Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

AC Milan yaangukia kwa Hojlund, mchongo mzima upo hivi

FUNUNU Pict

Muktasari:

  • AC Milan inaamini kwamba dili hilo la mkopo litaipa nafasi ya kumtumia kijana huyo mwenye kipaji kikubwa na ikiwa itaridhishwa na kiwango chake itamchukua moja kwa moja.

AC Milan imeonyesha nia kubwa ya kumsajili mshambuliaji wa Manchester United na timu ya taifa ya Denmark, Rasmus Hojlund kwa mkopo wa msimu mmoja ambao utakuwa na kipengele cha kumnunua moja kwa moja mwishoni mwa msimu ujao.

AC Milan inaamini kwamba dili hilo la mkopo litaipa nafasi ya kumtumia kijana huyo mwenye kipaji kikubwa na ikiwa itaridhishwa na kiwango chake itamchukua moja kwa moja.

Hata hivyo, Manchester United haijafurahishwa na pendekezo hilo kwani inataka kumuuza moja kwa moja kwa dau la takribani Pauni 73 milioni.

Rasmus ambaye alijiunga na Masheta Wekundu wa Pld Trafford akitokea Atalanta mwaka 2023 kwa ada ya takribani Pauni 64 milioni amewekwa sokoni na waajiri wake baada ya Benjamin Sesko kukubali kujiunga nao akitokea RB Leipzig ya Ujerumani jambo linalomuweka katika changamoto kubwa ya kupata nafasi hata kama akibaki katika timu hiyo.

Hojlund ambaye pia amechezea timu ya taifa ya Denmark mechi 21 na kufunga mabao tisa, anahitajika pia na wababe wa Italia, Napoli.

Ikiwa AC Milan itashindwa kumpata staa huyu, inafikiria kuhamia kwa  Joshua Zirkzee au Gianluca Scamacca.

Mkataba wa Rasmus Hojlund na Manchester United unatarajiwa kumalizika ifikapo Juni 2028, lakini kuna kipengele cha kuongeza mwaka mmoja hadi 2029 iwapo klabu hiyo itaamua kufanya hivyo.

Manchester United inapambana kuweka mambo yake sawa katika dirisha hili la usajili huko Ulaya ikiwa tayari imeshawaweka kando nyota wake kadhaa kwa ajili ya kuwauza, huku kundi kubwa la wachezaji wanaotokea katika timu B wakiondoka kwa mkopo.


Alexander Isak

MSHAMBULIAJI wa Newcastle United na timu ya taifa ya Sweden, Alexander Isak hatacheza katika mechi za maandalizi dhidi ya Espanyol na Atletico Madrid wikiendi hii kutokana na sintofahamu kuhusu hatma yake. Liverpool inatajwa kuwa na nia ya kumsajili straika huyo aliyefunga mabao 25 msimu uliopita katika mashindano yote, lakini changamoto ni ada ya uhamisho. Isak amewaambia mabosi Newcastle kuwa anahitaji kuondoka na kutua Liverpool.


Nico Paz

COMO ya Italia imekataa ofa ya Pauni 30 milioni kutoka Tottenham Hotspur inayoitaka saini ya mchezaji wa kimataifa wa Argentina, Nico Paz, mwenye umri wa miaka 20. Inadaiwa kwamba Como inahitaji kiasi kisichopungua Pauni 52 milioni ili kumuuza Paz ambaye ilimsajili kutoka timu ya vijana ya  Real Madrid. Mkataba wake wa sasa unatarajiwa kumalizika ifikapo 2028 na kwa sasa ni miongoni mwa wachezaji wa kikosi cha kwanza.


John McGinn

ASTON Villa imekataa ofa ya Pauni 18 milioni kutoka Everton iliyoiwasilisha dirisha hili kwa ajili ya kiungo wa kimataifa wa Scotland, John McGinn, 30. Mbali ya Everton, Newcastle pia inatajwa kumtaka staa huyo ambaye ni miongoni mwa wachezaji tegemeo katika kikosi cha Unai Emery. McGinn ambaye amecheza Villa tangu 2018, mkataba wake unamalizika 2027.


Yoane Wissa

MATAJIRI wa Saudi Arabia, Al-Nassr wako tayari kutimiza madai ya Brentford kwa mshambuliaji wa DR Congo, Yoane Wissa, 28. Wissa, aliyefunga mabao 12 msimu uliopita pia anahusishwa na Newcastle na Tottenham. Mkataba wake wa sasa unatarajiwa kumalizika mwakani na inaelezwa mabosi wa Brentford wanataka kumuuza kwa Pauni 30 milioni ili asiondoka bure mwisho wa msimu.


Inigo Martinez

BEKI kisiki wa Hispania, Inigo Martinez, 34, anaripotiwa kuwa katika hatua za mwisho za kuvunja mkataba  Barcelona ili ajiunge na Al-Nassr kwa uhamisho wa bure. Martinez ambaye alijiunga na Barca akitokea Athletic Bilbao mwaka jana si mmoja kati ya mastaa tegemeo wa wababe hao wa Hispania ambao wapo tayari kumwacha. Mkataba wake wa sasa unatarajiwa kumalizika Juni, mwakani. Kwa sasa yupo Barca kwa maandalizi ya msimu ujao.


Claudio Echeverri

MANCHESTER City imekataa ofa ya AS Roma kwa kiungo chipukizi wa Argentina, Claudio Echeverri, 19. Inaelezwa Man City inataka kumpeleka kwa mkopo Girona ambayo pia inamilikiwa na mmiliki wao. Echeverri ni mmoja wa wachezaji waliowika kwenye Kombe la Dunia la U17 mwaka 2023 lakini amekuwa hapati nafasi ya kutosha kikosi cha kwanza Barca.


Alfie Devine

KIUNGO mshambuliaji wa Tottenham Hotspur, Alfie Devine, 21, yuko mbioni kujiunga na Preston North End kwa mkopo. Devine ambaye ametokea akademi ya Spurs anatolewa kwa mkopo ili akapate nafasi kubwa ya kucheza tofauti na ilivyo akisalia Spurs. Amewahi kuchezea timu ya taifa ya vijana ya England. Mkataba wake unaisha Juni 2027.