Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Arsenal haijakata tamaa kuinasa saini ya Rodrygo

Muktasari:

  • Rodrygo ni miongoni kwa wachezaji waliopewa ruhusa ya kuondoka katika dirisha hili na kocha Xabi Alonso kwa sababu hayupo katika mipango yake kwa msimu ujao.

ARSENAL bado ina nia ya kumsajili winga wa Real Madrid na timu ya taifa ya Brazil, Rodrygo, 24, licha ya kuwa karibu kukamilisha usajili wa mshambuliaji wa Chelsea raia wa England Noni Madueke, 23, dirisha hili.

Rodrygo ni miongoni kwa wachezaji waliopewa ruhusa ya kuondoka katika dirisha hili na kocha Xabi Alonso kwa sababu hayupo katika mipango yake kwa msimu ujao.

Mbali ya Arsenal saini yake pia imekuwa ikinyemelewa na Liverpool ambayo inamhitaji kama mbadala wa Luis Diaz anayeweza kutimkia Bayern Munich.

Awali ilielezwa washika mitutu hawa wameachana na mpango wa kumsajili staa huyu kwa sababu  Madrid ilihitaji Pauni 70 milioni ambazo kwao zilikuwa ni nyingi.

Mkataba wa Rodrygo unatarajiwa kumalizika mwaka 2028 na msimu uliopita alicheza mechi 54 za michuano yote na kufunga mabao 14.

Mbali ya Arsenal na Bayern, huduma ya Rodrygo pia inahitajika sana na Bayern Munich ambayo tayari imeshaanza mazungumzo na wawakilishi wake kuhakikisha inamsajili.

 Liverpool pia inamwangalia nyota huyu ambaye amekuwa na kiwango bora licha ya umri wake bado mdogo na inamwona kama mwafaka kwenda kuendeleza ubora wa safu ya ushambuliaji ya Majogoo hao inayoongozwa na Mohamed Salah.


Daniel Muno

LICHA ya kusaini mkataba mpya wa kuendelea kusalia katika kikosi cha kwanza cha Crystal Palace hadi mwaka 2028, beki kisiki wa Palace na timu ya taifa ya Colombia, Daniel Munoz, 29, yupo tayari kuondoka katika kikosi hicho katika dirisha hili ikiwa ofa nono itawekwa mezani kutoka kwa timu yoyote inayomhitaji. Nyota huyo msimu uliopita alicheza mechi 12 pekee na kufunga mabao mawili na hivyo hakuwa na nafasi kubwa ya kucheza na anataka kusepa.


Marco Asensio

KOCHA wa Fenerbahce  ya Uturuki, Jose Mourinho amependekeza jina la kiungo mshambuliaji wa  Paris Saint-Germain na timu ya taifa ya Hispania, Marco Asensio, 29, akitaka asajiliwe katika dirisha hili.Asensio mkataba wake wa sasa unatarajiwa kumalizika mwakani na msimu uliopita alicheza mechi 37 za michuano yote na kufunga mabao10, huku katika Ligi Kuu England akifunga mabao matatu katika mechi 13 na kuasisti mara moja.


Rasmus Hojlund

MSHAMBULIAJI wa Manchester United, Rasmus Hojlund 22, ni miongoni mwa wachezaji ambao Inter Milan imewaweka katika vipaumbele vyao kwa ajili ya kuwasajili katika dirisha hili la majira ya kiangazi. Hojlund ambaye msimu uliopita akiwa na Man United alicheza mechi 52 za michuano yote na kufunga mabao 52. Mkataba wake unatarajiwa kumalizika mwaka 2028.

Chemsdine Talbi

SUNDERLAND iko karibu kukamilisha dili la kumsajili mshambuliaji wa Club Brugge na timu ya taifa ya Morocco, Chemsdine Talbi mwenye umri wa miaka 20 ambaye msimu uliopita alicheza mechi 44 za michuano yote na kufunga mabao saba. Mkataba wake wa sasa unatarajiwa kumalizika mwaka 2027 na kuna uwezekano mkubwa akatua Ligi Kuu England.Igeniatiis moluptaturem quat veris ea voluptatem none omnim es molum, ulparunt vel excea num volu


Mark Travers

EVERTON inataka kumsajili kipa wa Bournemouth mwenye miaka 26, Mark Travers, ambaye aliwavutia akiwa kwa mkopo Middlesbrough kutoka Bournemouth msimu uliopita.  Travers ambaye mkataba wake unatarajiwa kumalizika mwaka 2027, msimu uliopita alicheza mechi 22 za michuano yote.


Dani Ceballos

REAL  Madrid inahitaji kiasi kisichopungua pauni 40 milioni kama ada ya uhamisho ya  kiungo wao wa kimataifa wa Hispania Dani Ceballos, 28, na Pauni 30 milioni kwa kiungo wao wa kimataifa wa Morocco,  Brahim Diaz, 25, ambao kocha wao mpya, Xabi Alonso anadaiwa kuwa hawapo katika mipango yake kuelekea msimu ujao.


Romaine Mundle

Sunderland iko karibu kumsainisha mkataba mpya winga wao raia wa England, Romaine Mundle, mwenye umri wa miaka 22, katika dirisha hili. Vigogo wa Sunderland wanafanya haraka kuhakikisha wanamsainisha mkataba mpya baada ya kuona  PSV Eindhoven inainyatia saini yake. Mkataba wake wa sasa unatarajiwa kumalizika mwaka 2028.