Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

AFCON 2025: 16 Bora ramani nzima ipo hivi

RAMANI Pict

Muktasari:

  • Zambia, Comoros, Zimbabwe, Angola, Uganda, Botswana, Gabon na Guinea ya Ikweta zilishindwa kushikilia bomba na kuaga mapema michuano hiyo ya 35 tangu ilipoasisiwa 1957, lakini Botswana, Guinea ya Ikweta na Gabon zimeaga kwa aibu zaidi kwani hazikuambulia hata pointi moja kutokana na kupoteza mechi zote tatu za makundi yao.

BAADA siku 11 ya kushuhudiwa zikipigwa mechi 32 za makundi, hatimaye timu za nchi 16 kati ya 24 zilizoshiriki michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) 2025 zimetoboa kibabe kwenda hatua ya 16 Bora inayoanza wikiendi hii na kumalizikia Jumanne ijayo.

Zambia, Comoros, Zimbabwe, Angola, Uganda, Botswana, Gabon na Guinea ya Ikweta zilishindwa kushikilia bomba na kuaga mapema michuano hiyo ya 35 tangu ilipoasisiwa 1957, lakini Botswana, Guinea ya Ikweta na Gabon zimeaga kwa aibu zaidi kwani hazikuambulia hata pointi moja kutokana na kupoteza mechi zote tatu za makundi yao.

Timu 16 zilizopenya salama kuingia hatua inayoafuata ni wenyeji Morocco waliongoza Kundi A wakiwa mbele ya Mali, wakati Kundi B limetoa timu za Misri, Afrika Kusini, wakati Nigeria iliiyoongoza Kundi C mbele ya Tunisia na Tanzania zote zimefuzu hata hiyo. Tanzania imepenya katika kapu la washindwa bora, lenye timu nyingine za Benin, Msumbiji na Sudan.

RAMA 04

Kundi D limetoa timu za Senegal na DR Congo, wakati Algeria na Burkina Faso zimepenya kupitia Kundi E na watetezi Ivory Coast na Cameroon wenyewe wamefuzu kupitia Kundi F kutokana na kumaliza wakilingana kila moja ikiwa na pointi saba na wastani wa mabao +2, watetezi wakiwa na mabaio matano na kufungwa matatu, ilihali wapinzani wao wakifunga manne na kufungwa mawili.

Hatua ya mtoano ya 16 Bora imepangwa kuanza kesho na kuendelea hadi Jumanne ili kusaka timu nane za kwenda robo fainali na ratiba nzima ipo kama ilivyoainishwa hapo chini.

RAMA 03

KESHO JUMAMOSI

Kipenga cha 16 Bora kinatarajiwa kufunguliwa kesho Jumamosi kuanzia saa 1:00 usiku kwa Senegal kuvana na Sudan katika mechi itakayopigwa kwenye Uwanja wa Tangier Grand maarufu kama Ibn Batouta kabla ya saa 4:00 usiku kuwa zamu ya Mali na Tunisia kupepetana kwenye Uwanja wa Mohammed V uliopo jijini Casablanca.

Pambano la Senegal na Sudan litakuwa ni la nane kwa nchi hizo kukutana tangu mwaka 2012 katika michuano mbalimbali, huku Senegal ikibebwa na rekodi ya kushinda mara tano, ilihali Sudan ikiwa haijawahi kuonja ushindi zaidi ya kuambulia sare katika mechi mbili zilizosalia zikiwamo za makundi ya kuwania fainali hizi za AFCON 2025 na zile za Kombe la Dunia mbali na mechi moja ya kirafiki ya kimataifa ambapo Senegal ilishinda kwa bao 1-0.

Haitakuwa mechi nyepesi kwa timu zote, lakini bado mabingwa hao wa 2021 wakipewa nafasi kubwa kuvuka hapo.

Kwa mechi ya Mali na Tunisia, litakuwa ni ya 11 baina ya timu hizo katika michuano mbalimbali tangu mwaka 1994, huku Mali ikiongoza kwa kushinda mara nne dhidi ya tatu za Tunisia, huku mechi nyingine tatu zikiisha kwa sare tofauti, zikiwa mechi mbili za mwisho kukutana katika michuano ya kuwania fainali za Afcon na Kombe la Dunia.

Ni mechi ngumu kutabiri kutokana na timu zote kutoonyesha makali katika fainali za msimu huu, lakini kwa vile ni mechi ya mtoano, timu itakayojipanga vyema ndio itakayotoboa, ingawa Mali inapigiwa chapuo zaidi hadi sasa.

RAMA 02

KAZI YA JUMAPILI

Hii ndio siku inayosubiriwa na hamu kubwa na Watanzania walio wengi kwani timu ya taifa, Taifa Stars mapema tu saa 1:00 usiku itakuwa uwanjani kukabiliana na wenyeji Morocco, kabla ya Afrika Kusini kuumana na Cameroon saa 4:00 usiku.

Mechi zote zikitarajiwa kupigwa katika jiji moja la Rabat, Stars na wenyeji wakiumana kwenye Uwanja wa Prince Moulay Abdellah, ilihali Wasauzi na Cameroon watavaana kwenye Uwanja wa Al Medina.

Hilo litakuwa ni pambano la tisa kwa Tanzania kuumana na Morocco tangu mwaka 2010 kupitia mechi za michuano mbalimbali huku rekodi zikiwabeba wenyeji, kwani katika mechi nane za awali imeshinda saba, huku ni mara moja tu kwa Stars kutoka na ushindi mbele ya wapinzani wao hao.

