Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Bellingham apokewa kishujaa Birmingham

Muktasari:

  • Barcelona ilisafiri kutoka Hispania hadi kwenye Uwanja wa St Andrew’s kucheza mechi ya kirafiki ya maandalizi ya msimu mpya dhidi ya Birmingham City inayoshiriki Championship, jambo lililowapa mashabiki wa Blues nafasi adimu ya kuwaona mabingwa wa La Liga wakicheza mbele yao.

BIRMINGHAM, ENGLAND: JUDE Bellingham alipokewa kama shujaa na mashabiki wa Birmingham City juzi usiku aliporejea kwenye uwanja wa klabu yake ya utotoni na kushuhudia timu hiyo ikiifunga Barcelona kwa mikwaju ya penalti.

Barcelona ilisafiri kutoka Hispania hadi kwenye Uwanja wa St Andrew’s kucheza mechi ya kirafiki ya maandalizi ya msimu mpya dhidi ya Birmingham City inayoshiriki Championship, jambo lililowapa mashabiki wa Blues nafasi adimu ya kuwaona mabingwa wa La Liga wakicheza mbele yao.

Hata hivyo, tukio hilo lilikuwa maalumu zaidi kwa mashabiki wa Birmingham baada ya kiungo nyota wa England,  Bellingham, kutambulishwa kabla ya mchezo kuanza.

Bellingham alianza safari yake ya soka katika akademi ya Birmingham kabla ya kuondoka 2020 kwenda Borussia Dortmund, kisha baadaye kujiunga na Real Madrid 2023 ambako ameendelea kung’ara na kuwa mmoja wa viungo bora zaidi duniani.

Kabla ya mchezo kuanza, akaunti rasmi ya mitandao ya kijamii ya Birmingham City ilichapisha video ya Bellingham akikaa uwanjani na kuwasalimia mashabiki ikiwa na ujumbe:

“Jude. Ametimiza ndoto ya kurejea nyumbani.”

Alipoinua mikono yake kuwasalimia mashabiki waliokuwa wakimshangilia, wao walilipuka kwa kelele wakitamka jina lake: “Jude!” Kisha wakaendelea kuimba: “Yeye ni mmoja wetu.” Ilikuwa ni wakati wa kipekee kwa kiungo huyo wa England ambaye bado anapumzika baada ya kuwa sehemu muhimu ya kikosi cha timu ya taifa katika Kombe la Dunia la mwaka huu, hivyo hajarejea Real Madrid kuanza maandalizi ya msimu mpya chini.

Bellingham alishangilia kwa furaha wakati Birmingham City ikiibuka na ushindi dhidi ya wapinzani wakubwa wa Real Madrid, Barcelona, baada ya sare ya mabao 2-2 katika dakika 90 na kushinda kwa penalti 3-2.

Birmingham City ilistaafisha rasmi jezi yake namba 22 kwa heshima yake. Ingawa aliwasili St Andrew’s akiwa amevaa fulana nyeupe, Bellingham aliondoka akiwa amevalia jezi yake ya zamani ya Birmingham yenye namba 22.