Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Bruno hauzwi! Man United yaigomea Galatasaray

BRUNO Pict

Muktasari:

  • Galatasaray, Atletico Madrid, Juventus na AC Milan ni miongoni mwa klabu zinazotajwa kumuwania Fernandes mwenye umri wa miaka 31.

MANCHESTER, ENGLAND: MANCHESTER United imesisitiza kuwa nahodha wake, Bruno Fernandes, hayuko sokoni kwa bei yoyote katika dirisha hili la usajili wa majira ya kiangazi, licha ya Galatasaray kujiandaa kuwasilisha ofa nono kwa ajili ya kumsajili kiungo huyo.

Galatasaray, Atletico Madrid, Juventus na AC Milan ni miongoni mwa klabu zinazotajwa kumuwania Fernandes mwenye umri wa miaka 31.

Taarifa zinaeleza kuwa Galatasaray iko tayari kutoa pauni 42.7 milioni (zaidi ya Sh bilioni 150) pamoja na kumpa Fernandes mshahara mkubwa zaidi kuliko anaoupata sasa Old Trafford.

Kifungu cha kuvunja mkataba cha pauni 57 milioni kwa klabu za nje kilimalizika mwezi uliopita, jambo linalomaanisha United ina nafasi kubwa ya kudhibiti mustakabali wa nahodha huyo.

United inaamini itahitaji fedha nyingi zaidi kumtafuta mbadala wa Fernandes, hasa katika soko la sasa ambalo bei za wachezaji zimepanda kwa kiwango kikubwa.

BRUN 01

Hadi sasa hakuna ofa rasmi iliyowasilishwa kwa United, huku vigogo wa klabu hiyo wakiamini kwamba klabu zinazomuwania Fernandes zitakuwa zinapoteza muda kujaribu kumnasa.

Machi mwaka huu, iliripotiwa kuwa United ilikuwa imepanga kuanza mazungumzo ya mkataba mpya na Fernandes. Hata hivyo, mazungumzo hayo bado yako katika hatua za awali.

Hali hiyo ya kutokuwa na mkataba mpya ndiyo inayotajwa kuwa sehemu ambayo Galatasaray na klabu nyingine zinazomhitaji zinaweza kuitumia kumshawishi.

Fernandes amebakiza mwaka mmoja katika mkataba wake wa sasa, ukiwa na kipengele cha kuongeza mwaka mwingine. Kwa sasa ni miongoni mwa wachezaji wanaolipwa zaidi United, akipokea takribani pauni 220,000 kwa wiki.


ALIUMIA MWAKA JANA

Nahodha huyo aliumizwa na msimamo wa United mwaka jana wakati Al Hilal ilipokuwa tayari kutoa pauni 100 milioni kwa ajili yake.

Wakati huo United ilisema uamuzi wa kuondoka au kubaki ulikuwa mikononi mwa Fernandes. Hata hivyo, staa huyo wa Ureno alihisi klabu ilipaswa kuonyesha nia kubwa zaidi ya kumtaka abaki, ili kuthibitisha umuhimu wake kwa timu.

BRUN 02

Fernandes alijibu kwa vitendo uwanjani msimu uliopita baada ya kuweka rekodi ya Ligi Kuu England kwa kutoa asisti 21.

Kwa sasa anatajwa kuwa mmoja wa vinara wanaowania tuzo ya PFA Player of the Year 2025-26, ambayo mshindi wake anatarajiwa kutangazwa mjini Manchester wiki ijayo.


ANATAKA KUFANIKIWA OLD TRAFFORD

Licha ya uwezekano wa kupata fedha nyingi zaidi Saudi Arabia au kwingineko, Fernandes amesisitiza kuwa dhamira yake ni kubaki Old Trafford na kujaribu kutimiza ndoto yake ya kuiongoza United katika mbio za kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu.

Katika kipindi cha misukosuko chini ya Ruben Amorim na baadaye ufufuo wa timu chini ya Michael Carrick, Fernandes amebaki kuwa karibu na makocha hao na kuendelea kuonyesha mfano mzuri kwa wachezaji wenzake ndani ya uwanja.

Akizungumza mapema msimu huu, Fernandes alisema kuwa suala la kubaki United kwake si la uaminifu pekee, bali ni hamu ya kutimiza jambo ambalo hawezi kulipata katika klabu nyingine.

Alisema: “Ningeweza kuondoka miaka miwili iliyopita, miaka mitatu iliyopita au msimu uliopita, lakini napenda sana kuwa hapa.”

BRUN 03

Fernandes aliongeza kuwa mafanikio akiwa United yana thamani kubwa kwake kuliko mafanikio katika klabu nyingine yoyote.

“Nilishinda Carabao Cup na FA Cup, lakini kile ambacho klabu hii inataka, mashabiki wanataka na mimi pamoja na timu tunataka, bado hatujakipata. Hadi mkataba wangu utakapoisha, nitaendelea kujaribu,” alisema.


GALATASARAY YAANDAA MILIONI 18.3

Kwa mujibu wa taarifa za The Telegraph, rais wa Galatasaray, Dursun Ozbek, amedhamiria kumsajili Fernandes na yuko tayari kumlipa karibu mara mbili ya fedha anazopata sasa United.

Ofa hiyo inadaiwa kuwa na thamani ya pauni milioni 18.3 kwa mwaka. Kutokana na mfumo wa kodi nchini Uturuki, Fernandes angeweza kubaki na fedha za nyumbani ambazo ni karibu mara mbili ya anachopata Old Trafford.

BRUN 04

Ombi la Galatasaray linatarajiwa kuwa na malipo ya awali pamoja na bonasi mbalimbali zinazotegemea mafanikio.

Miongoni mwa bonasi hizo ni pauni milioni 1.3 kwa kila ubingwa, hadi kufikia jumla ya pauni milioni 5.1. Pia anaweza kupata pauni milioni 1.7 endapo atakuwa mtoa asisti bora zaidi wa ligi katika msimu wake wa kwanza, au pauni milioni 1.3 akifanikiwa kufanya hivyo msimu wa pili.

Galatasaray pia inaweza kumlipa pauni 850,000 endapo itafuzu Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu ujao, kiasi kingine cha pauni 850,000 ikifika hatua ya 16 bora, na pauni milioni 3 iwapo itafika robo fainali.