Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Beki afichua siri za Slot

Muktasari:

  • Polen ambaye kwa sasa ni mchambuzi wa michezo anasema kuna muda Slot alikuwa anawaambia hadi mabeki wacheze rafu kwa washambuliaji wakiwa mazoezini ili kufanya mazoezi yachangamke.

LIVERPOOL, ENGLAND: BEKI wa zamani wa  PEC Zwoll,  Bram van Polen  ambaye aliwahi kufundishwa na Arne Slot amemwelezea kocha huyo kama mmoja wa walimu wakali kuwahi kufundishwa nao na asiyekuwa na masihara hata kidogo mazoezini au katika mechi.

Polen ambaye kwa sasa ni mchambuzi wa michezo anasema kuna muda Slot alikuwa anawaambia hadi mabeki wacheze rafu kwa washambuliaji wakiwa mazoezini ili kufanya mazoezi yachangamke.

“Slot hutumia akili nyingi kwenye  vipindi vyake vyote vya mazoezi. Anahitaji kila mchezaji aonyeshe kiwango na maelekezo yake yafuatwe na wasipofanya hivyo huwa anabadilika kabisa,” alisema Van Polen.

“Ilikuwa timu isipofanya vizuri anakuja kwangu na kabla ya mazoezi ananiambia  nicheze rafu kwa washambuliaji na wachezaji wengine na mimi nilikuwa nikipenda sana maelekezo hayo.”

Liverpool imeilipa Feynoord Pauni 11 milioni kwa ajili ya kuvunja mkataba wake na wamelipa Pauni 320,000 ambao ni mshahara wa mwezi wa mmoja wa kocha huyo.

Ukiondoa ukali awapo mazoezini na katika mechi, Slot pia anafananishwa na Jose Mourinho kutokana na maneno yake ya karaha.

Mara kadhaa alizowahi kukutana na Mourinho katika michuano ya kimataifa alimshauri kocha huyo awe anatazama mechi za Pep Guardiola kwa sababu kuna vitu atakuwa anajifunza ili aongeze ujuzi wake.

Mourinho alimjibu kwa kumwambia yeye ndio awe anatazama mechi zake kwani kwa kufanya hivyo atakuwa anajifunza namna ya kushinda mataji makubwa.

Pia Diego Simeone naye aliwahi kulalamika juu ya kauli za shombo alizopewa na Slot alipokutana naye katika michuano ya kimataifa.

“Slot alikuwa na ujasiri wa kuniambia nilikuwa nimechanganyikiwa katika mechi na hakuna jambo la maana ambalo nilelifanya, kauli kama zile mimi siwezi kumwambia kocha mwenzangu.”