Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Buffon aibua ishu ya Chiesa kuitwa timu ya taifa

BUFFON Pict

Muktasari:

  • Chiesa hajawahi kuitwa katika kikosi cha Azzuri tangu 2024 na hiyo imetokea baada ya kusajiliwa na Liverpool ya England, ambayo bado haijampa nafasi ya kutosha ya kucheza mara kwa mara kama ilivyotarajiwa.

Gwiji wa soka wa Italia, Gianluigi Buffon, amesema kikosi cha Azzurri kinamsubiri Federico Chiesa kurejea katika timu hiyo, baada ya kushindwa kupata tiketi ya moja kwa moja ya kushiriki Kombe la Dunia 2026.

Chiesa hajawahi kuitwa katika kikosi cha Azzuri tangu 2024 na hiyo imetokea baada ya kusajiliwa na Liverpool ya England, ambayo bado haijampa nafasi ya kutosha ya kucheza mara kwa mara kama ilivyotarajiwa.

Kocha wa Italia, Gennaro Gattuso, amekuwa akitaka kumjumuisha Chiesa katika kikosi hicho hivi karibuni, lakini winga huyo amekuwa akikataa mwaliko huo wa timu ya taifa.

Buffon, ambaye sasa ni sehemu ya maofisa wa timu ya taifa ya Italia, amesema wazi kikosi kinamsubiri mchezaji huyo muhimu, kwa ajili ya mechi ya mchujo wa Kombe la Dunia dhidi ya Ireland ya Kaskazini.

BUFF 01

“Tunahitaji kuwarudisha wachezaji wote bora. Kama mtu anataonesha uwezo wa ubora wa kupambana, hakuna kizuizi chochote, kwa sababu tunawahitaji kwa ajili ya kuisaidia timu yetu ya taifa,” amesema kipa huyo wa zamani na kuongeza;
“Tunamsubiri Chiesa, kuna wachache kama yeye Ulaya. Lakini Gattuso hajamuacha nyumbani mtu yeyote anayestahili kuwa hapa. Tunaamini kila mtu ana umuhimu wa kuichezea timu hii.”

Gattuso alieleza Oktoba kwamba Chiesa alikataa kurejea katika kikosi cha timu ya taifa kwa sababu alihisi hakuwa fiti vya kutosha kuisaidia Italia kikamilifu.

Baada ya droo ya mechi za mchujo wa Kombe la Dunia, ambapo Italia imepangwa kucheza dhidi ya Ireland ya Kaskazini, Gattuso aliulizwa tena kuhusu Chiesa na kama angeweza kuwa mchezaji muhimu kwa mechi hiyo, kocha huyo alijibu kwa ukali: “Mnauliza maswali yaleyale kila wakati. Nimekuwa nikimwita Chiesa. Nimemwita kabla ya kila mapumziko ya kimataifa. Tatizo si Gattuso au benchi la ufundi. Tatizo ni lake si letu. Mnajua hilo vizuri. Mnauliza swali lilelile, na mimi nawapa jibu lilelile.”

BUFF 02

Licha ya sintofahamu hiyo, Chiesa alikuwa mmoja wa washambuliaji wenye tija zaidi wa Liverpool katika mechi za mwanzo wa msimu, amefunga mabao mawili na pasi tatu za mabao ndani ya dakika 344 pekee katika mashindano yote.

Amechangia moja kwa moja bao kila dakika 40 katika Ligi Kuu ya EPL msimu huu, lakini cha kushangaza bado hajapata nafasi ya kuanza mechi yoyote ya ligi.

Chiesa ana mkataba na Liverpool hadi majira ya kiangazi 2028, lakini iwapo hatapata muda zaidi wa kucheza kuelekea dirisha la usajili la Januari, mustakabali wake unaweza kuwa wa kuvutia kufuatilia hasa kwa kuwa atataka kuwa tayari kuisaidia Italia mwanzoni mwa mwaka mpya.