Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Cooper Flagg aanza mdogomdogo Las Vegas

Muktasari:

  • Japokuwa hakufunga kwa ufanisi, alionyesha ana kitu, kwani katika mchezo huo ambao Mavericks waliichapa Los Angeles Lakers kwa pointi 87-85, Flagg alipiga mashuti 21, akafunga matano, akakosa mara tano aliyojaribu kwa mbali (three-point) na kumaliza mchezo kwa ‘airball’.

LAS VEGAS, MAREKANI: KATIKA Uwanja wa Thomas & Mack jijini Las Vegas, kijana mwenye umri wa miaka 18 tu, Cooper Flagg alicheza mchezo wake wa kwanza katika NBA 2K26 Summer League akiwa na jezi za Dallas Mavericks.

Japokuwa hakufunga kwa ufanisi, alionyesha ana kitu, kwani katika mchezo huo ambao Mavericks waliichapa Los Angeles Lakers kwa pointi 87-85, Flagg alipiga mashuti 21, akafunga matano, akakosa mara tano aliyojaribu kwa mbali (three-point) na kumaliza mchezo kwa ‘airball’.

Hata hivyo, katika kupambana kwake, alichora picha ya mchezaji mwenye kitu kikubwa ikiwemo akili ya mchezo, uelewa wa nafasi, usomaji wa mpira na uwezo mkubwa wa kufanya maamuzi sahihi ndani ya dakika chache.

“Alipambana,” alisema Mark Cuban, mmiliki wa zamani wa Mavericks ambaye bado ni shabiki mkubwa wa klabu hiyo. “Hakuingia kwa jazba eti kwa sababu ni chaguo la kwanza kwenye draft. Alicheza mpira. Huo ndiyo ukomavu wa kweli.”

Ni kweli mashuti yake hayakuingia kama wengi walivyotarajia, lakini rekodi nyingine zake zilionyesha uelekeo mzuri. Alikusanya pointi 10, rebounds 6, asisti 4, aliiba mipira mara tatu na kuzuia moja muhimu ambayo ilisaidia kupindua matokeo dakika za mwisho. Katika muda huo huo, alitoa asisti iliyosaidia kufunga pointi za ushindi kwa Dallas.

Kocha wa muda wa Mavericks kwenye Summer League, Josh Broghamer, alisema: “Walikuwa wanamfanyia ‘pressing full court’. Lakini kila mara alichukua maamuzi sahihi. Hii ni ishara ya mchezaji aliye tayari kuishi maisha ya NBA.”

Ni lazima ieleweke, Summer League si kipimo cha mwisho kwa wachezaji chipukizi. Nyota kama Victor Wembanyama alipocheza mechi yake ya kwanza miaka miwili iliyopita, alipiga mbili kwa 13. Leo hii ni mchezaji mwenye jina kubwa. Hii inamaanisha hata Flagg hatapimwa kwa mchezo huu mmoja, bali kwa mfululizo wa maendeleo yake.

Katika mchezo huo, alionekana mara kadhaa akicheza kama point guard nafasi isiyotegemewa kwa mchezaji wa urefu wa futi 6 na inchi 9. Kocha Jason Kidd alisema atampanga kwenye nafasi hiyo kwa msimu ujao hasa wakati Kyrie Irving atakapokuwa anarejea baada ya majeraha ya paja (Achilles). Uamuzi huo unaonyesha imani kubwa aliyonayo kwa kijana huyo.

Kuna wakati Flagg alipambana na mchezaji pekee mwenye umaarufu zaidi ukumbini Bronny James, mtoto wa LeBron James. Katika tukio hilo, Bronny alimnyang’anya mpira Flagg na kusababisha minong’ono ukumbini lakini mwamuzi alipuliza filimbi na kuashiria faulo, jambo lililozua tafrani.

“Watu wasikurupuke. Hii ilikuwa mechi moja tu. Ana miaka 18 tu,” alisema Cuban kwa msisitizo. “Binti yangu alihitimu shule ya sekondari mwezi uliopita na yeye bado ni mdogo kuliko yeye.”

Flagg ambaye alikuwa tegemeo la timu ya chuo kikuu cha Duke, aliwahi kuwika pia kwenye kambi ya mafunzo ya timu ya taifa ya Marekani mwaka jana na hakuwahi kuonyesha kiwango duni kama hiki. Hii ni mara chache sana kwa yeye kuwa na siku ya kawaida lakini alichokionyesha kingine ndicho kilichobeba vichwa vya habari.

Katika kipindi hiki ambacho Mavericks wamepita kwenye kipindi kigumu wakimpoteza Luka Doncic kwa biashara ya kubadilishana, Anthony Davis akijeruhiwa kwenye mechi yake ya kwanza na Kyrie kufanyiwa upasuaji ujio wa Flagg ni tumaini jipya kwa klabu hiyo.

“Kwa sasa tunahitaji matumaini na huyo ni Cooper,” alisema Cuban. “Tulicheza bahati na kupata chaguo la kwanza. Sasa tuna mtu wa kutupeleka mbele.”

Kinyume na wachezaji wengine waliochaguliwa namba moja, Flagg hajaingia kwenye timu inayojengwa upya. Mavericks wana mastaa kama Anthony Davis, Klay Thompson na Kyrie Irving hivyo presha si ya juu kwake. Atajifunza polepole, bila kubanwa kutimiza matarajio ya kuwa ‘mkombozi’.

“Hiki ni kipindi chake cha kujifunza,” alisema Broghamer. “Hatutarajii awe na takwimu za ajabu kila mechi. Tunachotaka ni maendeleo ya kila siku.”

Flagg alimaliza kwa kusema: “Nilitaka kuwa na ‘aggression’ kwenye mechi. Huu unaweza kuwa mchezo mbaya zaidi maishani mwangu, lakini ninafuraha tumeshinda. Hicho ndicho muhimu zaidi kwa sasa.”