Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Kadi ya njano Uefa ‘yaundiwa zengwe’

Muktasari:

  • Mpango huo ni sawa na kuundiwa zengwe kwa kadi hizo na waamuzi wenye uchu wa kumzimwaga ambao unalenga kupunguza adhabu ili kulifanya boli litembee zaidi uwanjani.

NYON, USWISI: WAKATI hatua za makundi ya Ligi ya Mabingwa Ulaya zikitarajiwa kupangwa hivi karibuni, wachezaji na klabu shiriki wanaweza kuepukana na kufungiwa kutokana na kadi za njano msimu ujao, baada ya Shirikisho la Soka Ulaya (Uefa), kubadili kanuni za adhabu ili kuendana na mfumo mpya wa mashindano.

Mpango huo ni sawa na kuundiwa zengwe kwa kadi hizo na waamuzi wenye uchu wa kumzimwaga ambao unalenga kupunguza adhabu ili kulifanya boli litembee zaidi uwanjani.

Awali, baada ya Uefa kuanzisha mfumo mpya wa Ligi ya Mabingwa iliongeza idadi ya mechi katika hatua ya ligi kutoka sita hadi nane, huku ikiweka pia raundi ya mchujo ya hatua ya 16 bora inayochezwa kwa mechi mbili kwa timu zitakazomaliza nafasi ya tisa hadi ya 24.

Hii ilimaanisha kuwa klabu inaweza kucheza hadi mechi 17 katika safari yake ya kutwaa ubingwa, tofauti na kiwango cha juu cha mechi 13 katika mfumo wa zamani. Hata hivyo, Uefa awali iliendelea kutumia kiwango kilekile cha kadi za njano kinachosababisha mchezaji kufungiwa.

Chini ya mfumo wa zamani, mchezaji aliyefikisha kadi tatu za njano alifungiwa mechi moja, huku adhabu nyingine zikifuata baada ya kufikisha kadi ya tano, ya saba na kadi nyingine zinazofuata zenye idadi witiri. Lakini hilo limebadilika kuanzia msimu wa 2026/27.

Na sasa mchezaji atalazimika kufikisha kadi nne za njano ili kupata adhabu yake ya kwanza ya kufungiwa mechi moja. Baada ya hapo, adhabu nyingine zitatolewa akifikisha idadi inayofuata ya kadi zilizo shufwa, ikiwemo kadi ya sita, ya nane na ya 10.

Mabadiliko hayo yanawapa wachezaji nafasi kubwa zaidi ya kucheza bila kufungiwa katika kampeni ya Ligi ya Mabingwa Ulaya ambayo kwa sasa ni ndefu zaidi.

Kifungu kipya cha 63.02b cha kanuni za mashindano hayo kinaeleza kuwa kuanzia mchezo wa kwanza wa hatua ya ligi, wachezaji na maofisa wa timu watafungiwa mechi inayofuata baada ya kufikisha kadi nne za njano ambazo hazikuambatana na kadi nyekundu.

Adhabu nyingine zitafuata baada ya kadi za idadi shufwa kama vile ya sita na ya nane.

Jambo moja muhimu katika mfumo wa nidhamu limeendelea kubaki vilevile, ambapo kadi za njano hufutwa baada ya kumalizika kwa robo fainali na hazihamishwi kwenda hatua ya nusu fainali.

Kanuni hiyo inalenga kupunguza uwezekano wa mchezaji kukosa fainali ya Ligi ya Mabingwa kutokana tu na kuwa amekusanya kadi nyingi za njano.

Hata hivyo, iwapo mchezaji atafungiwa katika mchezo wa pili wa robo fainali atalazimika kuitumikia adhabu hiyo katika mchezo unaofuata.

Mchezaji pia anaweza kukosa fainali kutokana na kupewa kadi nyekundu au adhabu nyingine ya kinidhamu. Upande mwingine wa kanuni, Uefa imefanya pia mabadiliko, ambapo saa za uwanjani hazitalazimika tena kusimamishwa zinapofikisha dakika 45 na 90 na badala yake zitaendelea kuhesabu muda wakati wa dakika za nyongeza.

Vilevile katika kuhakikisha kwamba mashindano yote ya ngazi yanayosimamiwa na Uefa yanakuwa na ufanisi, shirikisho limetoa mwongozo mwingine unaowabana waamuzi ambapo ‘Clear Line’ ambayo kama maktaba ya video za waamuzi itakuwa inatoa fursa ya kipekee ya kutoa kwa uwazi miongozo ambayo inawapa waamuzi na waamuzi wa VAR, fursa ya kutekeleza kwa usawa na ufanisi wa sheria za mchezo katika maeneo yote ya Ulaya.