Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Chama la Yamal... Utake, usitake utapigwa tu!

UTAPIGWA Pict

Muktasari:

  • Linapokuja suala la kuchagua kikosi bora kwenye historia ya soka jambo hilo ni gumu sana, hata inapotakiwa kikosi chenyewe uchague kutoka kwa mastaa wa Barcelona.

BARCELONA, HISPANIA: KINDA matata kabisa wa Barcelona, Lamine Yamal ametaja kikosi chake cha muda wote cha miamba hiyo ya Nou Camp na kama ilivyotarajiwa, ni kikali balaa.

Linapokuja suala la kuchagua kikosi bora kwenye historia ya soka jambo hilo ni gumu sana, hata inapotakiwa kikosi chenyewe uchague kutoka kwa mastaa wa Barcelona.

Tuzo 12 za Ballon ‘Or zimenyakuliwa na wachezaji wa Barca, ukiweka kando mataji kitu kinachofanya uchaguzi wa kikosi bora kuwa mgumu.

Miongoni mwa mastaa wa Barcelona ni Yamal, 18, ambaye amechagua kikosi chake cha kwanza na kukiweka hadharani. Ni moto wa kuotea mbali.

Kipa: Victor Valdes; Golini atakuwapo kipa fundi wa kuanzisha mashambulizi nyuma, akiwa ni mwanzo wa makipa wa kisasa kama ilivyo kwa Ederson na Alisson, ambao wamekuwa hodari kwa kutumia vyema miguu yao. Valdes alicheza mechi 536 Barca.

Beki wa kati: Carles Puyol; Kama unataka beki wa kazi basi nafasi hiyo inamhusu Carles Puyol. Staa huyo alicheza karibu mechi 600 kwenye kikosi hicho huku akiwa nguzo imara katika mtindo wa soka la mvuto la miamba hiyo ya Camp Nou.

Beki wa kati: Gerard Pique; Pique alianzia kwenye akademia ya La Masia kabla ya kunaswa na Manchester United na kisha kurudu tena Barca, ambako alikwenda kuwa mtu muhimu kwenye kikosi cha kwanza cha miamba hiyo ya Camp Nou.

Beki wa kati: Javier Mascherano; Wakati Mascherano alipojiunga na Barca kutoka Liverpool, alinaswa kama kiungo mkabaji, lakini baadaye kocha Pep Guardiola alimrudisha kucheza beki ya kati, eneo ambalo Muargentina huyo amelitendea haki.

Kiungo mkabaji: Sergio Busquets; Sergio Busquets hakuzungumzwa sana kama ilivyo kwa viungo wengine wa Barca, lakini Mhispaniola huyo alikuwa injini ya mipango mingi ya timu hiyo kuifanya kufiti uwanjani. Alicheza mechi 722.

Kiungo wa kati: Xavi; Fundi wa kupiga pasi uwanjani. Umahiri mkubwa wa Xavi ulikuwa kutuliza kasi ya mchezo na kuamua uende vile yeye anataka. Kila mpira ulipokuwa kwenye miguu yake, basi alipepesa macho pande zote, kabla ya kutua pasi.

Kiungo wa kati: Andres Iniesta; Moja ya viungo mahiri kabisa waliopata kutokea kwenye soka, Andres Iniesta alivutia kumtazama mpira ulipokuwa kwenye miguu yake.

Kiungo mshambuliaji: Ronaldinho; Staa huyo wa Kibrazili amepata nafasi kwenye kikosi cha Yamal, licha ya kwamba winga mkali huyo aliondoka wakati kinda huyo wa Kihispaniola akiwa na umri wa mwaka mmoja. Ronaldinho alikuwa kivutio kingine kwenye kikosi cha Barcelona wakati anakipiga katika timu hiyo.

Winga wa kulia: Lionel Messi; Mchezaji mahiri kabisa, si tu Barcelona bali kwenye historia ya mchezo wa soka, hivyo haishangazi kuona Messi anapata namba kwenye kikosi hiki cha Yamal kinachohusu mastaa waliowahi kukipiga Barcelona.

Winga wa kushoto: Neymar; Yamal alimwelezea Neymar kuwa ni kipenzi chake na hilo linaonekana wazi kutokana na staili yake ya uchezaji kufanana kabisa na Mbrazili huyo. Neymar aliunda safu matata sana ya ushambuliaji sambamba na Messi na Luis Suarea, aliyefahamika kwa jina la MSN, wakati wanakipiga pamoja Camp Nou.

Straika: Luis Suarez; Kuna baadhi ya watu walishtuka wakati Barcelona ilipolipa Pauni 64.98 milioni kunasa saini ya Luis Suarez, tena kwa wakati huo akiwa amefungiwa kucheza soka kutokana na kosa la kumng’ata mchezaji mwenzake uwanjani.

Lakini, alichokwenda kukifanya Suarez huko Camp Nou, ndicho kitu kilichomfanya Yamal aone atastahili kuipata nafasi kwenye kikosi chake cha muda wote na kuwapiga chini washambuliaji wa kati kibao waliowahi kucheza kwenye timu hiyo.