Antonio Rudiger azidi kuwachanganya Juventus
Muktasari:
- Juventus inaamini uzoefu wake utaongeza chachu katika harakati za kukijenga upya kikosi ambacho kwa misimu ya hivi karibuni kimekuwa hakifanyi vizuri katika michuano ya ndani na kimataifa.
JUVENTUS inaendelea kumfuatilia kwa karibu beki wa kati wa Real Madrid, Antonio Rudiger, 33. Inaelezwa vigogo hao wa Italia wamepata matumaini makubwa baada ya kuona mkataba wa Rudiger unamalizika mwisho wa msimu na hadi sasa hakuna mazungumzo yaliyoanza kati ya wawakilishi wake na Madrid.
Juventus inaamini uzoefu wake utaongeza chachu katika harakati za kukijenga upya kikosi ambacho kwa misimu ya hivi karibuni kimekuwa hakifanyi vizuri katika michuano ya ndani na kimataifa.
Hata hivyo, bado haijafahamika kama Real Madrid itafungua mazungumzo naye au itaachana naye mwisho wa msimu ingawa taarifa za ndani zinadai benchi la ufundi halitamani kuona staa huyo akiondoka.
Tangu kuanza kwa msimu huu Rudiger amecheza mechi 18 za michuano yote na kufunga bao moja. Msimu huu amekuwa akisumbuliwa na majeraha ya mara kwa mara yaliyosababisha asipate muda mwingi ucheza tofauti na ilivyozoelekea.
Ibrahim Mbaye
ASTON Villa ni miongoni mwa timu za Ligi Kuu England zinazofikiria kumsajili mshambuliaji chipukizi wa kimataifa wa Senegal, Ibrahim Mbaye mwenye umri wa miaka 18. Mbaye ambaye kwa sasa anacheza Paris Saint-Germain amevutia vigogo vingi Ulaya kutokana na kiwango bora alichoonyesha akiwa na PSG. Mkataba wake unamalizika 2028 na tangu kuanza kwa msimu huu amecheza mechi 26 za michuano yote na kufunga bao moja.
Sandro Tonali
INAELEZWA Manchester City na Manchester United zipo katika vita kali ya kutaka kumsajili kiungo wa Newcastle United, Sandro Tonali mwenye umri wa miaka 25. Hata hivyo, inaelezwa kuwa Tonali hana mpango wa kutaka kuendelea kusalia England ikiwa ataondoka Newcastle United badala yake anataka kurudi Italia. Timu kadhaa za Italia nazo tayari zimeshaanza kujizogeza kwa ajili ya kutaka kumsajili ingawa hataki kufanya uamuzi wowote hadi msimu utakapomalizika.

Santiago Castro
WEST Ham United na Nottingham Forest zitakutana na ushindani kutoka AC Milan katika mbio za kumsajili mshambuliaji wa Bologna na Argentina, Santiago Castro, 21. Castro ambaye ameendelea kuonyesha makali Serie A, amekuwa akitazamwa na maskauti wa klabu hizo tangu kuanza kwa msimu huu. Inaelezwa kuwa West Ham na Nottingham Forest zinataka kumsajili ili kuimarisha safu za ushambuliaji.
Antonee Robinson
MANCHESTER United imeongeza jina la beki wa kushoto wa Fulham, Antonee Robinson, 28, katika orodha ya wachezaji inaowataka katika dirisha lijalo la majira ya kiangazi. Robinson, ambaye ni mchezaji wa kimataifa wa Marekani, amevutia benchi la ufundi la Man United kutokana na uwezo wake wa kupandisha mashambulizi. Inaelezwa kuwa Man United inaangalia uwezekano wa kuongeza ubora safu ya ulinzi.
Lucas Bergvall
TOTTENHAM Hotspur imesisitiza kwamba haina mpango wa kumuuza kiungo wa kimataifa wa Sweden, Lucas Bergvall, 20, katika dirisha lijalo la majira ya kiangazi baada ya Aston Villa na Chelsea zilizowasilisha ofa Januari kuonyesha nia ya kurudi mezani mwisho wa msimu. Bergvall anaonekana kuwa sehemu muhimu ya mipango ya muda mrefu ya Spurs baada ya kuonyesha kiwango bora tangu ajiunge na klabu hiyo.
Randal Kolo Muani
MSHAMBULIAJI wa kimataifa wa Ufaransa, Randal Kolo Muani, 27, ameonyesha nia ya kujiunga na Juventus dirisha lijalo la kiangazi. Muani ambaye yupo kwa mkopo Tottenham Hotspur akitokea PSG amevutiwa zaidi na ofa ya kujiunga na Juventus ambayo imemhakikishia kumpa nafasi ya kutosha na kumfanya kuwa straika tegemeo. Mkataba na PSG unamalizika 2028.
Fermin Lopez
MANCHESTER United ipo tayari kutumia hadi Euro 100 milioni kumsajili kiungo mshambuliaji wa Barcelona, Fermin Lopez, 22, katika dirisha lijalo. Hata hivyo, inaelezwa kuwa Lopez hana nia ya kuondoka Camp Nou, jambo linaloweza kuwa kikwazo Man United kukamilisha dili hilo. Kiungo huyo ni mmoja kati ya mastaa tegemeo wa Barca. Tangu kuanza msimu huu amecheza mechi 39 na kufunga mara 12.