Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Usajili dirisha dogo ni njaanuari

Usajili Pict

Muktasari:

  • Moja kati ya sababu zinazochangia timu hizo kutofanya usajili katika dirisha hili huwa ni idadi ndogo ya wachezaji wazuri wanaopatikana sokoni na mara nyingi inahitaji kuvunja benki kuhakikisha unasajili mchezaji mwenye kiwango cha juu.

LIVERPOOL, ENGLAND: DIRISHA la usajili la Januari linazidi kuyoyoma barani Ulaya na timu nyingi zimeonekana kusua sua katika kufanya usajili wa kuboresha vikosi vyao.

Moja kati ya sababu zinazochangia timu hizo kutofanya usajili katika dirisha hili huwa ni idadi ndogo ya wachezaji wazuri wanaopatikana sokoni na mara nyingi inahitaji kuvunja benki kuhakikisha unasajili mchezaji mwenye kiwango cha juu.

Vilevile, wachezaji wengi wanaosajiliwa katika dirisha hili huwa wanapitia kipindi kigumu kwa kutoonyesha kiwango kilichotarajiwa. Hawa hapa wachezaji watano waliowahi kusajiliwa na timu za EPL ambao usajili wao ulikuwa na matumaini makubwa lakini walifeli vibaya.


US 01

5. Alexandre Pato Mkopo

Chelsea ilimsajili fundi huyu kwa mkopo wa miezi sita, akitokea Corinthians ya Brazil, lengo likiwa ni kuhakikisha inaboresha eneo lao la ushambuliaji kwa ajili ya kupambana vizuri katika vita ya kuliwania taji la EPL.

Staa huyu ambaye alisajiliwa Januari mwaka 2016 akiwa na umri wa miaka 26, alifunga katika mechi yake ya kwanza dhidi ya Aston Villa kupitia penalti wakati Chelsea ikishinda mabao 4-0 na baada ya mechi hiyo alicheza nyingine moja na tangu hapo hakucheza tena na msimu ulipomalizika alirudi Corinthians licha ya mkataba wake kuwa na kipengele ambacho kingewawezesha kumnunua mazima ikiwa wangehitaji.


US 02

4. Juan Cuadrado Pauni 23.3 milioni

Chelsea ilimsajili Cuadrado kwa ada kubwa baada ya kuvutiwa na kiwango alichoonyesha kwenye Kombe la Dunia akiwa na Colombia majira ya kiangazi mwaka 2014.

Hata hivyo, alikaa miezi saba tu kabla ya kutolewa kwa mkopo kwenda Juventus mwaka  huo huo.

Chelsea ilifikia hatua ya kumruhusu aondoke kwenda Fiorentina kwa ajili ya kumpisha Cuadrado lakini bado hakukuwa na matokeo chanya.

Cuadrado alicheza mechi 13 kwenye kikosi chao  bila ya kufunga wala kutoa pasi ya goli.


US 03

3. Andy Carroll Pauni 35 milioni

Alisajiliwa sawa na Luis Suarez lakini Liverpool ililipa kiasi kikubwa zaidi cha pesa kuhakikisha inaipata saini yake.

Alipotua, matumaini yalikuwa makubwa sana kwake na akakabidhiwa hadi jezi namba tisa iliyokuwa inavaliwa na Fernando Torres, lakini alishindwa kujiunga na orodha ya washambuliaji wakubwa wa Liverpool akifunga mabao manane tu katika mechi 58 alizocheza.


US 04

2. Wilfried Bony Pauni 25 milioni

Bony alikuwa nyota wa Swansea na katika msimu wake wa kwanza, alifunga mabao 25 kwenye mashindano yote.

Aliendelea na kiwango hicho katika msimu wake wa pili wa 2014/15  akifunga mabao tisa hadi kufikia Januari 2015 hali iliyoishawishi Man City kuvutiwa naye na kumsajili.

Hata hivyo, mshambuliaji huyo raia wa  Ivory Coast hakufanya kilichotarajiwa na kuwa hapati nafasi kubwa ya kucheza.

Hali ilikuwa mbaya zaidi baada ya Guardiola kuingia kuhamia Man City na baada ya kudumu kwa miezi 18, alitolewa kwa mkopo kwenda Stoke City kabla ya kuuzwa mazima kurudi Swansea kwa Euro 13 milioni.


US 05

1. Alexis Sanchez Euro 34 milioni

Baada ya kufanya vizuri sana akiwa na Arsenal, Manchester United walivutiwa naye sana na kuamini kwamba anaweza kusaidia sana timu yao hususani eneo la ushambuliaji.

Man United ililipa Euro 34 milioni pia ikamtoa kiungo wao Henrikh Mkhitaryan kama sehemu ya ofa ili kumpata Sanchez.

Kwa bahati mbaya haikuwa hivyo, kwani mchezaji huyo wa kimataifa wa Chile alishindwa kuonyesha kilichotarajiwa akifunga mabao matatu tu kwenye Ligi Kuu England katika kipindi cha miezi 18, alitolewa kwa mkopo kwenda Inter Milan mwaka 2019 mwisho wa msimu wake wa pili na baadaye akajiunga nao mazima kwa usajili huru.