Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Chelsea yapigwa nyumbani

CHELSEA Pict

Muktasari:

  • Alejandro Garnacho aliitanguliza The Blues kwa bao safi alipoupitisha mpira kwenye tobo la kipa wa Sunderland, lakini wapinzani wao hao walitokea nyuma na kushinda kibabe.

LONDON, ENGLAND: SUNDERLAND imeiduwaza Chelsea uwanjani kwao Stamford Bridge baada ya kuichapa mabao 2-1 katika mchezo wa Ligi Kuu England uliofanyika Jumamosi.

Alejandro Garnacho aliitanguliza The Blues kwa bao safi alipoupitisha mpira kwenye tobo la kipa wa Sunderland, lakini wapinzani wao hao walitokea nyuma na kushinda kibabe.

Sunderland ilisawazisha kupitia kwa Wilson Isidor kabla ya Talbi kufunga bao la ushindi kwenye dakika za mwisho kabisa kuifanya timu hiyo kupanda hadi nafasi ya pili kwenye msimamo wa ligi hiyo kabla ya timu nyingine kama Manchester City hazijacheza.

Hicho ni kipigo cha tatu kwa Chelsea katika mechi tisa ilizocheza msimu huu kwenye Ligi Kuu England na hivyo kuzidi kumweka kocha Enzo Maresca katika wakati mgumu.

Katika mchezo mwingine wa ligi hiyo, Newcastle United imefanikiwa kuichapa Fulham mabao 2-1 katika mechi ya kibabe kabisa iliyofanyika St James' Park. 

Bao la dakika 90 la Bruno Guimaraes liliisaidia Newcastle United kupata pointi tatu muhimu baada ya lile bao lao la kwanza lililofungwa na Jacob Murphy kwenye kipindi cha kwanza kusawazishwa na Sasa Lukic wa Fulham mapema kwenye kipindi cha pili.

Matokeo hayo yameifanya Newcastle kufikisha pointi 12 katika mechi tisa, huku Fulham ikibaki na pointi nane ilizovuna katika idadi kama hiyo ya mechi.