Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Baba Lamine Yamal amkataa mpenzi wa mwanae

YAMAL Pict

Muktasari:

  • Nasraoui amesema tofauti ya umri kati ya Yamal (19) na Ines (21) ni miongoni mwa sababu zinazoweza kumpoteza kijana wake na namna ambavyo bado anaendelea kujifunza kuhusu mahusiano.

BABA mzazi wa nyota wa Barcelona na Timu ya Taifa ya Hispania, Lamine Yamal, Mounir Nasraoui amesema kama angepewa nafasi ya kumshauri kijana wake kuhusu maisha yake ya mapenzi basi ni kuachana na mpenzi wake Ines Garcia.

Nasraoui amesema tofauti ya umri kati ya Yamal (19) na Ines (21) ni miongoni mwa sababu zinazoweza kumpoteza kijana wake na namna ambavyo bado anaendelea kujifunza kuhusu mahusiano.

Baba huyo amesema anatambua kuna mipaka ambayo haipaswi kuingiliwa katika maisha binafsi ya mwanae, akisisitiza kuwa sio jukumu lake kuingilia kila uamuzi wa Yamal.

Nasraoui pia alidai kuwa yeye binafsi anamkubali zaidi mpenzi wa zamani wa kijana wake ambaye ni msanii wa Argentina, Nicki Nicole, kuliko Inés.

YAMA 01

Akizungumzia hilo baba huyo amesema anatambua kuwa kuna mipaka ambayo haipaswi kuvukwa katika maisha binafsi ya mwanae, akisisitiza kuwa si jukumu lake kuingilia kila uamuzi wa Yamal.

Nasraoui amesema “Nawatakia mema hata hivyo. Ninachojali ni taaluma yake, na sitaki achanganye mapenzi ya uongo na mapenzi ya kweli. Mimi binafsi nampendelea Nicki Nicole kuliko Inés.”

YAMA 02

Pamoja na kutoa maoni hayo, Mounir alidai kuwa yeye na Yamal hawako karibu kiasi cha yeye kuweza kumuelekeza kila kitu kuhusu maisha yake. Hata hivyo, anasema winga huyo anasikiliza zaidi ushauri kutoka kwa mama yake pamoja na baba yake wa kambo, hivyo anaona ni muhimu kuheshimu nafasi zao katika maisha ya kijana huyo.

Wiki chache zilizopita kumezuka taarifa mitandaoni ya kwamba Ines ambaye ni mwanamitandao na ameachana na Yamal na sasa ni picha zilizosambaa zikimuonyesha kijana huyo akila bata na mwanamke mmoja akiwa baharini.

Hata hivyo, taarifa hizo zimeendelea kuwa mjadala mkubwa kwenye mitandao ya kijamii lakini si Yamal wala Ines mwenyewe aliyethibitisha hilo.