Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Urembo wao usikudanganye, hawa ni mabondia hatari Tanzania

Muktasari:

  • Baadhi yao wana rekodi za tofauti, historia lakini nyuma yake wamekuwa na ushawishi mkubwa kwa wasichana wengine wanaotamani kuwa mabondia. Mwanaspoti linakuletea mabondia warembo Tanzania na wanachofanya ulingoni.

UKIACHANA na mabondia wa kiume wanaofanya vizuri kwenye mchezo huo, miaka ya hivi karibuni mabondia wanawake wamekuwa na ubora mkubwa na kuchangia kwa kiasi chake kwenye maendeleo ya mchezo huo Tanzania.

Baadhi yao wana rekodi za tofauti, historia lakini nyuma yake wamekuwa na ushawishi mkubwa kwa wasichana wengine wanaotamani kuwa mabondia. Mwanaspoti linakuletea mabondia warembo Tanzania na wanachofanya ulingoni.


SARA ALEX

Achana na anachokifanya ndani ya ulingo, Sara amekuwa kivutio kikubwa kwenye ndondi za wanawake nchini kutokana na anavyojiweka.

Bondia huyo anayekuja kwa kasi kwa mujibu wa Boxrec Sara amecheza jumla ya mapambano 10 ambayo yapo kwenye rekodi.

Kati ya hayo ameshinda saba, vipigo viwili na sare moja katika uzito wa super bantamweight. BoxRec inamtaja akiwa miongoni mwa mabondia wa juu wa Tanzania.

Mojawapo wa pambano lililompa umaarufu zaidi ni mwaka huu alipokutana na Halima Vunjabei katika pambano la kuwania taji la UBO female world featherweight. Vunjabei alishinda pambano hilo kwa uamuzi wa majaji baada ya raundi 10.

“Napenda ninachokifanya kwa sababu mwanzoni ngumi zilikuwa zinaonekana kufanywa na mabondia wa kiume tu, lakini sasa wanawake nao wanafanya vizuri sana,” anasema Sara


REHEMA MAFUNDO

Huyu ni bondia mwingine ambaye ukimfuatilia nje ya kazi yake ya ngumi unaweza kudhani mtu wa kawaida tu lakini akiwa ulingoni anafanya balaa. Mojawapo wa rekodi zinazovutia kwa bondia huyo, kwenye mapambano 14 akishinda 13 na sare moja akiwa hajapoteza pambano lolote.

Mafundo mwenye uzito wa welterweight nje na urembo wake anapiga kazi kwelikweli na kutajwa kama mmoja wa mabondia wanawake wenye ushawishi mkubwa ulingoni.

Mafundo anasema pambano lake dhidi ya Happy Daudi 2017 aliloshinda kwa TKO katika ubingwa wa PST wa uzito wa lightweight, limeacha alama kubwa kwenye taaluma yake.

“Ni pambano ambalo sitalisahahu kwa sababu tulikutana mabondia wote wazuri na nilifanya mazoezi sana ndani ya wiki za mwisho kabla ya kupanda ulingoni,” anasema.


HALIMA VUNJABEI

Mwanadada huyo ana uzoefu mkubwa ulingoni akiwa amecheza mapambano zaidi ya 30, kati ya hayo ameshinda 17, vipigo 16 na sare moja akiwa na KO 10 katika mapambano 34.

Vunjabei amecheza mapambano ya kimataifa katika nchi mbalimbali na pia amewahi kushinda mikanda ya kimataifa. Mwaka 2026 alikutana na Sara Alex katika pambano la kuwania taji la UBO la dunia la featherweight, akashinda kwa uamuzi wa majaji baada ya raundi 10.

DORISIA MAZIGE

Huyu ni bondia aliyekuja kitofauti kabisa. Amekuwa akitumia hijabu kama utambulisho wake anapopanda kupima uzani au hata kwenye mechi.

Ni bondia mrembo hasa aliyeanza kupigana 2024 ana rekodi ya mapambano matano akishinda manne na kupoteza moja dhidi ya Sara Alex.

Mazige mwenye  uzito wa super featherweight katika rekodi ya kupoteza pambano moja kati ya matano inamfanya kuwa mmoja wa mabondia wanaotajwa kuanza vizuri katika ndondi.

“Sidhani kama kazi ndio inafanya mwanamke ajibadilishe muonekano wako, kwangu mimi ninafurahi kuona kama mwanamke ninayepambana ndani na nje ya ulingo.”


HAWA NEWTON

Mrembo huyo alianza kupigana 2022, lakini hakuwa na mwendelezo mzuri wa kupanda ulingoni.

Bondia huyo anayepigana uzito wa lightweight ana mapambano sita akishinda manne, sare moja na kupoteza pambano moja.

Ndani ya miaka minne bondia huyo amecheza mapambano sita tu ikiwa ni idadi ndogo kwa bondia ambaye alianza vizuri miaka minne iliyopita.


HIDAYA ZAHORO

Sio rahisi kumjua Hidaya akiwa mtaani kama bondia kutokana na aina yake ya maisha. Kulingana na Boxrec bondia huyo ameshinda pambano moja na kupoteza moja. Bado anajitafuta kwenye ndondi za kulipwa akiwa na miaka 32 Hidaya amekuwa kivutio kikubwa kwenye ndondi kutokana na aina yake ya maisha.


STUMAI MUKI

Bondia huyo mwenye miaka 25 alianza kazi ta ngumi mwaka 2019.Paulo ana uzoefu mkubwa katika ndondi za kulipwa akiwa ameshinda mapambano 12 na vipigo sita, bila sare, katika uzito wa bantamweight. Uzoefu wake wa mapambano 18 unamfanya kuwa miongoni mwa mabondia waliokwisha pitia mapambano mengi katika kundi hili.

“Familia yangu inanisapoti hasa mama japo mwanzoni alikuwa anaogopa sana, sidhani kama mchezo wa ngumi unaweza kumbadilisha mwanamke hiyo ni dhana tu na michezo ni sehemu yetu wanawake.”


DEBORA MWENDA

Kuna muda baadhi ya mashabiki hujisahau kama Mwenda ni bondia kutokana na namna anavyojiweka kama mwanamke mwenye mvuto na urembo.

“Napenda sana kupendeza na kuonekana mtu wa tofauti mimi ni mwanamke na kuna maisha nje ya ngumi kwahiyo kuwa mrembo na haiathiri chochote kwenye kazi yangu,” anasema.

Ukiachana na hao mabondia wengine warembo ni Egine Kayange , Grace Mwakamele , Nargis Selemani Mbange , Flora Machela , Zawadi Kutaka na Najma Isike na wengineo.