Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Arsenal, Man City zatawala ubashiri wa ubingwa EPL

UBASHIRI Pict

Muktasari:

  • Katika kipindi cha miaka sita iliyopita, Manchester City imeshinda mataji manne ya Ligi Kuu, huku Arsenal ikimaliza nafasi ya pili kwa misimu mitatu mfululizo kabla ya kutwaa ubingwa wa kwanza baada ya miaka 22 msimu uliopita.

LONDON, ENGLAND: MABINGWA watetezi Arsenal pamoja na Manchester City zinaendelea kutajwa kuwa timu zenye nafasi kubwa zaidi ya kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu England msimu wa 2026/27, kufuatia ubora waliouonyesha katika miaka ya karibuni.

Katika kipindi cha miaka sita iliyopita, Manchester City imeshinda mataji manne ya Ligi Kuu, huku Arsenal ikimaliza nafasi ya pili kwa misimu mitatu mfululizo kabla ya kutwaa ubingwa wa kwanza baada ya miaka 22 msimu uliopita.

Msimu uliomalizika, Arsenal ilimaliza kileleni mwa msimamo na kutwaa taji, huku Manchester City ikishika nafasi ya pili.

UBA 01

Kwa kuwa timu zote mbili zimeendelea kuimarisha vikosi vyao kuelekea msimu mpya, zinatajwa tena kuwa vinara wa mbio za ubingwa.

Kutokana na matarajio hayo, kampuni za ubashiri zimeongeza ofa maalumu kwa wanaobashiri matokeo ya mwisho ya msimu.

Awali, ubashiri wa Arsenal kumaliza nafasi ya kwanza na Manchester City kushika nafasi ya pili ulikuwa ukilipwa kwa uwiano wa 5/1, lakini sasa umeongezwa hadi 7/1.

Hii ina maana kwamba anayebashiri mpangilio huo ukajirudia kama ulivyokuwa msimu uliopita atapata malipo makubwa zaidi endapo utatokea.

UBA 02

Kwa mujibu wa soko la sasa la ubashiri, Arsenal ndiyo ikipewa nafasi kubwa ya kutetea ubingwa ikiwa na odds za 6/4, huku Manchester City ikifuata kwa 11/4.

Kutokana na ushindani mkubwa kati ya vigogo hao wawili, wadau wengi wa soka wanaamini mbio za ubingwa zinaweza tena kuamuliwa kati ya Arsenal na Manchester City, kama ilivyokuwa msimu uliopita.