3. Davido

Staa huyu wa Afrobeats aliyevuma zaidi Afrika kwa mara ya kwanza kupitia wimbo wake, Dami Duro (2011), tayari ameshirikiana na wanamuziki watatu wa Bongofleva ambapo kolabo ya kwanza ilitoka miaka 13 iliyopita.

Davido ameshirikishwa na Diamond Platnumz (My Number Remix - 2013), Joh Makini (Kata Leta - 2017), na Dayna Nyange (Elo - 2021), kolabo ambazo kila moja ilifanya vizuri kwa nafasi yake.

Hivyo Jux kushirikiana na Davido haitakuwa habari mpya Bongo, labda akifanya hivyo kwa Wizkid, Ayra Starr au Tems ambaye ni mshindi wa tuzo za Grammy mara mbili. Mastaa hawa bado hawajashirikishwa na mwanamuziki yeyote wa Bongo Fleva hadi sasa.