Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Alexander Isak aisikilizia Liverpool kabla ya kujua Muhtasari wake

Muktasari:

  • Isak ambaye kwa sasa hafanyi mazoezi na timu baada ya kutokea kwa sintofahamu juu ya dili lake la kujiunga ja Liverpool kwa  wiki mbili zilizopita alikuwa Hispania ambako alikuwa akifanya mazoezi katika viwanja vya timu yake ya zamani Real Sociedad.

MSHAMBULIAJI wa Newcastle na timu ya taifa ya Sweden, Alexander Isak, 25, amewaambia wawakilishi wake kuwa ataendelea  kucheza Newcastle na kusaini  mkataba mpya katika dirisha hili ikiwa tu Liverpool itamjulisha rasmi kuwa haiwezi kumsajili katika dirisha hili la majira ya kiangazi.

Isak ambaye kwa sasa hafanyi mazoezi na timu baada ya kutokea kwa sintofahamu juu ya dili lake la kujiunga ja Liverpool kwa  wiki mbili zilizopita alikuwa Hispania ambako alikuwa akifanya mazoezi katika viwanja vya timu yake ya zamani Real Sociedad.

Liverpool inahitaji sana huduma ya fund huyu lakini changamoto ni kitita cha Pauni 150 milioni ambacho Newcastle inakihitaji ili kumuuza inaonekana kuwa ni kikubwa sana kwao.

Ofa ya mwisho ya majogoo hao wa Jiji la Liverpool inaripotiwa kuwa ni Pauni 110 milioni ambayo ilikataliwa na wakaambiwa kwamba staa huyo hauzwi kwa sasa.

Suala hilo liliripitiwa kumkera sana Isak ambaye amesisitiza kwamba hataki kuendelea kubakia Newcastle.

Liverpool kwa sasa imetuma ujumbe kwenda Newcastle na kuiambia kwamba ikiwa haitobadilisha msimamo wao wa kutomuuza Isak, wao hawatoongeza ofa yoyote zaidi ya hapo.

Mkataba wa sasa wa fundi huyu unamalizika mwaka 2028 na kuna uwezekano mkubwa ikiwa Liverpool itaamua kuachana naye, anaweza akasaini mkataba mpya na kubakia katika timu hiyo inayomilikiwa na matajiri wa Saudi Arabia.

Msimu uliopita alifunga mabao 20 ya Ligi Kuu England.


Rodrygo

MANCHESTER City huenda ikalazimika kutoa Pauni 87 milioni  ili kuipata saini ya  mshambuliaji wa Real Madrid na timu ya taifa ya Brazil, Rodrygo  mwenye umri wa miaka 24, katika dirisha hili lamajira ya kiangazi.

Rodrygo ambaye msimu uliopita alifunga mabao 17 na kutoa asisti nane katika michuano yote alikuwa akitajwa sana kuondoka Madrid katika dirisha hili kwa sababu haoni nafasi ya kucheza katika kikosi hicho kwa msimu ujao lakini sasa anadaiwa kubadilisha mawazo ingawa Madrid itakuwa tayari kumwachia ikiwa yeye mwenyewe ataonyesha nia hiyo.


James McAtee

KLABU ya Nottingham Forest ipo karibu kufikia makubaliano ya kumsajili kiungo raia wa England, James McAtee mwenye umri wa miaka 22 kutoka Manchester City.

 McAtee alitolewa kwa mkopo Sheffield United msimu uliopita ambapo alicheza mechi 33 za Ligi Daraja la kwanza.

Staa huyu ameripotiwa kuwasilisha maombi ya kutaka kuondoka kwa ajili ya kutua timu itakayompa nafasi kubwa zaidi ya kucheza tofauti.

Piero Hincapie

CHELSEA inafikiria kumsajili beki kisiki wa Bayerl Leverkusen na timu ya taifa ya  Ecuador Piero Hincapie, 23, katika dirisha hili.

Vigogo wa Chelsea wanataka kutua kwa beki huyu baada ya kuvutiwa na kiwango bora alichoonyesha msimu uliopita.

Leverkusen haionekani kuwa tayari kumuuza Piero kwa sasa ingawa inaweza kufikiria kufanya hivyo ikiwa itapokea ofa nono inayoweza kuanzia Pauni 50 milioni kiasi ambacho Chelsea haionekani kuwa tayari kutoa kwa sasa.


Kieran Trippier

AS Monaco imeonyesha nia ya kumsajili beki wa kulia wa Newcastle na timu ya  taifa ya England, Kieran Trippier, mwenye umri wa miaka 34.

 Trippier ambaye ana uzoefu mkubwa ameivutia sana Monaco ambayo inaamini ataongeza nguvu kwenye kikosi chao kuelekea michuano ya kimataifa msimu ujao.

Katika dirisha hili, Monaco tayari imefanikisha usajili wa mchezaji mwingine mwenye jina kubwa Paul Pogba.


Ibrahim Konate

CHELSEA imewasilisha ofa ya Pauni 43 milioni kwenda Liverpool kwa ajili ya kumnunua beki wa kati wa klabu hiyo na timu ya taifa ya Ufaransa, Ibrahima Konate, mwenye umri wa miaka 26. Konate amekuwa sehemu ya kikosi cha Liverpool tangu 2021.

Mkataba wa sasa wa staa huyu anatarajiwa kumalizika mwakani na anadaiwa kukataa kusaini mkataba mpya na hadi sasa ripoti zinaeleza Liverpool ipo tayari kumuuza ili kuepuka kumpoteza kwa pesa ndogo ifikapo Januari mwakani au kuondoka bure mwisho wa msimu ujao.


Rasmus Hojlund

INTER Milan, Roma, Juventus, AC Milan na Napoli zipo katika vita kali ya kuiwania saini ya mshambuliaji wa Manchester United na timu ya taifa ya Denmark, Rasmus Hojlund, 22, katika dirish hili. Manchester United ipo tayari kumuuza staa huyu lakini inahitaji ofa inayoanzia Pauni 30 hadi 40 milioni. Katika msimu uliopita alifunga mabao 12 ya Ligi Kuu England.

Nafasi ya staa huyu katika kikosi cha Man United inaonekana kuwa finyu baada ya klabu hiyo kusajili washambuliaji watatu katika dirisha hili.


Mateus Fernandes

WEST Ham inajiandaa kuwasilisha ofa ya kumsajili kiungo wa Southampton na timu ya taifa ya  Ureno kwa vijana wenye umri chini ya miaka 21, Mateus Fernandes, 21, katika dirisha hili.

Mabosi wa West Ham wanadaiwa kutaka kutoa Pauni 30 milioni kama ada ya uhamisho ya fundi huyu kiasi ambacho Soton imeonyesha kuwa tayari kukikubali.

Mateus alionyesha kiwango bora sana katika ligi ya Championship England msimu uliopita.