Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Aziz KI afichua mchongo wa mabilioni Yanga

AZIZ Pict


YANGA iko uwanjani kesho nchini Botswana, itakapokutana na wenyeji wa jiji la Gaborone, Gaborone United. Sasa staa wao mmoja amefichua malengo ambayo timu hiyo imejiwekea msimu huu katika Ligi ya Mabingwa Afrika.


Aliyefichua hayo ni kiungo mshambuliaji, Stephanie Aziz KI, ambaye ameliambia Mwanaspoti kuwa alipokutana na mabosi wa juu wa klabu hiyo, walimuweka wazi kwamba msimu huu shabaha yao ya kwanza ni kuhakikisha wanafika hatua ya robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika.


Aziz KI amesema mabosi wa klabu hiyo walimfafanulia kuwa usajili mkubwa walioufanya msimu huu umetokana na malengo hayo, ambapo nguvu kubwa itawekwa katika kufikia hatua hiyo au kwenda mbali zaidi.

Kauli hiyo ya Aziz KI inakuja wakati Yanga, msimu uliopita iliposhiriki Ligi ya Mabingwa Afrika, ilipoishia hatua ya makundi baada ya kukosa kidogo kufuzu robo fainali, huku AS FAR Rabat ya Morocco na Al Ahly ya Misri zikifuzu na baadaye kukutana katika fainali.

Yanga katika kundi lake ilikutana na vigogo waliowahi kubeba ubingwa huo, lakini ilifmaliza katika nafasi ya tatu, huku ikizipiku baadhi ya klabu za Afrika Kaskazini na kuiacha JS Kabylie ya Algeria ikimaliza mkiani mwa kundi hilo.

“Wakati nilipokutana na viongozi wa juu wa klabu katika mazungumzo ya kurejea hapa, waliniambia mradi huu walionao, msimu huu ambao tunauanza Jumamosi (kesho), malengo yao makubwa yapo kwenye Ligi ya Mabingwa,” amesema Aziz KI, ambaye amerejea Yanga kwa kipindi cha pili.

“Wanataka kuona tunafanya makubwa kwenye mashindano haya. Wanataka kuona timu, angalau kwa kiwango cha chini, inafika robo fainali. Waliniambia hata usajili huu mkubwa ambao wameufanya na uamuzi wa kulipa fedha nyingi kununua mkataba wangu ni kwa ajili ya kufanikisha hilo.”

AZI 06

Aidha, Aziz KI ameongeza kuwa mabosi wa Yanga, na hata yeye mwenyewe, hawana wasiwasi na mashindano ya ndani kutokana na ubora wa kikosi chao. Amesema sasa kazi kubwa itakuwa kutafuta matokeo bora katika mashindano hayo makubwa barani Afrika.

“Unaweza kuona tumeanza ligi kwa kasi kubwa, tumeshinda mechi zote tano za kwanza na tumekuwa tukicheza vizuri. Hata hivyo, mechi hizi za ligi ya ndani tunazitumia kujiweka sawa kwa ajili ya mashindano haya ya Afrika. Tukifanya vizuri katika Ligi ya Mabingwa, itakuwa rahisi kwetu kushinda mechi yoyote ndani ya Tanzania.

“Hizi mechi za ligi ya ndani hatutazidharau. Tutazitumia kujiweka sawa na kupandisha ubora wetu kiushindani, kwa sababu ukipoteza mechi za ndani, utakwenda kimataifa kucheza kwa presha. Tuna kikosi ambacho, tukifikia ubora ambao makocha wanautaka, tunaweza kushinda kokote.”