Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Atletico Madrid yampeleka Alvarez arsenal

ALVAREZ Pict

Muktasari:

  • Mustakabali wa Alvarez (26), umeendelea kuwa gumzo msimu huu wa usajili kutokana na kuvutiwa na huduma zake na miamba ya Hispania, Real Madrid na Barcelona, huku Arsenal pia ikitajwa kuwa miongoni mwa klabu zinazomtaka.

MADRID, HISPANIA: ATLETICO Madrid ipo tayari kumuuza mshambuliaji wake Julian Alvarez kwa Arsenal, lakini nyota huyo wa Argentina hana mpango wa kuhamia Emirates, kwa mujibu wa taarifa kutoka Hispania.

Mustakabali wa Alvarez (26), umeendelea kuwa gumzo msimu huu wa usajili kutokana na kuvutiwa na huduma zake na miamba ya Hispania, Real Madrid na Barcelona, huku Arsenal pia ikitajwa kuwa miongoni mwa klabu zinazomtaka.

Kwa mujibu wa gazeti la Hispania, Mundo Deportivo, Alvarez ambaye awali aliwahi kuichezea Manchester City, anataka kujiunga na Barcelona pekee endapo ataondoka Atletico Madrid.

Atletico imekuwa ikifanya kila linalowezekana kumbakiza mshambuliaji huyo, lakini viongozi wa klabu hiyo sasa wanaaminika kukubali kuwa hali yake imekuwa “isiyovumilika” katika klabu hiyo ya Madrid.

ALVA 02

Taarifa zinaeleza kuwa Atletico iko tayari kuruhusu Alvarez kuhamia Arsenal ikiwa klabu hiyo itawasilisha ofa inayokidhi mahitaji yao.

Hata hivyo, kwa sasa Alvarez anaonekana kusimamia msimamo wake wa kutaka kuhamia Barcelona.

Atletico inatambua kuwa itakuwa vigumu kumpata mshambuliaji mbadala wa kiwango cha Alvarez iwapo itaamua kumuuza, hasa ikizingatiwa kuwa dirisha la usajili limebakiza chini ya wiki mbili kufungwa.

Katika mpango huo, Arsenal inaweza kumruhusu Viktor Gyokeres kuhamia Atletico Madrid kama sehemu ya uwezekano wa kubadilishana washambuliaji, huku kocha Diego Simeone akiripotiwa kuwa tayari kumpokea mshambuliaji huyo raia wa Sweden.

Arsenal pia inadaiwa kumweka Gyokeres sokoni msimu huu, mwaka mmoja tu baada ya kumsajili kutoka Sporting CP kwa ada ya pauni63.5 milioni.

Miongoni mwa klabu ambazo zimehusishwa na kupewa nafasi ya kumsajili Gyokeres ni Barcelona.

Gyokeres aliyetokea benchi na kucheza dakika 15 katika mchezo wa Ngao ya Jamii wikiendi iliyopita, alifunga mabao 14 katika Ligi Kuu England msimu wake wa kwanza akiwa Arsenal.

ALVA 01

Arsenal inataka kumsajili mshambuliaji mkubwa msimu huu kama sehemu ya mpango wa kuimarisha safu yake ya ushambuliaji.

Mapema msimu huu wa usajili, ilikosa nafasi ya kumsajili Vinicius Junior baada ya nyota huyo kuamua kusaini mkataba mpya wa kuendelea kuichezea Real Madrid.

Mwezi uliopita, kocha wa Arsenal, Mikel Arteta, 44, alikiri kuwa anatamani klabu hiyo ifanye usajili mkubwa utakaobadili kiwango cha kikosi.

Arteta amesema wanatambua wanachohitaji kufanya ili kuipeleka Arsenal katika kiwango kingine, akisisitiza kuwa hilo litahitaji kikosi bora zaidi pamoja na wachezaji wenye uwezo mkubwa.

Amesema klabu imebaini maeneo ambayo inahitaji kuimarika na kubadilika ili kufikia malengo yake, huku akitarajia mipango hiyo kuanza kutekelezwa hivi karibuni.

Wakati huo huo, Alvarez hakushiriki katika mchezo wa Atletico Madrid dhidi ya Malaga uliochezwa Jumatano usiku, ambapo Atletico iliibuka na ushindi dhidi ya timu hiyo mpya katika Ligi Kuu Hispania.