Mkude: Simba SC tunapambana kutetea ubingwa Ligi Kuu Tanzania Bara

Muktasari:

Simba inaongoza Ligi Kuu Tanzania Bara ikiwa na pointi 44 baada ya kucheza mechi 17.

Dar es Salaam.Kiungo wa Simba, Jonas Mkude amesema ushindani uliopo katika Ligi Kuu Tanzania Bara, anaamini utawafanya wacheze kwa kiwango cha juu kuhakikisha wanatetea ubingwa msimu huu.

Licha ya kukiri si kazi rahisi kufikia lengo lao, wanachokifanya nikujituma kwa bidii ili kuvuna matunda mwisho wa msimu.

"Kiukweli ligi ni ngumu inahitaji kukaza msuri ili kuishi malengo yetu mwisho wa msimu, kila timu inapambana kadri inavyoweza ili kutimiza kile wanachojipangia,"

Ameongeza kuwa "Jambo la kushuru nikupata pointi tatu kwa mechi ambazo tumezicheza pia kucheza kama fainali kwa michezo iliopo mbele yetu,"amesema.

Mbali na hilo amesisitiza kwamba wataheshimu kila timu watakayokutana nayo ili kuweza kuvuna pointi "Nidhamu ya mchezo ni kila kitu kwa mafanikio yetu, tunapigania kutwaa ubingwa mara tatu mfululizo,"amesema.