Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Camavinga atua katika anga la Liverpool, dau kumvuta latajwa

FUNUNU Pict

Muktasari:

  • Kwa sasa Camavinga ni miongoni mwa wachezaji muhimu wa kikosi cha Xabi Alonso akitumika kama kiraka katika nafasi mbalimbali.

LIVERPOOL inaandaa ofa ya Pauni 52.5 milioni ili kumsajili kiungo wa Real Madrid, Eduardo Camavinga, 23.

Kwa sasa Camavinga ni miongoni mwa wachezaji muhimu wa kikosi cha Xabi Alonso akitumika kama kiraka katika nafasi mbalimbali.

Inaelezwa Liverpool inataka kufanya mabadiliko makubwa eneo la kiungo kutokana na kiwango kibovu ambacho kikosi kimeonyesha msimu huu.

Hata hivyo, Real Madrid inadaiwa kuwa haitakuwa tayari kumuuza kiungo huyo ingawa ikiwekewa ofa nono inaweza kufikiria.

Katika eneo la kiungo Real Madrid tayari kuna Aurelien Tchouameni, Federico Valverde na Jude Bellingham, hivyo mpango wa kumuuza staa huyo hauonekani kawa utaathiri chochote.Taarifa zinadai Real Madrid  inafanya mazungumzo kuhusu mkataba mpya na wawakilishi wa Camavinga lakini yanaweza kusimama baada ya Liverpool kuonyesha nia ya kumsajili. Mkataba wake unaisha 2029.


Iliman Ndiaye
EVERTON haitakuwa tayari kupokea au kujadili ofa yoyote inayomhusu mshambuliaji wa kimataifa wa Senegal, Iliman Ndiaye, 25, ambaye anahitajika na vigogo wengi England ikiwemo Liverpool. Ndiaye ni miongoni mwa wachezaji tegemeo katika kikosi cha Everton na mabosi wa timu hiyo wanaamini itakuwa vigumu kupata mbadala wake ikiwa itamuuza kwa sababu ya changamoto ya masuala ya kifedha. Mkataba wa wa sasa wa Ndiaye unatarajiwa kumalizika 2029.


Antoine Semenyo
MANCHESTER City inajadili namna ya kulipa Pauni 65 milioni kwa ajili ya kuvunja mkataba wa mshambuliaji wa Bournemouth na timu ya taifa ya Ghana, Antoine Semenyo, 25. Semenyo amekuwa miongoni mwa wachezaji bora wa Bournemouth tangu msimu uliopita. Inaelezwa katika mkataba wake kuna kipengele ambacho kinamruhusu kuondoka ikiwa timu inayomhitaji italipa Pauni 65 milioni. Pep Guardiola anamwonan kama mbadala sahihi wa Erling Haaland.


Rodrigo Mendoza
MKURUGENZI wa Michezo wa Arsenal, Andrea Beta, anaongoza mchakato wa mazungumzo ya kumsajili kiungo wa Elche na timu ya taifa ya Hispania, Rodrigo Mendoza, 20. Arsenal ipo tayari kulipa zaidi ya Pauni 15  milioni ili kumpata Mendoza lakini Elche inahitaji ofa inayoanzia Pauni 20 milioni ili kumuuza staa huyo ambaye mkataba wake wa sasa unatarajiwa kumalizika 2028.


Federico Valverde
MANCHESTER United inaonekana kudhamiria kumsajili kiungo wa Real Madrid na timu ya taifa Uruguay, Federico Valverde, 27. Inaelezwa inatamani huduma ya Vakverde ambaye anadaiwa kutokuwa na uhusiano mzuri na kocha Xabi Alonso na anatamani kuondoka kwenda sehemu ambayo anaamini atakuwa na furaha. Akiwa Real Madrid msimu uliopita alicheza mechi 50 za michuano yote.


Guendouzi
SUNDERLAND imeanza mazungumzo na Lazio kwa ajili ya kumsajili kiungo wa timu hiyo na Ufaransa, Matteo Guendouzi, 26, katika dirisha lijalo. Hata hivyo kuna upinzani mkali kutoka kwa Newcastle United ambayo inahitaji huduma yake. Taarifa zinaeleza Sunderland inataka kuongeza nguvu kwenye eneo la kiungo katika jitihada za kupambania nafasi za juu ili kufuzu kucheza michuano ya kimataifa msimu ujao. Lazio inahitaji Pauni 20 milioni.


Elliot Anderson
MANCHESTER City inataka kulipa Pauni 60 milioni Nottingham Forest  kumsajili staa wa timu ya taifa ya England, Elliot Anderson, 23, katika dirisha lijalo. Inaelezwa Man City inataka kumfanya kuwa miongoni mwa vipaumbele kuelekea dirisha la usajili la majira ya baridi mwakani. Taarifa zinaeleza kuwa benchi la ufundi la Man City linamhusudu sana Anderson kuliko Adam Wharton.


Marcus Rashford
BARCELONA inaonekana kuvutiwa sana na mshambuliaji wa Manchester United anayecheza katika kikosi hicho kwa mkopo, Marcus Rashford 28 na inaongeza kasi ili kumsainisha mkataba wa kusalia katika kikosi chake. Ili kumsainisha mkataba wa moja kwa moja Barca inatakiwa kulipa zaidi ya Pauni 50 milioni. Pia mkurugenzi wa michezo wa Barcelona, Deco de Souza, amemkubali.