Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Bellingham, Vozinha wastua Kikosi cha Dunia

KIKOSI Pict

Muktasari:

  • England ilimaliza katika nafasi ya tatu baada ya kuifunga Ufaransa kwenye mchezo wa kusaka mshindi wa medali ya shaba, ikiwa ni mafanikio yao makubwa zaidi katika Kombe la Dunia tangu mwaka 1966.

LONDON, ENGLAND: KIUNGO wa Real Madrid, Jude Bellingham, ndiye mchezaji pekee wa England aliyejumuishwa katika Kikosi Bora cha Kombe la Dunia 2026, kilichotangazwa na FIFA baada ya kumalizika kwa mashindano hayo.

England ilimaliza katika nafasi ya tatu baada ya kuifunga Ufaransa kwenye mchezo wa kusaka mshindi wa medali ya shaba, ikiwa ni mafanikio yao makubwa zaidi katika Kombe la Dunia tangu mwaka 1966.

Bellingham mwenye umri wa miaka 23 aliweka rekodi mpya kwa kufunga mabao saba na kuwa mfungaji bora wa England katika Kombe la Dunia moja.

KIKO 01

NYOTA WA LIGI KUU ENGLAND WATAWALA

Bellingham ameungana na nyota wengine wanaocheza au waliocheza Ligi Kuu England akiwemo beki wa kulia wa Tottenham, Pedro Porro, pamoja na kiungo wa Manchester City, Rodri, ambaye alikuwa nguzo muhimu katika safari ya Hispania kutwaa ubingwa.

Beki wa Manchester United, Lisandro Martinez, na mshambuliaji wa Manchester City, Erling Haaland, pia wamejumuishwa baada ya kung'ara wakiwa na Argentina na Norway.

Beki wa kushoto, Marc Cucurella, aliyekamilisha uhamisho wa pauni51.8 milioni kwenda Real Madrid mwezi uliopita, ametajwa kuwa beki bora wa kushoto wa mashindano hayo.

Wachezaji wa Bayern Munich, Dayot Upamecano na Michael Olise, pia wamepata nafasi katika kikosi hicho.

Safu ya ushambuliaji imekamilishwa na nyota wa Ufaransa, Kylian Mbappe, aliyeshinda Kiatu cha Dhahabu, pamoja na Lionel Messi, aliyeiongoza Argentina hadi fainali ya mashindano hayo.

KIKO 02

VOZINHA AMSHINDA UNAI SIMON

Moja ya uamuzi uliouza mjadala mkubwa ni kutokuwepo kwa kipa wa Hispania, Unai Simon, licha ya kuwa sehemu muhimu ya mafanikio ya La Roja.

Simon aliweka rekodi ya kutoruhusu bao katika fainali na alifungwa bao moja pekee katika safari yote ya Hispania kuelekea ubingwa.

Badala yake, nafasi ya kipa ilichukuliwa na Vozinha, ambaye aliingia kwenye mashindano akiwa hana klabu na kuisaidia Cape Verde kufika hatua ya 32 bora, jambo lililomfanya kuwa mmoja wa wachezaji waliovutia zaidi katika Kombe la Dunia.