Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Carroll anusurika jela, kisa fedha zake

CARROL Pict

Muktasari:

  • Carroll, 37, alifikishwa katika Mahakama ya Kaunti ya Chelmsford kutokana na mgogoro wa kifedha unaomhusisha aliyekuwa mke wake, Billi Mucklow, nyota wa zamani wa kipindi cha uhalisia cha televisheni cha The Only Way Is Essex.

LONDON, ENGLAND: MSHAMBULIAJI wa zamani wa England, Andy Carroll ameepuka kifungo cha jela baada ya kukiuka mara tano amri ya mahakama iliyomzuia kutumia fedha zake kwa matumizi yasiyo ya lazima.

Carroll, 37, alifikishwa katika Mahakama ya Kaunti ya Chelmsford kutokana na mgogoro wa kifedha unaomhusisha aliyekuwa mke wake, Billi Mucklow, nyota wa zamani wa kipindi cha uhalisia cha televisheni cha The Only Way Is Essex.

Mahakama ilielezwa kuwa Carroll alitumia Pauni 69,181 (Sh253 bilioni ) ambazo alipaswa kuzihifadhi hadi kusikilizwa kwa shauri la kifedha litakalofanyika kwa siku tano mwezi ujao.

Wakili wake, Lauren Lanson,aliiambia mahakama kuwa kiasi hicho ni kidogo ikilinganishwa na thamani ya mali na fedha zinazohusika katika mzozo huo, pamoja na gharama kubwa za kisheria.

Kwa mujibu wa orodha ya matajiri ya Sunday Times ya mwaka 2019, utajiri wa Carroll ulikadiriwa kufikia Pauni19 milioni.

CARR 01

Katika kesi hiyo, Carroll alikiri kukiuka mara tano amri ya mahakama. Miongoni mwa matumizi yaliyotajwa ni Pauni 5,556 alizotumia kuboresha gari lake, Pauni 10,000 alizompa kaka wa mpenzi wake na fedha alizotumia kugharamia ujenzi wa wazazi wake.

Hata hivyo, wakili wa Mucklow, Jenna Lucas, alidai kuwa hakuna matumizi hayo yaliyokuwa ya lazima.

“Hakuna matumizi yoyote yaliyokuwa ya lazima. Kwa mtazamo wangu, amepuuza kabisa amri ya mahakama,” amesema Lucas.

Kwa upande wake, wakili wa Carroll amesema mchezaji huyo si mtu mwenye mpangilio mzuri katika kusimamia fedha zake, akidai kuwa kazi hiyo hufanywa na watu wengine huku yeye akijikita katika soka.

CARR 02

“Si mtu mwenye mpangilio mzuri zaidi katika kusimamia fedha zake. Kuna watu wengine wanaofanya kazi hiyo kwa niaba yake. Yeye hujikita katika kazi yake kama mchezaji wa soka,” amesema Lanson.

Carroll aliwasili mahakamani akiwa ameambatana na mpenzi wake, Lou Teasdale.

Licha ya ukiukwaji huo, hakimu wa wilaya Teresa Foss aliamua kutompeleka jela, akisema adhabu hiyo ingekuwa kali kupita kiasi.

Badala yake, Carroll alitozwa faini ya Pauni 20,000.


CARR 03

CARROLL BADO KESI MLANGONI

Matatizo ya kisheria ya Carroll hayajaishia hapo, kwani anakabiliwa pia na kesi nyingine ya tuhuma za kukiuka amri iliyowekwa kumzuia kumsumbua au kumkaribia mtu fulani.

Carroll aliwahi kuzichezea Newcastle United, Liverpool na West Ham United kabla ya kujiunga na Dagenham & Redbridge ya Ligi ya Taifa Kusini mwaka 2025.

Kabla ya hapo, alicheza soka nchini Ufaransa akiwa na Amiens na Bordeaux.