Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Simba inavyojichongea kwa Yanga kimtindo

KUJICHONGEA Pict


SIMBA SC imeanza vyema kampeni zake katika Ligi Kuu Bara 2026-2027 baada ya kushinda mechi zote mbili ilizocheza, huku moja ya dosari inayokigharimu kikosi hicho kwa sasa ni kutokana na wachezaji wake wawili kuonyeshwa kadi nyekundu.


Timu hiyo ilianza msimu wa 2026-2027 kwa ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Kagera Sugar, Agosti 16, 2026, huku ikishuhudia beki wa kulia wa kikosi hicho, David Kameta ‘Duchu’ akionyeshwa kadi nyekundu baada ya kumchezea vibaya, David Luhende.


Baada ya hapo, timu hiyo ikaifunga Pamba Jiji mabao 2-1, Agosti 19, 2026, huku pia ikishuhudiwa nyota wa kikosi hicho, Ibraheem Jabaar raia wa Nigeria akionyeshwa kadi nyekundu kwa kumpiga kiwiko, Abdulkarim Yunus.

KUJICH 01

Kwa misimu ya hivi karibuni, mara ya mwisho kwa wachezaji wa Simba kuonyeshwa kadi nyekundu zaidi ya mbili msimu mmoja, ubingwa wa Ligi Kuu Bara ulichukuliwa na watani zao wa jadi Yanga, jambo ambalo linasubiriwa kuona msimu wa 2026-2027 hali itakuwaje.

Kwa msimu wa 2015-2016, ilishuhudiwa wachezaji wa tatu wa Simba wakionyeshwa kadi nyekundu, ambao ni mabeki, Abdi Banda, Hassan Kessy na kiungo mshambuliaji, Ibrahim Ajibu, kisha Yanga kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu Bara ikiwa na pointi 73.

Katika msimu huo, Simba ilimaliza ya tatu na pointi 62, baada ya kushinda mechi 19, sare tano na kupoteza sita kati ya 30, nyuma ya Azam FC iliyomaliza ya pili na pointi zake 64 na mabingwa Yanga iliyokuwa na 73.

KUJICH 02

Banda alionyeshwa kadi nyekundu katika mechi dhidi ya Yanga iliyopigwa Februari 20, 2016 na kushuhudia kikosi hicho kikipoteza kwa mabao 2-0, yaliyofungwa na Donald Ngoma dakika ya 36 na Amissi Tambwe dakika ya 72.

Kadi nyekundu ya Banda ilitokana na kuonyeshwa kadi ya njano ya pili iliyotokana na kumchezea madhambi, Donald Ngoma na kuigharimu Simba kupoteza mechi hiyo iliyokuwa ya 96, ya ‘Kariakoo Derby’, kati yao ya Ligi Kuu Bara tangu mwaka 1965.

Kwa beki wa kulia, Hassan Kessy, alionyeshwa kadi nyekundu baada ya kumchezea madhambi aliyekuwa mshambuliaji wa Toto Africans, Edward Christopher ‘Edo’ na Simba kuchapwa bao 1-0, lililofungwa na Waziri Junior Shentembo, Aprili 17, 2016.

KUJICH 03

Kwa Ajibu, alionyeshwa kadi nyekundu baada ya kumchezea madhambi, Hassan Kabunda katika mechi ya Simba iliyochapwa bao 1-0, dhidi ya Mwadui FC, Mei 7, 2016, kwa bao lililofungwa na aliyekuwa winga wa kikosi hicho, Jamal Mnyate.

Kwa maana hiyo, kwa misimu ya hivi karibuni, wachezaji zaidi ya wawili wa Simba walioonyeshwa kadi nyekundu katika msimu mmoja walikosa ubingwa wa Ligi Kuu Bara, kama ilivyotokea msimu wa 2015-2016, ulivyoenda kwa watani zao wa jadi, Yanga.