Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Barca yamgeukia Joao Pedro kisa Julian Alvarez

Muktasari:

  • Tovuti ya  Mundo Deportivo, imefafanua kuwa Barcelona inaamini Pedro mwenye umri wa miaka 24 anaweza kupatikana kwa bei rahisi zaidi tofauti na ilivyo kwa Alvarez.

BARCELONA inaripotiwa kupunguza spidi kuwania saini ya mshambuliaji wa Atletico Madrid na timu ya taifa ya Argentina, Julian Alvarez, iliyetaka kumsajili  katika dirisha lijalo la majira ya kiangazi na badala yake imeelekeza macho na masikio kwa staa wa Chelsea, Joao Pedro.

Tovuti ya  Mundo Deportivo, imefafanua kuwa Barcelona inaamini Pedro mwenye umri wa miaka 24 anaweza kupatikana kwa bei rahisi zaidi tofauti na ilivyo kwa Alvarez.

Taarifa zinaeleza kuwa gharama kubwa pamoja na ushindani wa kumpata Alvarez zimeifanya Barcelona kuanza kutafuta mbadala.

Pedro ameendelea kuvutia kutokana na uwezo wake wa kucheza nafasi mbalimbali katika safu ya ushambuliaji na gharama yake kuonekana kuwa nafuu. Staa huyo ni mmoja kati ya wachezaji walioonyesha viwango bora msimu huu akiwa na Chelsea ambapo amefunga mabao 20.


Paulo Dybala

MSHAMBULIAJI wa AS Roma na Argentina, Paulo Dybala, anaripotiwa kuwa tayari kusikiliza ofa za klabu Ligi Kuu England katika dirisha lijalo la majira ya kiangazi. Kwa mujibu wa Sky Sports, nyota huyo mwenye umri wa miaka 32, mkataba wake na Roma unamalizika mwisho wa msimu huu na hadi sasa hakuna mazungumzo ya mkataba mpya. Taarifa zinaeleza kuwa miongoni mwa klabu zinazohitaji saini yake ni Aston Villa.


Jarrod Bowen

CHELSEA, Liverpool na Manchester United zinaripotiwa kuonyesha nia ya kumsajili mshambuliaji wa West Ham United na England, Jarrod Bowen, kuelekea dirisha lijalo la majira ya kiangazi. Kwa mujibu wa tovuti Guardian, Bowen, 29, ameonekana kuwa mmoja wa wachezaji muhimu zaidi wanaoweza kuondoka West Ham ikiwa hali ya klabu itakuwa ngumu kifedha baada ya kushuka daraja. Bowen amekuwa tegemeo kikosini.


Matt O’Riley

ATLETICO Madrid na Borussia Dortmund zinadaiwa kuwa katika vita ya kuwania saini ya kiungo wa Brighton na Denmark, Matt O’Riley. Kwa mujibu wa Teamtalk, nyota huyo mwenye umri wa miaka 25 ameendelea kuvutia vigogo wa Ulaya kutokana na uwezo wake mkubwa wa kuchezesha timu. Taarifa hizo pia zinaeleza kuwa kocha wa Tottenham Hotspur, Roberto De Zerbi anamkubali sana O’Riley na huenda atapendekeza jina lake ili asajiliwe.


Federico Valverde

REAL Madrid inaripotiwa kuwa tayari kusikiliza ofa kwa ajili ya kumuuza kiungo raia wa Uruguay, Federico Valverde, katika dirisha lijalo la majira ya kiangazi. Taarifa kutoka tovuti ya Mundo Deportivo zinaeleza kwamba, Madrid inaweza kusikiliza ofa kwa ajili ya kumuuza Valverde kwa sababu hana furaha na anahitaji kuondoka kutafuta changamoto mpya akiwindwa sana na Manchester United.


Joao Gomes

ARSENAL bado haijakata tamaa katika harakati zao za kuiwania saini ya  kiungo wa Wolves na timu ya taifa ya Brazil, Joao Gomes mwenye umri wa miaka 25, kuelekea dirisha lijalo la majira ya kiangazi. Ripoti za awali zilieleza kuwa Gomes yuko karibu kufikia makubaliano na Atletico Madrid ambayo yeye ndio chaguo lake kwa sasa, lakini sasa mambo yanaweza kubadilika. Kiungo huyo amekuwa akiwindwa na vigogo wengi Ulaya.


Jannik Schuster

WEST Ham United, Leeds United na Brighton zinapambana kuwania saini ya beki raia wa Austria, Jannik Schuster, 19, kutoka Red Bull Salzburg, ili kumsajili katika dirisha  lijalo la majira ya kiangazi. Brentford ilionekana kuwa mbele katika mbio hizo, lakini sasa ushindani kutoka klabu nyingine za Ligi Kuu England unaonekana kufanya  dili hilo kuwa gumu zaidi. Mkataba wake unaisha 2028.


Jack Grealish

EVERTON inafikiria kumsajili straika wa Everton na England, Jack Grealish ambaye msimu huu anacheza kwa mkopo katika kikosi hicho.Kwa mujibu wa vyanzo vya ndani,inaelezwa kuwa Everton imemuweka Grealish kama kipaumbele kikuu cha usajili katika dirisha lijalo baada ya kuvutiwa na kiwango alichoonyesha tangu kuanza kwa msimu huu.Hata hivyo, klabu hiyo italazimika kutoa mshahara mnono kumshawishi.