Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Joshua arejea ulingoni 'kumvaa' Prenga

JOCHUA Pict

Muktasari:

  • Waandaaji wa pambano hilo sasa wamethibitisha ratiba kamili ya mapambano ya utangulizi yatakayopamba usiku huo mkubwa wa ngumi.

LONDON, ENGLAND: BONDIA nyota wa Uingereza, Anthony Joshua atarejea rasmi ulingoni Julai 25 nchini Saudi Arabia kupambana na Kristian Prenga katika pambano linalotajwa kuwa hatua ya mwisho kabla ya kukutana na Tyson Fury baadaye mwaka huu.

Waandaaji wa pambano hilo sasa wamethibitisha ratiba kamili ya mapambano ya utangulizi yatakayopamba usiku huo mkubwa wa ngumi.

Miongoni mwa vivutio vikubwa ni pambano la bingwa mpya wa uzani wa super middleweight wa WBO, Hamzah Sheeraz, ambaye atatetea mkanda wake kwa mara ya kwanza dhidi ya Mjerumani Simon Zachenhuber.

Sheeraz mwenye umri wa miaka 27 alitwaa ubingwa huo baada ya kumchapa Alem Begic kwa TKO katika raundi ya pili kwenye pambano lililofanyika Misri.

Kwa upande wa Zachenhuber mwenye miaka 28, ana rekodi ya ushindi 29 na kupokea kichapo kimoja pekee, huku mapambano 18 kati ya hayo yakimalizika kwa mtoano.

JOSH 02

Josh Kelly kutetea ubingwa

Bingwa wa IBF wa uzani wa super-welterweight, Josh Kelly, naye atapanda ulingoni kutetea mkanda wake kwa mara ya kwanza tangu autwae Januari baada ya kumshinda Bakhram Murtazaliev.

Kelly mwenye umri wa miaka 32 atakabiliana na Caoimhin Agyarko, ambaye hajawahi kupoteza pambano lolote katika rekodi yake ya mapambano 18 ya kulipwa.

JOSH 01

Joshua arejea baada ya kipindi kigumu

Joshua mwenye umri wa miaka 36 atakuwa anapigana kwa mara ya kwanza tangu alipomshinda Jake Paul kwa TKO katika raundi ya sita kwenye pambano lililofanyika Miami mwezi Desemba mwaka jana.

Hata hivyo, siku kumi tu baada ya ushindi huo, Joshua alihusika katika ajali ya gari nchini Nigeria iliyosababisha vifo vya marafiki zake wawili, Latif Ayodele na Sina Ghami.

Bondia huyo alinusurika akiwa na majeraha madogo na sasa anarejea ulingoni miezi minane baadaye akiwa tayari kuendeleza safari yake ya kurejea kileleni mwa uzani wa juu.

JOSH 03

Pambano la Tyson Fury bado linasubiri

Joshua tayari amesaini mkataba wa kupigana na Tyson Fury katika pambano kubwa linalosubiriwa kwa miaka mingi.

Fury mwenye umri wa miaka 37 naye anatarajiwa kuwa na pambano la maandalizi dhidi ya Mariusz Wach nchini Thailand usiku mmoja kabla ya Joshua kupigana na Prenga.

Hadi sasa tarehe na eneo rasmi la pambano la kihistoria kati ya Joshua na Fury bado havijatangazwa.

Hata hivyo, mkuu wa masuala ya ngumi nchini Saudi Arabia, Turki Alalshikh, ambaye anafadhili pambano hilo, ameeleza kuwa yuko tayari kulipeleka nchini Uingereza, ingawa anataka mapambano hayo yaanze saa 2:00 usiku kwa saa za London ili kuwarahisishia watazamaji wa Marekani.

Mbali na Uingereza, miji ya Las Vegas na New York nayo imeonyesha nia ya kuwa mwenyeji wa pambano hilo linalotarajiwa kuwa moja ya makubwa zaidi katika historia ya ngumi za uzani wa juu.