Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Arsenal yaingia anga za Liverpool

ARSENAL Pict

Muktasari:

  • Arsenal ilikuwa imeweka mpango mkubwa wa kumsajili Vinicius kutoka Real Madrid, lakini matumaini hayo yalizimwa baada ya winga huyo wa Brazil kusaini mkataba mpya wa miaka sita wa kubaki Santiago Bernabeu.

LONDON, ENGLAND: ARSENAL baada ya kumkosa Vinicius Junior imeanza kuangalia uwezekano wa kumnasa winga wa Paris Saint-Germain, Bradley Barcola, katika hatua ambayo inaweza kuivuruga mipango ya Liverpool ya kumsajili nyota huyo.

Arsenal ilikuwa imeweka mpango mkubwa wa kumsajili Vinicius kutoka Real Madrid, lakini matumaini hayo yalizimwa baada ya winga huyo wa Brazil kusaini mkataba mpya wa miaka sita wa kubaki Santiago Bernabeu.

Vinicius, ambaye awali alikuwa amebakiza mwaka mmoja katika mkataba wake, amekubali mkataba mpya unaomlipa takribani £480,000 kwa wiki, hivyo kuifanya Arsenal iondoke kwenye mbio za kumsajili.

ARS 01

Licha ya kukosa Vinicius, Arsenal bado inaendelea kusaka winga mpya wa upande wa kushoto, hasa baada ya kumruhusu Leandro Trossard kuondoka na kujiunga na Besiktas.

Kwa mujibu wa Independent, Barcola ni mmoja wa wachezaji wanaovutia Arsenal, ingawa klabu hiyo italazimika kuongeza kasi kwa sababu Liverpool tayari imeanza mazungumzo kuhusu masharti binafsi ya mchezaji huyo.

Liverpool inamuhitaji Barcola kama sehemu ya mpango wake wa kujenga upya safu ya ushambuliaji baada ya kuondoka kwa Mohamed Salah.

Hata hivyo, dili hilo limekwama kutokana na bei kubwa inayotajwa na PSG, ambayo inadaiwa kutaka takribani pauni 130 milioni kwa ajili ya kumwachia nyota huyo mwenye umri wa miaka 23.

Taarifa kutoka Ufaransa zimeeleza kuwa Liverpool tayari imeiambia PSG haina uwezo wa kufikia kiwango hicho cha fedha, jambo ambalo linaweza kuipa Arsenal nafasi ya kuingia kwenye mbio hizo.

Barcola alijiunga na PSG akitokea Lyon mwaka 2023 na tangu wakati huo ameichezea klabu hiyo mara 152 katika mashindano yote, akifunga mabao 39.

ARS 02

Katika kipindi hicho amesaidia PSG kutwaa mataji mawili ya Ligi ya Mabingwa Ulaya pamoja na mataji matatu ya Ligue 1.

Msimu uliopita alikuwa sehemu ya kikosi cha PSG kilichokutana na Arsenal katika fainali ya Ligi ya Mabingwa, akianza benchi kabla ya kuingia dakika ya 83 katika ushindi wa PSG.

Hata hivyo, nafasi yake katika kikosi cha kwanza inaweza kuwa hatarini kutokana na shughuli za PSG kwenye dirisha hili la usajili.

Baada ya kuondoka kwa Lee Kang-in, Goncalo Ramos na Randal Kolo Muani, PSG imemsajili mshambuliaji wa kimataifa wa Ufaransa, Maghnes Akliouche, huku pia ikimfuatilia winga wa Ajax, Mika Godts.

Mshambuliaji wa Barcelona, Ferran Torres, ambaye pia amekuwa akihusishwa na klabu hiyo, anaongeza ushindani katika safu ya ushambuliaji ya mabingwa hao wa Ufaransa.

ARS 03

ARSENAL INA CHAGUO JINGINE

Mbali na Barcola, Arsenal pia inamfikiria mshambuliaji wa Atletico Madrid, Julian Alvarez.

Hata hivyo, usajili huo unaonekana kuwa mgumu kukamilika kwa sababu mshambuliaji huyo wa zamani wa Manchester City anaonekana kuwa na uwezekano mkubwa wa kubaki LaLiga.

Chaguo jingine ni mshambuliaji wa Everton, Iliman Ndiaye, ambaye mustakabali wake Goodison Park haujawa na uhakika.

Klabu ya Al-Hilal ya Saudi Arabia pia imeonyesha nia ya kumsajili Ndiaye, jambo linaloweza kuongeza ushindani katika mbio za kumpata.

Wakati Arsenal ikiendelea na harakati za usajili, kocha Mikel Arteta amesisitiza umuhimu wa kikosi chake kuwa na njaa ya mafanikio baada ya kuanza maandalizi ya msimu kwa matokeo yasiyoridhisha.

Arsenal ilipoteza kwa mabao 3-1 dhidi ya Real Betis mjini Dublin mapema wiki hii, lakini Arteta alisema amefurahishwa na namna wachezaji walivyopokea kipigo hicho.

“Wamekasirika sana, wamepata wakati mgumu. Wamefura, lakini hili ni jambo zuri. Hicho ndicho tunachohitaji,” alisema Arteta.

Sasa Arsenal inatazamiwa kuongeza nguvu katika harakati za kumsajili winga mpya, huku Barcola akiwa miongoni mwa majina yanayoonekana kuwa kwenye orodha ya mastaa wanaoweza kuziba pengo lililoachwa kwenye safu hiyo.