Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Cameroon yatwaa taji la Kwanza WAFCON

CAMEROON Pict

Muktasari:

  • Marie Ngah alikuwa shujaa wa Cameroon baada ya kufunga mabao mawili, huku Naomi Ndjoah Eto akifunga bao lingine na kuisaidia timu hiyo kupata ushindi ulioandika historia nyingine kwa taifa hilo.

TIMU ya Taifa ya Cameroon imeandika historia  katika soka la wanawake Afrika baada ya kutwaa kwa mara ya kwanza taji la Kombe la Mataifa ya Afrika kwa Wanawake (WAFCON) 2026, kufuatia ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Malawi katika mchezo wa fainali uliochezwa kwenye Uwanja wa Moulay El Hassan, Rabat.

Marie Ngah alikuwa shujaa wa Cameroon baada ya kufunga mabao mawili, huku Naomi Ndjoah Eto akifunga bao lingine na kuisaidia timu hiyo kupata ushindi ulioandika historia nyingine kwa taifa hilo.

Ngah alianza kuandika historia hiyo dakika ya 20 baada ya kuipatia Cameroon bao la kuongoza, kabla ya Ndjoah Eto kuongeza la pili dakika ya 30 akimalizia pasi ya Myriam Nyadjou.

Ushindi huo umeifanya Cameroon kuwa taifa la nne kutwaa WAFCON, ikiungana na Nigeria, Equatorial Guinea na Afrika Kusini katika orodha ya mabingwa wa michuano hiyo.

Timu hiyo imevunja mwiko wa fainali nne zilizopita ambazo hazijawahi kutwaa taji ikiishia kuchapwa na bingwa mtetezi Nigeria.

Cameroon ilipoteza fainali hizo mwaka 1991 ikapoteza kwa mabao 2-0, mwaka 2004 ikapoteza tena kwa mabao 5-0, mwaka 2014 ikapoteza tena mabao 2-0 na mwaka 2016 ikadungwa bao 1-0.

Timu hiyo ilianza kwa ushindi wa mabao mabao 2-1 dhidi ya Mali, ikashinda 1-0 dhidi ya Ghana na kumaliza hatua ya makundi kwa sare ya 1-1 dhidi ya Cape Verde.

Katika robo fainali, Cameroon iliiondoa Nigeria, mabingwa mara 10, kwa ushindi wa bao 1-0. Kisha kwenye nusu fainali iliitoa Morocco kwa mikwaju ya penalti 3-1 baada ya dakika 90 kumalizika bila bao.

Kufikia fainali, Cameroon ilikuwa haijaruhusu bao lolote katika hatua ya mtoano, jambo lililoendelea katika mchezo wa fainali licha ya Malawi kuwa miongoni mwa timu zilizokuwa na safu hatari zaidi ya ushambuliaji katika mashindano hayo.

Malawi, ambayo ilikuwa imeshiriki WAFCON kwa mara ya kwanza, iliingia katika fainali ikiwa na rekodi bora ya kufunga mabao 12. Ndugu wawili Temwa na Tabitha Chawinga wamechangia kwa kiasi kikubwa historia ya taifa hilo.

Hata hivyo, Cameroon ilitumia uzoefu, nidhamu ya ulinzi na umaliziaji mzuri kuwadhibiti Scorchers. Malawi ilijaribu kufanya mabadiliko kipindi cha pili ili kurejea mchezoni, lakini haikuweza kuvunja ngome ya Cameroon.

Kwa upande wa Malawi, licha ya kupoteza fainali, safari yao imebaki kuwa ya kihistoria. Ilikuwa timu ya kwanza kutoka Kusini mwa Afrika kushiriki WAFCON kwa mara ya kwanza na kufika fainali.