Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Chelsea sasa inamtaka Alejandro Garnacho

TETESI Pict

Muktasari:

  • Garnacho ni miongoni mwa wachezaji waliopewa taarifa za kutafuta timu mpya watakazochezea msimu ujao kwani hawapo katika mipango ya kocha wa Man United, Ruben Amorim.

BAADA ya mazungumzo ya awali yaliyofanyika Januari mwaka huu baina ya wawakilishi wa Chelsea a wasimamizi wa winga wa Manchester United na timu ya taifa ya Argentina, Alejandro Garnacho, mwenye umri wa miaka 21, sasa taarifa zinaeleza matajiri hao wa London wapo tayari kumsajili staa huyo na watawasilisha ofa ndani ya wiki chache zijazo.

Garnacho ni miongoni mwa wachezaji waliopewa taarifa za kutafuta timu mpya watakazochezea msimu ujao kwani hawapo katika mipango ya kocha wa Man United, Ruben Amorim.

Staa huyu nia yake ni kuendelea kucheza Ligi Kuu England na ikishindikana ndio ataangalia sehemu nyingine nje ya ligi hiyo ambako timu kibao pia zinamhitaji.

Moja kati ya timu za nje ya England zinammezea sana mate ni Napoli ambayo raia wao Aurielo de Laurentiis ameweka wazi nia yao ya kutaka kumsajili akiamini ni mchezaji mzuri na ataonyesha makubwa akiwa katika kikosi chao.

Awali kulikuwa na ofa za nje ya bara la Ulaya ambapo Al-Nassr ilidaiwa kuwasilisha ofa lakini fundi huyu amekataa na kusisitiza kuwa anahitaji kucheza soka la kiushindani.

Kocha wa Chelsea Enzo Maresca ndio anatamani sana huduma ya mchezaji huyu raia mwenzake wa Argentina na anamhusudu sana kutokana na uchezaji wake ambao anaona utaendana kabisa na mifumo yake.

Amorim hataki kusafiri na fundi huyu kwenda Marekani kwa ajili ya maandalizi ya msimu hivyo kuna uwezekano wa dili lake la kujiunga na moja kati ya timu tajwa likakamilika wiki chache zijazo. Man United inahitaji takriban Pauni 50 milioni kumuuza.


Pierre-Emerick Aubameyang

MSHAMBULIAJI wa kimataifa wa Gabon anayeichezea Al-Qadsiah ya Saudi Arabia, Pierre-Emerick Aubameyang, mwenye umri wa miaka 36, anatarajiwa kuwasili Ufaransa mwisho wa wiki hii kwa ajili ya kumalizana na Marseille ambayo inataka kumsajili. Licha ya umri kumtupa mkono, Kocha wa Marseille, Roberto de Zerbi anaamini staa huyu atamsaidia kuboresha eneo lake la ushambuliaji pamoja na kuongeza uzoefu katika timu.


Jhon Arias

WOLVES iko karibu kufikia makubaliano ya kutoa Pauni 15 milioni kwenda Fluminense kwa ajili ya kumsajili winga wa timu hiyo na Colombia, Jhon Arias, mwenye miaka 27. Benchi la ufundi la Wolves limevutiwa sana na kiwango ambacho winga huyu amekionyesha katika michuano ya Kombe la Dunia la klabu iliyofanyika Marekani. Arias mweyewe hataki kubaki katika timu hiyo na anatarajia dili la kwenda Ulaya litakamilika.


James McAtee

MANCHESTER City ipo tayari kumuuza kiungo wao na timu ya taifa ya vijana ya England chini ya miaka 21, James McAtee, mwenye umri wa miaka 22, katika dirisha hili ili kuendana na matakwa ya kanuni za kifedha. Ripoti zinadaiwa kwa sasa McAtee yuko Ujerumani ambako ameenda kutembelea makao makuu ya  Eintracht Frankfurt inayohitaji kumsajili.


Granit Xhaka

KIUNGO wa Bayer Leverkusen, Granit Xhaka amekubali kujiunga na Neom SC ya Saudi Arabia dirisha hili. Timu hii imeripotiwa kuwasilisha ofa ya kumsajili katika wiki kadhaa zilizopita na baada ya staa huyu kukubali sasa matajiri hao wanazungumza na wawakilishi wa Leverkusen kuhusiana na masuala ya ada ya uhamisho. Xhaka, 32, amekubali ofa hiyo kwa sababu haitaji tena kuendelea kucheza soka la kiushindani.


Leandro Trossard

KOCHA wa Fenerbahce, Jose Mourinho amesisitiza kwa mabosi wa timu hiyo anahitaji sana huduma ya  mshambuliaji wa Arsenal na timu ya taifa ya Ubelgiji, Leandro Trossard, dirisha hili kwa ajili ya kumtumia msimu ujao. Inadaiwa Arsenal ipo tayari kumuuza mchezaji huyo mwenye miaka 30 ili kupata pesa itakazoongezea katika usajili wa dirisha hili. Hata hivyo, hivi karibuni Bayern pia imeonyesha nia ya kumsajili.


Ederson

MANCHESTER United inataka kuwasilisha ofa kwenda Atalanta kwa ajili ya kumsajili kiungo wa timu hiyo na Brazil, Ederson, ambaye huduma yake pia inahitajika na Inter Milan na Juventus. Staa huyu mwenye umri wa miaka 26 anauzwa kwa kiasi kisichopungua pauni 44 milioni. Man United inaonekana kuwa katika nafasi nzuri ya kukamilisha dili hili.


Neil El Aynaoui

SUNDERLAND, Leeds United na Wolves bado zinapambana kumsajili kiungo wa kati wa Lens na timu ya taifa ya Morocco chini ya miaka 23, Neil El Aynaoui, lakini wanakabiliwa na ushindani kutoka AS Roma, Juventus na AC Milan ambazo pia zinahitaji saini ya mchezaji huyo, 24. Hata hivyo, ripoti zinadai Neil mwenyewe anatamani sana kucheza Ligi Kuu England kwa sababu ni ndoto yake.