Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mkenya awindwa Kagera Sugar

MKENYA

Muktasari:

  • Nyota huyo anayemudu kucheza pia nafasi ya beki wa kati kwa ufasaha, amefikia makubaliano ya awali kwa ajili ya kujiunga na kikosi hicho cha ‘Wanankurukumbi’ na sasa zimebakia hatua chache kabla ya dili hilo la nyota huyo kukamilika rasmi.

BAADA ya Kagera Sugar kukata tiketi ya kucheza Ligi Kuu Bara kwa msimu wa 2026-2027, mabosi wa timu hiyo wanasuka upya kikosi hicho na sasa imefungua mazungumzo na beki wa kushoto wa Kakamega Homeboyz ya Kenya, Mkenya Boniface Onyango.

Nyota huyo anayemudu kucheza pia nafasi ya beki wa kati kwa ufasaha, amefikia makubaliano ya awali kwa ajili ya kujiunga na kikosi hicho cha ‘Wanankurukumbi’ na sasa zimebakia hatua chache kabla ya dili hilo la nyota huyo kukamilika rasmi.

Beki huyo aliyewahi kucheza timu za Ulinzi Stars, Kariobangi Sharks FC, Tusker FC, Gor Mahia na sasa Kakamega Homeboyz, ni miongoni mwa nyota wenye uwezo mkubwa jambo lililowavutia mabosi wa Kagera kuitaka saini yake kwa msimu wa 2026-2027.

Akizungumza na Mwanaspoti, Meneja wa Kagera Sugar, Bernard Samson Sikira amesema suala la usajili limeanza kufanyika kwa sasa ila, bado hakuna makubaliano rasmi yaliyofikiwa na mchezaji yeyote, ili kujiunga na kikosi hicho cha Kagera Sugar.

“Tunatarajia kuingia kambini wiki ijayo na hapo ndipo nitakapokuwa na nafasi nzuri ya kuzungumzia kuhusu suala lolote la usajili wetu, kwa sasa ni mapema kwani hakuna makubaliano yaliyofikiwa licha ya mchakato huo kuuanza,” amesema Sikira.

Hata hivyo, Mwanaspoti linatambua mchezaji huyo amefikia makubaliano ya kujiunga na kikosi hicho kilichorejea Ligi Kuu Bara kwa msimu wa 2025-2026, kikiungana na Geita Gold iliyokuwa mabingwa wa Championship na maafande wa Polisi Tanzania.