Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Straika Mkenya kutua Kagera Sugar

MKENYA Pict

Muktasari:

  • Nyota huyo alionyesha kiwango kizuri akiwa na Fortune Sacco FC na msimu wa 2025-2026 alimaliza kinara wa ufungaji baada ya kufunga mabao 25 kwenye michuano ya National Super League (Championship), jambo lililoivutia Kagera Sugar kumhitaji.

WIKI mbili zilizopita Mwanaspoti liliripoti kuhusu uongozi wa Kagera Sugar kumfuatilia mshambuliaji wa Fortune Sacco FC, Mkenya Collins Maina baada ya kuridhishwa na kiwango chake, ambapo kwa sasa dili hilo liko hatua za mwisho kukamilika.

Nyota huyo alionyesha kiwango kizuri akiwa na Fortune Sacco FC na msimu wa 2025-2026 alimaliza kinara wa ufungaji baada ya kufunga mabao 25 kwenye michuano ya National Super League (Championship), jambo lililoivutia Kagera Sugar kumhitaji.

Baada ya Mwanaspoti kuripoti wiki mbili zilizopita kuhusu dili hilo, taarifa mpya ni mchezaji huyo anakuja Tanzania kesho Jumatatu kwa ajili ya majadiliano hayo na Kagera Sugar na ikiwa watafikia makubaliano atasaini mkataba.

“Ni kweli anakuja Tanzania kwa ajili ya mazungumzo hayo na endapo tutafikia makubaliano atasaini mkataba wa miaka miwili wa kuichezea Kagera Sugar, tunaamini kila kitu kitaenda vizuri na hakuna kitakachoshindikana,” kilisema chanzo hicho.

Akizungumza na Mwanaspoti, Meneja wa Kagera Sugar, Bernard Samson Sikira amesema suala la usajili limeanza kufanyika kwa sasa ila, bado hakuna makubaliano rasmi yaliyofikiwa na mchezaji yeyote, ili kujiunga na kikosi hicho cha Kagera Sugar.

“Tunatarajia kuingia kambini wiki ijayo na hapo ndipo nitakapokuwa na nafasi nzuri ya kuzungumzia kuhusu suala lolote la usajili wetu, kwa sasa ni mapema kwani hakuna makubaliano yaliyofikiwa licha ya mchakato huo kuuanza,” amesema Sikira.