Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Claressa Shields atamba hana mpinzani

SHIELD Pict

Muktasari:

  • Kauli hiyo aliitoa jana ikiwa ni siku chache tu tangu amchape bondia raia wa Australia, Kaye Scott kwa TKO raundi ya sita mbele ya mashabiki zaidi ya 16,000 waliojitokeza katika uwanja wa State Farm Arena, Atlanta.

BONDIA wa Marekani Claressa Shields amesema hakuna bondia anayeweza kushindana naye kwa sasa kutokana na ubora alionao na kiwango anachoendelea kukionyesha kwenye mchezo huo duniani.

Kauli hiyo aliitoa jana ikiwa ni siku chache tu tangu amchape bondia raia wa Australia, Kaye Scott kwa TKO raundi ya sita mbele ya mashabiki zaidi ya 16,000 waliojitokeza katika uwanja wa State Farm Arena, Atlanta.

Ushindi huo ulimfanya Shields kutwaa tena taji la dunia la uzito wa kati WBA na WBC middleweight, lakini pamoja na ushindi huo mkubwa, mjadala mpya umeibuka kuhusu bondia huyo mwenye miaka 31; ana kila kitu isipokuwa mpinzani wa kiwango chake.

SHI 03

Shields ambaye hajawahi kupoteza katika mapambano yake 19 ya kulipwa, tayari ameshinda mataji ya dunia katika madaraja matano tofauti ya uzito sambamba na medali mbili za dhahabu za Olimpiki.

“Ninahisi ni baraka na laana. Huwezi kumuona msichana mwingine akiingia ulingoni na kuwa 50-50 na mimi. Hilo halitatokea. Mungu alinichagua kuwa namba moja na mimi nafanya mazoezi kuwa namba moja,” amesema Shields.

SHI 01

HAKUNA WA KUMTINGISHA

Licha ya ubora wake, changamoto kubwa inayomkabili Shields sasa ni kumpata bondia mwenye uwezo wa kumpa changamoto na ushindani mkubwa.

Lakini mabondia kama Katie Taylor na Amanda Serrano wanaonekana wanaweza kubato na Shields na kumpa chalenji kwenye ngumi.

Mhamasishaji wa Shields, Dmitry Salita anakataa hoja ya watu kwamba Shields hajawahi kukutana na mabondia wenye upinzani mkubwa.

“Alipokuwa na rekodi ya mapambano tisa bila kupoteza alitwaa ubingwa wa dunia dhidi ya Christina Hammer aliyekuwa na rekodi ya ushindi wa mabapambano 24-0. Baadaye akaenda England na kumshinda Savannah Marshall aliyekuwa 12-0. Claressa amepanda na kushuka madaraja ya uzito na amekuwa akiwashinda wote,” amesema Salita.

SHI 02

WANAWAKE WAONGEZA NGUVU

Shields anaamini mafanikio yake yanaenda sambamba na ukuaji wa michezo ya wanawake duniani.

Anatoa mfano wa WNBA ambako ushindani kati ya nyota Caitlin Clark na Angel Reese umeongeza hamasa na kuvuta mashabiki wengi.

“Michezo ya wanawake imekuwa ikibadilika. Sote tunajaza viwanja, tuna chapa kubwa na mashabiki wanaotutaka. Ngumi za wanawake ni burudani kama zilivyo michezo mingine,” amesema Shields.

Shields pia amekuwa akitumia mitandao ya kijamii kujenga jina lake, huku maisha yake binafsi, mitindo na kauli zake zikivuta mjadala mkubwa kwa mashabiki.

“Kwa sasa niko kwenye kipindi changu cha Mike Tyson. Kila mtu anakuja uwanjani kuona Claressa Shields atafanya nini,” amesema.