Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Nascimento afariki dunia usingizini

NASCIMENTO Pict

Muktasari:

  • Pambano la mwisho la mpiganaji huyo wa UFC lilikuwa Juni 20 katika UFC Fight Night 279 dhidi ya Mitch Raposo, ambaye alikatisha mfululizo wa ushindi wa Nascimento baada ya kushinda mara anne mfululizo dhidi ya Jake Hadley, Carlos Hernandez, Jafel Filho na Cody Durden, kwa mujibu wa ESPN.

SAO PAOLO, BRAZIL: BONDIA wa mchezo wa mapambano mchanganyiko (UFC), Allan Nascimento, amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 34 baada ya kudaiwa kupata mshtuko wa moyo akiwa amelala.

Taarifa hiyo imekuja wiki sita tu baada ya pambano lake la mwisho lililofanyika Las Vegas, Marekani, Juni 20, ambapo Nascimento alipoteza kwa uamuzi wa majaji uliogawanyika (split decision) dhidi ya Mitch Raposo katika mchezo wa UFC Vegas 119.

Taarifa ya UFC ilisema jana kuwa, “mpiganaji wetu mpendwa wa uzito wa flyweight, Allan Nascimento, alipatikana akiwa hajitambui baada ya kupata mshtuko wa moyo akiwa usingizini. Licha ya juhudi za timu ya madaktari waliofika eneo la tukio alitangazwa kuwa amefariki dunia papo hapo.” Taarifa hiyo ya UFC iliambatana na picha moja ya kumbukumbu ya Nascimento akiwa anacheka huku akiwa ameinua ngumi yake iliyovaa glovu ya UFC.

NASCI 01

Mzaliwa wa Sao Paulo, Brazil, Nascimento alijijengea jina kubwa baada ya kushinda mapambano 17 kati ya 22 ya mwanzo ya taaluma yake.

Akiwa mpiganaji wa uzito wa flyweight, Nascimento aliyekuwa akifahamika kwa jina la utani “Puro Osso”, msemo wa Kireno unaomaanisha “ngozi na mifupa” alipigana katika mashindano mbalimbali kabla ya kujiunga na UFC, yakiwemo RIZIN, Legacy FC na Dana White’s Contender Series.

Alijiunga rasmi na UFC 2021 na kushinda mapambano manne kati ya sita aliyocheza katika shirikisho hilo, na alimaliza maisha yake ya ushindani akiwa na rekodi ya ushindi 22 na kupoteza mapambano saba.

Nascimento pia aliwahi kushinda tuzo za Performance of the Night baada ya kuwavutia mashabiki kwa ushindi wa kuwachapa wapinzani wake kwa njia ya ‘submission’ dhidi ya Carlos Hernandez na Cody Durden.

Bingwa wa zamani wa UFC wa uzito mwepesi (lightweight), Charles Oliveira, ambaye alikuwa akifanya mazoezi pamoja na Nascimento huko Sao Paulo, alitoa ujumbe wake kupitia mitandao ya kijamii, ambapo aliandika kwa Kireno: “Leo nimepoteza kaka ambaye mchezo wa mapambano ulinipa. Asante kwa kuwa pamoja nami kila wakati, kwa kushiriki mikeka ya mazoezi na kona ya pambano.”

NASCI 02

“Sina chochote zaidi ya shukrani kwa kuwa ulikuwa nami kwenye mazoezi, kwenye kona (eneo la ushauri wakati mchezo ulingoni) na hata wakati wa mapumziko. Nakupenda rafiki yangu; wewe ni gwiji. Kaka yangu, siwezi hata kuamini. Utakumbukwa sana.”

Katika ujumbe alioweka juu ya ukurasa wake wa Instagram mwezi Juni, Nascimento alieleza historia fupi ya safari yake kuingia kwenye mchezo huo akisema alianza mazoezi ya Muay Thai 2007 akiwa “mtu mwembamba na mdogo sana”, hali iliyomfanya apewe jina la utani “Puro Osso”, linalomaanisha “mfupa mtupu”.

Alieleza kuwa awali wazazi wake hawakuunga mkono ndoto yake ya kuwa mpiganaji wa kulipwa, lakini baadaye walibadilika baada ya kuona juhudi na kujituma kwake kufikia malengo yake.

Nascimento pia alizungumzia kifo cha baba yake kilichotokea wiki tatu tu kabla ya pambano lake la kwanza la UFC, akisema ulikuwa, “wakati mgumu zaidi katika maisha yangu. Lakini yeye ni mtu ambaye yuko pamoja nami katika kila pambano. Yupo kila wakati kwenye picha ninayokuwa nayo.”

Pambano la mwisho la mpiganaji huyo wa UFC lilikuwa Juni 20 katika UFC Fight Night 279 dhidi ya Mitch Raposo, ambaye alikatisha mfululizo wa ushindi wa Nascimento baada ya kushinda mara anne mfululizo dhidi ya Jake Hadley, Carlos Hernandez, Jafel Filho na Cody Durden, kwa mujibu wa ESPN.