Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Coventry yamvizia beki wa Chelsea

BEKI Pict

Muktasari:

  • Awali, Chelsea ilikataa ofa kadhaa za kumsajili Acheampong, 20, ikisisitiza kuwa beki huyo aliyelelewa kwenye akademi ya klabu hiyo hayuko kwenye orodha ya wachezaji wanaouzwa.

LONDON, ENGLAND. COVENTRY City imeingia kwenye mbio za kumsajili beki wa Chelsea, Josh Acheampong, huku mabingwa hao wa England sasa wakionekana kuwa tayari kusikiliza ofa kwa ajili ya mchezaji huyo, kwa mujibu wa talkSPORT.

Awali, Chelsea ilikataa ofa kadhaa za kumsajili Acheampong, 20, ikisisitiza kuwa beki huyo aliyelelewa kwenye akademi ya klabu hiyo hayuko kwenye orodha ya wachezaji wanaouzwa.

Klabu hiyo pia ilimchukulia Acheampong kuwa sehemu muhimu ya mipango ya kocha mpya, Xabi Alonso, kuelekea msimu huu.

Hata hivyo, msimamo huo sasa umeanza kubadilika, huku Chelsea ikiwa tayari kutathmini uwezekano wa kumruhusu beki huyo kuondoka iwapo itapokea ofa inayokidhi mahitaji yake.

Coventry, ambayo inataka kuimarisha safu yake ya ulinzi, imeonyesha nia ya kumsajili Acheampong, ambaye amekuwa akipewa nafasi katika kikosi cha kwanza cha Chelsea kutokana na uwezo wake wa kucheza kama beki wa kati na upande wa kulia.

Matarajio ya Coventry kumpata mchezaji huyo sasa yanaongezeka kutokana na Chelsea kuwa tayari kusikiliza ofa, ingawa bado haijafahamika kama klabu hizo zimefikia hatua ya makubaliano.