Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Dabo amtaka Sibo amrudishie jezi ya Bellingham

Muktasari:

  • Dabo, ambaye pia ni mmiliki wa Dabo Soccer Academy, amesema Bellingham alimkabidhi Sibo jezi yake ili apewe baada ya mchezo huo uliochezwa Boston, Marekani.

ACCRA, Ghana: MUIGIZAJI maarufu wa Ghana, Yaw Dabo, amemtaka kiungo wa Black Stars, Kwasi Sibo, kumrudishia jezi ya Jude Bellingham ambayo ilipaswa kufikishwa kwake, wiki saba baada ya Ghana kucheza dhidi ya England katika Kombe la Dunia 2026.

Dabo, ambaye pia ni mmiliki wa Dabo Soccer Academy, amesema Bellingham alimkabidhi Sibo jezi yake ili apewe baada ya mchezo huo uliochezwa Boston, Marekani.

Muigizaji huyo alisema baada ya mchezo aliwaomba wachezaji na viongozi wa timu ya taifa ya Ghana kumsaidia kupata jezi ya Bellingham.

Katika video iliyosambaa mitandaoni, Dabo pia alionekana akimuomba nyota wa zamani wa England na Chelsea, John Terry, kumjulisha Bellingham kwamba alikuwa uwanjani.

Baada ya kuzungumza na Sibo baada ya mchezo, kiungo huyo wa zamani wa Real Oviedo alikubali kuichukua jezi hiyo kutoka kwa Bellingham na kumkabidhi Dabo.

Hata hivyo, jezi hiyo haikufika kwa Dabo. Badala yake, muigizaji huyo alidai kumuona Sibo kwenye mitandao ya kijamii akiwa amevaa jezi hiyo.

“Nilikuwa nimewaambia wachezaji wamjulishe Jude Bellingham kwamba nipo uwanjani. Kwa kweli, nilimuona Sibo akiwa amevaa jezi ya Bellingham. Nirudishieni jezi yangu, nasisitiza,” alisema Dabo.

“Sibo ni rafiki yangu mzuri. Nilimwambia amkumbushe Bellingham kuhusu ahadi yake ya kunipa jezi. Alitakiwa tu kuichukua kwa ajili yangu. Aliniambia amemuona Bellingham, na hilo lilikuwa kabla hawajaingia vyumba vya kubadilishia nguo,” aliongeza.

Dabo amesema wachezaji na viongozi wa Black Stars wanaweza kuthibitisha upande wake wa simulizi hilo, akidai aliwaomba wengi wao kumjulisha Bellingham kuhusu uwepo wake uwanjani na kumsaidia kupata jezi hiyo.

“Wachezaji na viongozi wa Black Stars wanaweza kuthibitisha upande wangu wa habari hii. Niliwaambia wengi wao wamjulishe Bellingham kwamba nipo na wamchukulie jezi hiyo kwa ajili yangu. Inaonekana Sibo aliichukua na kuihifadhi mwenyewe,” alisema Dabo.

Dabo na Bellingham wamekuwa marafiki tangu walipokutana kwa mara ya kwanza nchini Ujerumani wakati nyota huyo wa England alipokuwa akiichezea Borussia Dortmund.

Wakati huohuo, Sibo anatarajiwa kuhamia klabu nyingine katika dirisha hili la usajili baada ya kufanya vizuri kwenye Kombe la Dunia lililofanyika Amerika Kaskazini.