Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Arteta awatuliza mashabiki wa Arsenal

ARTETA Pict

Muktasari:

  • Arteta, ambaye mkataba wake wa sasa umebakiza miezi 12, anatarajiwa kupewa mkataba mpya utakaoambatana na nyongeza ya mshahara kutoka pauni milioni 10 (zaidi ya Sh25 bilioni) kwa mwaka.

LONDON, ENGLAND: KOCHA wa Arsenal, Mikel Arteta amewataka mashabiki wa klabu hiyo kutokuwa na wasiwasi kuhusu mustakabali wake baada ya kutoa ishara kuwa yuko tayari kuongeza mkataba wake na kikosi hicho.

Arteta, ambaye mkataba wake wa sasa umebakiza miezi 12, anatarajiwa kupewa mkataba mpya utakaoambatana na nyongeza ya mshahara kutoka pauni milioni 10 (zaidi ya Sh25 bilioni) kwa mwaka.

Kocha huyo amekuwa sehemu muhimu ya mafanikio ya Arsenal, ikiwamo kuiongoza kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu msimu uliopita, jambo lililoifanya klabu hiyo kutaka kumfunga kwa mkataba mpya.

Akizungumza kabla ya mchezo wa Ngao ya Jamii dhidi ya Manchester City utakaopigwa Cardiff jana, Arteta amesema mashabiki hawapaswi kuwa na hofu kuhusu suala hilo.

ART 01

“Mashabiki hawana haja ya kuwa na wasiwasi kuhusu hilo kwa sababu nataka kuwa hapa. Nina furaha sana. Ninajisikia mwenye shukrani kufanya kazi na watu ninaofanya nao kazi na tutakapopata nafasi, tutalitatua suala hilo,” amesema.

Arteta aliongeza: “Daima kuna jambo lingine la kupewa kipaumbele. Hivyo ndivyo tumekuwa tukilishughulikia kwa sababu kila mtu yuko huru kuwa na imani kuwa muda uliobaki kwenye mkataba hautakuwa tatizo.

“Nia yangu ni kubaki hapa na nina furaha. Hisia zangu kuhusu klabu ni zilezile. Ndiyo maana kila kitu kinaendelea kwa utaratibu mzuri.”

ART 02

Wakati huohuo, Arsenal bado inaendelea kusaka mshambuliaji mpya, lakini Arteta amekiri kushangazwa na gharama kubwa za usajili katika dirisha hili.

Arsenal ilikuwa ikimfuatilia Morgan Rogers kabla mchezaji huyo kujiunga na Chelsea kwa ada ya pauni milioni 117 (zaidi ya Sh292 bilioni).

“Ndiyo, nimeshangazwa. Sikutegemea kabisa. Huo ndiyo mwenendo wa soko. Ina maana kuna klabu ambazo ziko tayari kuwekeza au zinaamini thamani ya wachezaji hao ni hiyo, na hilo ni jambo linalokubalika,” amesema.

ART 03

Arteta pia alikataa kuzungumzia taarifa za Arsenal kuwafuatilia mabeki Ezri Konsa na Jarell Quansah, lakini alitoa taarifa nzuri kuhusu hali ya baadhi ya wachezaji wake kabla ya mchezo dhidi ya City.

Bukayo Saka, Declan Rice na Martin Zubimendi walikosa mchezo wa kirafiki dhidi ya Como Jumatano iliyopita, lakini wote wanatarajiwa kurejea kikosini.

Arteta amesema kwa William Saliba, kama tunavyojua, ana jeraha linalohitaji muda mrefu zaidi kupona.