Katika hatua ya makundi ya AFCON 2023, Tanzania ilikandikwa mabao 3-0, lakini pie zimekutana katika mechi za kuwania kufuzu ushiriki wa fainali za Kombe la Dunia 2026 zitakazofanyika Marekani, Canada na Mexico na mara zote Stars imepasuka nje ndani kwa mabao 2-0 na katika robo fainali ya michuano ya CHAN 2024 ililala pia kwa bao 1-0.

Kwa kuangalia namna rekodi zilivyo na aina ya vikosi vilivyopo katika fainali hizo za AFCON 2025, ni wazi turufu inawaangukia wenyeji, ingawa soka huwa na matokeo ya kikatili na ndicho wanachotegemea Watanzania kwa Stars.

Ni pambano la sita kwa timu za Afrika Kusini na Cameroon tangu mwaka 1996, kwani awali zilishakutana mara tano ikiwamo mechi mbili za kirafiki na tatu za michuano ya Afrika ambapo Wasauzi wameshinda mara mbili huku nyingine zikiisha kwa sare zikiwamo za mwisho za makundi ya kuwania fainali za AFCON 2018.

Hii ni kuonyesha pambano hilo la 16 Bora halitabiriki kirahisi, kwani kila timu ina nafasi japo Cameroon ya msimu huu inaonekana kuwa imara zaidi kulinganisha na Afrika Kusini.

RAMA 01

BALAA LA JUMATATU

Jumatatu nako kuna balaa jingine katika hatua ya 16 Bora kwani zitapigwa mechi mbili kama itakavyokuwa wikiendi.

Mabingwa wa kihistoria wa michuano hiyo, Misri watashuka kwenye Uwanja wa Adrar, uliopo Agadir saa 1:00 usiku kupepetana na Benin kabla ya Nigeria haijashuka kwenye Uwanja wa Fez, mjini Fez kuumana na Msumbiji kuanzia saa 4:00 usiku.

Benin iliyotinga hatua hiyo kama mmoja ya timu nne zilipenya kwa kapu la washindwa bora baada ya kuandikisha ushindi wake wa kwanza wa michuano hiyo dhidi ya Botswana inavaana na Misri ikiwa ni mara ya tano kwao kukutana tangu 2024.

Haijawahi kuonja ushindi katika mechi nne zilizopita dhidi ya Mafarao hao.

Mara ya mwisho kukutana ilkuwa katika mechi ya makundi ya AFCON 2010 ilipolala kwa mabao 2-0, huku mechi moja pekee iliyokuwa ya kuwania kufuzu ushiriki wa fainali za Kombe la Dunia 2006 ilipojitutumua na kutoka sare ya 3-3 kabla ya kupasuliwa 4-1 ziliporudiana. Kiufupi, turufu inawabeba Misri yenye nyota Mohammed Salah.

Kwa mechi ya Nigeria na Msumbiji itakuwa ni ya sita kwa timu hizo kwani zimeshakutana mara tano, ikiwamo moja ya kirafiki, mbili za kuwania kufuzu ushiriki wa fainali za Kombe la Dunia na zile za michuano ya CHAN na AFCON, huku ni mara moja tu Msumbiji alikomaa na kupata sare, huku mechi nyingine nne ikipasuka ikiwamo ile ya kirafiki.

Msumbiji imepenya hatua hiyo kama ilivyo kwa Benin, Tanzania na Sudan na itakuwa na kibarua kigumu cha kukabiliana na nyota wa Nigeria ambao safari hii wameonekana wamepania kuondoka na taji hilo wanalolisaka tangu walipotwaa mara ya mwisho mwaka 2013 na kulikosa katika fainali zilizopita kwa kuzidiwa na wenyeji Ivory Coast.


FUNGA KAZI

Mechi za kuhitimisha hatua ya 16 Bora zitakuwa Jumanne ambako nako kutapigwa mechi mbili za kukata na shoka. Mabingwa wa 2019 Algeria watakuwa na kibarua dhidi ya DR Congo ya Fiston Mayele mapema saa 1:00 usiku kwenye Uwanja wa Moulay Hassan, mjini Rabat kabla ya saa 4:00 usiku kwenye Uwanja wa Marrakech wakati watetezi Ivory Coast watakapomalizana na majirani zao wa Burkina Faso ya Stephanie Aziz Ki.

Hizi ni mechi zinazotajwa kama ngumu zaidi katika hatua hiyo kutokana na vikosi na upinzani wa timu zinazovaana kwani kwa pambano la Algeria ya Riyad Mahrez na DR Congo litakuwa ni la sita kwa timu hizo tangu 1988, kwani zimeshakutana mara mbili katika hatua tofauti za fainali za AFCON na nyingine tatu za kirafiki.

Katika mechi hizo tano za awali ni mara mbili tu ndio zimetoa mshindi zote zikiwa ni Algeria ikiwamo ya kirafiki iliyopigwa Juni 9, 2022 na wababe hao kushinda kwa mabao 3-0, lakini ilishinda pia mechi ya makundi ya AFCON 1988 kwa bao 1-0 kuonyesha kuwa ni mechi ngumu kutabirika na itakayojipanga itapenya kwenda robo fainali.

Pambano la majirani Ivory Coast na Burkina Faso litakuwa ni la 14 baada ya awali kukutana mara 13 katika michuano mbalimbali, huku rekodi zikiwabeba watetezi ambao wameshinda mara nane, huku wapinzani wakitakata mara mbili na mechi nyingine tatu zikiisha kwa sare.

Mara mbili za mwisho zilipokutana ilikuwa ni katika mechi za kuwania kufuzu ushiriki wa Fainali za CHAN 2024 ambapo kila moja ilishinda nyumbani kwa mabao 2-0 na kuamuliwa kwa penalti ambazo ziliibeba Burkina Faso, lakini kwa rekodi zilivyo ni wazi kina Aziz KI watakuwa na kazi kubwa kukabiliana na watetezi hao Tembo wa Ivory Coast.