Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mastaa wawili wapya Simba waitaka dabi


NYOTA wapya wa Simba, Keletso Makgalwa na Ibrahim Doumbia wameonyesha kiu ya kuingia kwenye vita ya Dabi ya Kariakoo baada ya kueleza uzoefu wao wa mechi zenye presha kubwa katika mataifa waliyotoka huku wakiahidi kuleta uzoefu huo Msimbazi.


Makgalwa, raia wa Afrika Kusini ametua Msimbazi akiwa na historia ya kupitia klabu kadhaa za nchi hiyo, ikiwamo Mamelodi Sundowns, Maritzburg United, Moroka Swallows, TS Galaxy, All Stars, Upington City na Sekhukhune United, jambo linalompa uzoefu wa mazingira ya ushindani.

Kiwango chake bora zaidi kilionekana akiwa Upington City msimu wa 2023/24, alipofunga mabao 11 na kutoa asisti saba, akifikisha mchango wa jumla ya mabao 18, kabla ya kuhamia Sekhukhune United ambako msimu wa 2024/25 aling’ara zaidi kwenye kutengeneza mabao, akitoa asisti 11 katika mechi 28 za Ligi Kuu ya Afrika Kusini na kumaliza akiwa mmoja wa vinara wa pasi za mwisho kwenye ligi hiyo.

Lakini zaidi ya takwimu hizo, Makgalwa anaamini uzoefu wake wa kucheza mechi zenye presha Afrika Kusini utakuwa msaada kwake endapo atapata nafasi katika mchezo wa leo, Jumatano kwenye Dabi ya Kariakoo kwa ajili ya ufunguzi wa msimu ujao wa mashindano wa 2026/27.

“Itakuwa mechi yenye presha na uzito mkubwa kama zilivyo dabi nyingine, lakini tayari nimewahi kukutana na mechi za namna hiyo Afrika Kusini. Najua namna ya kucheza katika mazingira yenye presha na hiyo itanisaidia kukabiliana na Dabi,” alisema Makgalwa.

Kwa upande wa Doumbia, ambaye msimu uliopita aliibuka mfungaji bora wa Ligi Kuu ya Mali baada ya kufunga mabao 17 na kutoa pasi tano za mabao katika mechi 24, anafika Simba akiwa na rekodi inayompa sababu ya kujiamini.

Katika mashindano yote msimu uliopita, Doumbia alifunga mabao 21 akiwa AS Korofina, kiwango kilichomfanya Simba kuvutiwa na huduma yake na hatimaye kuinasa saini yake kwa mkataba wa miaka miwili.

Mshambuliaji huyo tayari amepata nafasi ya kuonja ushindani wa soka la Tanzania baada ya kucheza dhidi ya Singida Black Stars Kigali, Rwanda, wakati wa mashindano ya CECAFA.

“Nilikutana na testi yangu ya kwanza ya soka la Tanzania nilipocheza dhidi ya Singida Black Stars pale Kigali. Ulikuwa mchezo muhimu kwangu kwa sababu ulinipa picha ya ushindani na aina ya soka nitakayokutana nayo hapa,” alisema Doumbia.

Katika mchezo huo uliofanyika Uwanja wa Amahoro, Doumbia alifunga bao moja wakati Simba ikiibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Singida Black Stars, hivyo kupata ladha ya kwanza ya ushindani wa timu za Tanzania kabla ya kuanza rasmi maisha yake Msimbazi.


MAGWIJI WAAMUA DABI

DABI ya Kariakoo imerejea tena, safari hii ikiwa katika mazingira tofauti baada ya Simba na Yanga kukutana katika mechi wa ufunguzi wa msimu wa Ligi Kuu Bara 2026/27 Uwanja wa New Amaan, Zanzibar.

Wachezaji wa zamani wa timu hizo, Sekilojo Chambua, Jerson Tegete, Credo Mwaipopo na Abdallah Shaibu ‘Ninja’, wamechambua kinachoweza kuamua mechi hiyo, huku wakisisitiza dabi haiamuliwi kwa historia pekee.

Chambua, ambaye aliwahi kuichezea Yanga, anaiona Dabi hiyo kama mtihani mkubwa kwa wachezaji wapya ambao bado hawajazoea presha ya soka la Tanzania.

“Dabi ni mechi tofauti na nyingine. Unaweza kuwa na kikosi kizuri na wachezaji wenye majina makubwa, lakini kama hawatakuwa tayari kiakili, wanashindwa kuonyesha uwezo wao. Simba na Yanga zinahitaji kucheza kwa utulivu na kutumia nafasi zitakazopatikana,” alisema Chambua.

Kwa upande wa Tegete, aliyewahi kuwa mshambuliaji wa Yanga, macho yake yanaelekezwa zaidi katika safu za ushambuliaji na alisema;

“Katika Dabi, unaweza kupata nafasi mbili au tatu tu za wazi. Huwezi kujua ni ipi itakuwa nafasi ya ushindi, ndiyo maana mshambuliaji anatakiwa kuwa makini muda wote. Ukipata nafasi, lazima uitumie.”

Mtazamo huo unaifanya vita ya washambuliaji kuwa moja ya maeneo ya kufuatiliwa kwenye mchezo huo, hasa kwa sababu timu zote zina wachezaji wenye uwezo wa kubadili matokeo.

Mwaipopo ambaye pia amewahi kucheza katika mazingira ya ushindani wa Simba na Yanga, alisema;

“Dabi haiwezi kushinda na mshambuliaji pekee. Kiungo kina nafasi kubwa sana. Ukidhibiti katikati, unamdhibiti mpinzani na unapata nafasi ya kuwafikisha washambuliaji wako kwenye maeneo mazuri. Timu itakayoshinda vita hiyo itakuwa imejipa nafasi kubwa.”

Ninja, ambaye naye ana uzoefu wa mechi hiyo, alisema; “Beki anatakiwa kuwa makini kwa dakika zote. Dabi inaweza kuamuliwa na kosa moja la beki, mpira wa pili au mpira uliokufa. Huwezi kumpa mpinzani nafasi rahisi halafu ukategemea kurekebisha baadaye.