Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Benitez ampeleka Trent Bernabeu

Benitez Pict

Muktasari:

  • Alexander-Arnold ni mmoja wa mastaa wa Liverpool - sambamba na Virgil van Dijk na Mohamed Salah - ambao mikataba yao itafika ukomo mwisho wa msimu huu na hakuna dalili ya kusaini dili mpya.

MADRID, HISPANIA: ALIYEKUWA kocha wa Liverpool, Rafa Benitez amekiri beki Trent Alexander-Arnold atakwenda kuwa moto zaidi kwenye kikosi cha Real Madrid, wakati huu uvumi ukiwa mkubwa juu ya mpango wa kwenda kukipiga kwenye kikosi hicho cha Bernabeu.

Alexander-Arnold ni mmoja wa mastaa wa Liverpool - sambamba na Virgil van Dijk na Mohamed Salah - ambao mikataba yao itafika ukomo mwisho wa msimu huu na hakuna dalili ya kusaini dili mpya.

Trent, 26, amekuwa kwenye kikosi cha Liverpool tangu alipokuwa na umri wa miaka sita, amecheza zaidi ya mechi 342 na kushinda mataji kadhaa na timu hiyo, ikiwamo Ligi Kuu England na Ligi ya Mabingwa Ulaya.

Na sasa, Mwingereza huyo anajipanga na changamoto mpya kwenye dirisha lijalo la majira ya kiangazi, jambo lililomwibua kocha wa zamani wa Liverpool, Benitez kuamini uchezaji wa Alexander-Arnold utakwenda kufiti vyema katika kikosi cha kocha Carlo Ancelotti.

"Real Madrid ni timu ya kushambulia, wao ni timu bora Hispania na wataendelea kuwa bora," alisema.

"Hata kama Barcelona au Atletico Madrid zitafanya vizuri, Real Madrid bado itaendelea kuwa bora, hivyo hali itakuwa hivyo. Kwa beki wa kushambulia kuna nafasi kubwa ya kuasisti na kufanya mashambulizi ya kutosha. Kile anachofanya Liverpool hakinishangazi, lakini Real Madrid itampa uhakika wa kutamba miaka mingi."

Alexander-Arnold amefunga mabao mawili na kuasisti mara saba katika michuano yote akiichezea Liverpool msimu huu na msimu huu ipo kwenye nafasi kubwa ya kushinda taji la Ligi Kuu England chini ya kocha wao mpya Mdachi Arne Slot. Kwenye kikosi cha Madrid, upande wa kulia una mabeki kama Raul Asencio, Lucas Vasquez na Federico Valverde.