Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Namba za Bruno Guimaraes zinaongea

BRUNO Pict

Muktasari:

  • Mbrazil huyo amekuwa akikabiliana na Arsenal kila msimu tangu 2021/22, hivyo ubora na uwezo wake tayari unafahamika vyema kwa kikosi cha Arteta.

LONDON, ENGLAND: Arsenal imekamilisha usajili wa kiungo Bruno Guimaraes kutoka Newcastle United, huku Mikel Arteta akitarajiwa kupata nguvu mpya kwenye eneo la kiungo kuelekea msimu wa 2026/27 na miaka inayofuata.

Mbrazil huyo amekuwa akikabiliana na Arsenal kila msimu tangu 2021/22, hivyo ubora na uwezo wake tayari unafahamika vyema kwa kikosi cha Arteta.

Lakini, Bruno anatarajiwa kuleta nini kwenye safu ya kiungo ya Arsenal msimu wa 2026/27 na kuendelea?

Takwimu za OPTA zinaonyesha kwa kina kile ambacho mashabiki wa Arsenal wanaweza kutarajia kutoka kwa kiungo huyo mpya.

GIIM 01

NI MPIGANAJI WA KWELI

Katika mahojiano yake ya kwanza, Bruno alijitambulisha kama “shujaa” na kusisitiza kuwa “sitasalimu amri kamwe.”

Na takwimu zinaonekana kuthibitisha kauli hizo.

Hakuna mchezaji anayemkaribia Bruno Guimaraes kwa idadi ya mipira aliyopokonya tangu alipoanza kucheza Ligi Kuu England Februari 2022.

Mbrazil huyo amepokonya jumla ya mipira 1,030 katika kipindi hicho, takribani 40 zaidi ya anayemfuatia, James Tarkowski wa Everton.

Kwa upande wa viungo, mchezaji anayemkaribia zaidi ni Moises Caicedo wa Chelsea, ambaye amepokonya mara 867.

Bruno si tu kwamba anajua namna ya kupokonya mpira, bali mara tu anapoupata, inakuwa vigumu zaidi kwa wapinzani kuurudishia mpira huo.

Kiungo huyo ambaye sasa atavaa jezi yenye namba 39 ndiye anayeongoza Ligi Kuu England kwa idadi ya faulo alizoshinda tangu alipocheza mechi yake ya kwanza akiwa Newcastle.

Bruno ameshinda faulo 410 kutoka kwa wapinzani, zaidi ya 100 kuliko mchezaji anayemfuatia, John McGinn.

GIIM 02

MWANA-MARATHON

Kushinda faulo na kupokonya ni sehemu ya mchezo wa Bruno, lakini pia kiungo huyo ni mchezaji anayefahamu umuhimu wa kufunika eneo kubwa la uwanja katika kipindi chote cha mchezo.

Tangu Februari 2022, Bruno amekimbia jumla ya kilomita 1,640.8 katika mechi 153, akifikisha wastani wa karibu kilomita 11 kwa kila mchezo.

Katika kipindi cha miaka minne na nusu iliyopita, ni Bruno Fernandes pekee pamoja na kiungo wa Arsenal, Declan Rice, waliokimbia umbali mkubwa zaidi kuliko Bruno Guimaraes.

Ingawa Bruno amepata sifa nyingi kutokana na bidii yake na uwezo wa kushinda dueli katikati ya uwanja, ubunifu wake pia umemfanya kuwa miongoni mwa viungo wanaotafutwa zaidi barani Ulaya.

Tangu alipowasili England, mchango wake katika kufunga mabao na kutoa pasi za mwisho umeendelea kukua.

Na msimu uliopita, hakuna mchezaji wa Newcastle aliyefunga mabao mengi zaidi ya Bruno katika Ligi Kuu England.

Uwezo wake wa kutengeneza nafasi wakati mpira ukiwa kwenye mchezo wa kawaida ni silaha nyingine muhimu.

Miongoni mwa wachezaji waliotengeneza nafasi 200 au zaidi tangu Februari 2022, ni wachezaji wawili tu waliotengeneza asilimia kubwa zaidi ya nafasi kutoka kwenye mchezo wa kawaida kuliko Bruno.

Kati ya nafasi 213 alizotengeneza kiungo huyo, 197 zilitokana na mchezo wa kawaida, sawa na asilimia kubwa ya 92.5.

Uwezo wa kupeleka mpira mbele ni silaha nyingine muhimu aliyonayo Bruno.

Katika kipindi cha miaka minne na nusu iliyopita, ni kiungo mmoja pekee aliyepiga pasi za mbele 2,401 au zaidi kuliko Bruno.

Akiwa katika kiwango hicho, Bruno pia alikwenda nacho kwenye Kombe la Dunia.

Katika mechi tano alizocheza, alifanikiwa kutoa asisti nne, idadi ambayo ilizidiwa na mchezaji mmoja pekee, Michael Olise wa Ufaransa.

Pia, Bruno amekuwa mchezaji anayeaminika kutokana na uwezo wake wa kudumu katika kikosi.

Tangu alipowasili Newcastle wakati wa majira ya baridi ya mwaka 2022, amekosa mechi 16 tu za Ligi Kuu England.

GIIM 03

ANA NGUVU

Bruno aliwahi kueleza kuwa kucheza dhidi ya Arsenal ni “jambo gumu sana,” lakini kwa upande wa Arsenal, hali imekuwa hivyo hivyo.

Tangu alipocheza mechi yake ya kwanza kwenye Ligi Kuu England Februari 2022, Bruno amekimbia umbali mkubwa zaidi dhidi ya Arsenal kuliko timu nyingine yoyote, akiwa amefikisha kilomita 98.6.

Pia, amepokonya mipira 71 dhidi ya Arsenal, idadi ambayo ni kubwa kuliko dhidi ya timu nyingine yoyote.

Sasa swali ni: takwimu za Bruno zinasimama vipi ukilinganisha na viungo wenzake wapya Arsenal?

Katika msimu uliopita, usajili huyo mpya wa Arsenal:

Alifunga mabao 9;

Alishinda faulo 75;

Alishinda dueli 168;

Takwimu hizo zote zilikuwa juu kuliko za kiungo yeyote wa Arsenal.

BRUN 01

NAMBA ZINASEMA

Ukiangalia takwimu kwa wastani wa dakika 90, inaonekana wazi kwa nini Mikel Arteta ameamua kumuongeza Bruno Guimaraes kwenye kikosi chake kuelekea msimu wa 2026/27.

Uwezo wake wa kupokonya, kukimbia umbali mrefu, kushinda faulo, kupeleka mpira mbele, kutengeneza nafasi, kutoa pasi za mwisho na kufanya presha kubwa unaonyesha kuwa Arsenal imeongeza kiungo mwenye uwezo wa kufanya kazi katika maeneo mbalimbali ya uwanja.

Kwa kifupi, Bruno si kiungo anayesubiri mpira umfuate. Ni mchezaji anayekwenda kuutafuta, kuupigania na kuusogeza mbele.

Na kwa Arteta, ujio wake unamaanisha kuongeza nguvu, ubunifu, ukakamavu na kasi ya kazi katikati ya uwanja wakati Arsenal ikijiandaa kwa kampeni ya 2026/27 na miaka inayofuata, mipira ya vurugu ya kona sasa imepata mwenyewe.