Chelsea yaandaa mzigo mrefu kumpata Lukaku
MABOSI wa Chelsea wanandaa zaidi ya Euro 100 milioni ili kufanikisha dili la kumsajili straika wa Inter Milan na timu ya taifa ya Ubelgiji, Romelu Lukaku, 27, katika dirisha lijalo la majira ya kiangazi.
Chelsea inataka kufanya hivyo baada ya kuona uwezekano wa kuipata huduma ya staa wa Borussia Dortmund na timu ya taifa ya Norway, Erling Braut Haaland, 20, unazidi kuwa mgumu.
Lukaku amekuwa kwenye rada za timu nyingi kubwa barani Ulaya kuelekea dirisha lijalo la majira ya kiangazi kutokana na kiwango alichoonyesha kwa msimu huu ambapo amecheza mechi 36 za michuano yote na kufunga mabao 27.
Mbali ya Chelsea saini ya Lukaku pia inawindwa na Manchester City na Barcelona ambazo zote zinaonekana kuwa na upungufu makubwa kwenye safu zao za ushambuliaji vikosini.