Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

BIG BOSS VINI JR: Wasaudia wataka kuvunja rekodi

Muktasari:

  • Vinicius Jr, 25, anasakwa na vigogo wa ligi hiyo ya Mashariki ya Kati baada ya kusikia kwamba amekuwa kwenye kusumbuana na Real Madrid juu ya dili jipya.

MADRID, HISPANIA: MABOSI wa Saudi Pro League wanafikiria mpango wa kuvunja rekodi ya dunia kwenye uhamisho wa wanasoka, wakipanga kumchukua supastaa wa Real Madrid, Vinicius Jr.

Vinicius Jr, 25, anasakwa na vigogo wa ligi hiyo ya Mashariki ya Kati baada ya kusikia kwamba amekuwa kwenye kusumbuana na Real Madrid juu ya dili jipya.

Winga huyo wa Kibrazili anatajwa kama moja ya wachezaji bora kabisa duniani na kwa mujibu wa TalkSPORT, mabosi wa Saudia wanamtaka mchezaji huyo akacheze kwenye Saudi Pro League akiwa bado kwenye kiwango bora kabisa cha soka lake.

Kinachoelezwa ni kwamba mabosi hao wa Saudia wamepanga kuipa Real Madrid ofa yenye thamani ya Pauni 302 milioni kuwashawishi ili Vinicius Jr akacheze kwao.

Ofa hiyo itavunja rekodi ya uhamisho inayoshikilia dunia kwa sasa ya Pauni 200 milioni, ambayo Paris Saint-Germain ililipa kupata saini ya Neymar mwaka 2017.

Na itazidi ile ofa ya Al-Hilal ya Pauni 257 milioni ambayo ilikataliwa katika mpango wao wa kumchukua supastaa wa Ufaransa, Kylian Mbappe wakati alipokuwa PSG, 2023.

Mabosi hao wa Saudia wanashawishika juu ya kumfukuzia staa huyo wa Kibrazili baada ya kuona kwamba hakuna tangazo lolote la kuhusu mkataba mpya Santiago Bernabeu.

Vinicius yupo kwenye mazungumzo ya kuhusu dili jipya baada ya hili la sasa kufikia tamati kwenye dirisha la majira ya kiangazi 2027.

Wadau wakubwa wa Saudia wameweka malengo yao makubwa katika kunasa saini ya Vinicius Jr na hata kama atasaini dili la kubaki Hispania, mpango huo utaendelea hata kwa baadaye. Na Al Ahli inatajwa kwamba ndiyo inayopigiwa debe Vini Jr akacheze huko, ikiwa ni moja ya timu iliyopo chini ya Public Investment Fund (PIF) na Waziri wa Michezo wa Saudia anaamini huyo ni staa mkubwa ajaye kwenye ligi yao.

Vinicius Jr aliwahi kusema hadharani kwamba dhamira yake ni kubaki Real Madrid, lakini anaweza kushawishika kwa dili hilo tamu lililowekwa mezani na Saudi Arabia.

Imeelezwa kwamba staa huyo wa zamani wa Flamengo amewekewa mezani ofa ya dili la miaka mitano lenye thamani ya Pauni 866 milioni na bonasi nyingine kibao.

Kiwango cha pesa kama hiyo itamfanya Vinicius Jr kuwa mmoja wa wachezaji wanaolipwa pesa nyingi duniani, akilipwa Pauni 475,000 kwa wiku au Pauni 3.3 milioni kwa wiki. Ukitaka kufahamu kwamba pesa hiyo si ya mchezo, linganisha na mchezaji anayelipwa pesa nyingi zaidi kwenye Ligi Kuu England, Erling Haaland, anayelipwa Pauni 525,000 kwa wiki, ambayo ni karibu mara tano ya kiwango ambacho Vini Jr atakwenda kulipwa atakapoamua kutimkia Saudia.

Kwa kifupi tu, Vini Jr atakuwa analipwa Pauni 19,829 kwa saa na Pauni 330 kwa kila dakika. Staa huyo alifunga mabao 22 na kuasisti 19 kwenye mechi 58 alizochezea Real Madrid msimu uliopita. Saudia ni kivutio cha mastaa wengi wa soka la Ulaya, ikiwamo Cristiano Ronaldo, Karim Benzema, Ivan Toney na Sadio Mane kwa kuwataja kwa uchache, ambao kwa sasa wanakipiga kwenye ligi hiyo, Saudi Pro League.