Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Arsenal, Liverpool zaendelea kumnyatia Rodrygo

Muktasari:

  • Rodrygo, ambaye msimu uliopita alifunga mabao 14 na kutoa asisti 11 amekuwa akihusishwa kuondoka Madrid kwa sababu hapati nafasi ya kutosha katika kikosi cha kwanza na hana furaha pia katika timu hiyo.

LIVERPOOL na Arsenal zinajiandaa kutuma ofa Real Madrid dirisha la usajili la Januari ili kumsajili mshambuliaji wa kimataifa wa Brazil, Rodrygo, 24.

Rodrygo, ambaye msimu uliopita alifunga mabao 14 na kutoa asisti 11 amekuwa akihusishwa kuondoka Madrid kwa sababu hapati nafasi ya kutosha katika kikosi cha kwanza na hana furaha pia katika timu hiyo.

Real Madrid ipo tayari kumuuza, lakini inahitaji kiasi kisichopungua Euro 100 milioni.

Mabosi wa Liverpool wanamuona kuwa mbadala wa muda mrefu wa Mohamed Salah ambaye anatarajiwa kuondoka mwisho wa msimu huu kwenda Saudi Arabia.

Arsenal inavutiwa na uwezo wake wa kucheza nafasi nyingi za ushambuliaji, lakini changamoto inaonekana kuwa ni kiasi cha pesa inachohitaji Real Madrid.

Timu nyingi zinaonekana kuwa tayari kulipa chini ya Euro 70 milioni ili kumnunua staa huyu, lakini Madrid imeendelea kushikilia msimamo wa kuhitaji Euro 100.


Mohamed Salah

TTIMU za Ligi Kuu Saudi Arabia zinaendelea kufuatilia kwa makini maendeleo ya mshambuliaji wa Liverpool, Mohamed Salah, 33, ambaye anaonekana kutokuwa na furaha kwenye kikosi cha majogoo. Salah anawindwa na Al-Ittihad, Al-Hilal na Al-Ahli, ambazo zipo tayari kulipa Pauni 150 milioni ili kumnunua. Mkataba wa Liverpool na Salah unatarajiwa kumalizika 2027. Msimu huu amecheza mechi 18 za michuano yote na kufunga mabao matano.


Marc Guehi

LIVEPPOOL imefungua tena mazungumzo na mawakala wa beki wa Crystal Palace na England, Marc Guehi, 25, wanaotaka kujaribu kumsajili dirisha la usajili la Januari baada ya kufeli kumpata lililopita. Mkataba wa sasa wa Guehi unatajiwa kumalizika mwisho wa msimu huu na Liverpool inamwangalia kama mbadala wa Ibrahim Konate ambaye pia mkataba wake unamalizika mwisho wa msimu lakini amegoma kusaini mpya.


Christos Mouzakitis

MANCHESTER United inafuatilia kiungo wa Olympiacos na timu ya taifa ya Ugiriki, Christos Mouzakitis ambaye  Real Madrid nayo inamnyemelea kimyakimya ikiwa tayari kutoa hadi Pauni 25 milioni kwa ajili ya nyota huyo mwenye umri wa miaka 18. Mouzakitis amekuwa gumzo Ulaya kutokana na uwezo wake wa kupiga pasi ndefu, kumiliki mpira na kushambulia.


Marcus Rashford

BARCELONA haijafanya uamuzi wa mwisho juu ya kumsainisha mkataba wa moja kwa moja mshambuliaji wa Manchester United, Marcus Rashford, 28, ambaye anaichezea kwa mkopo. Rashford ameonekana kurejea kwenye ubora akifunga mabao manne na kuasisti mara mbili katika mechi 11 za ligi. Kutofanya uamuzi kwa Barca kunasababishwa na hali  ya kiuchumi.


Tiago Gabriel

wEST Ham United na Brentford zinajiandaa kuwasilisha ofa katika dirisha la usajili la  Januari kwa ajili ya beki wa kati wa Lecce, Tiago Gabriel, 20, lakini zinakumbana na ushindani kutoka kwa Juventus. Mkataba wa sasa wa Gabriel unatarajiwa kumalizika 2027, lakini kuna kipengele kinachowezesha Lecce na wawakilishi wa staa huyo kuurefusha kwa miaka miwili zaidi kwa makubaliano.


Guglielmo Vicario

KIPA wa Tottenham Hotspurs, Guglielmo Vicario, 29, anafikiria kuondoka katika dirisha lijalo la majira ya baridi kurudi Italia ambako Inter Milan inahitaji huduma yake. Vicario amecheza mechi 14 za Ligu Kuu England msimu huu na amemaliza nne kati ya hizo bila kuruhusu bao. Inter inamuona kuwa mrithi sahihi wa muda mrefu wa Yann Sommer, hasa baada ya kuonyesha kiwango kizuri.


Ederson

LIVERPOOL imepiga hatua kubwa katika mchakato wa kuwania saini ya kiungo wa Atalanta na Brazil, Ederson, 26, kuelekea dirisha lijalo la majira ya baridi. Mbali ya Liverpool, huduma ya Ederson pia inahitajika na Barcelona ambayo inaonekana kusuasua kutokana na hali ya kiuchumi. Ederson amekuwa kwenye kiwango bora Serie A tangu msimu uliopita. Mkataba wake wa sasa unamalizika 2027.