Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Wikiendi ya GG ligi za Ulaya

GG Pict
GG Pict

Muktasari:

  • Basi usikonde, shughuli nyingine ni leo Jumamosi na kesho Jumapili huko kwenye Ligi Kuu England na simpo tu, chomoka na ishu ya mabao, kwenye mechi hizo, nyavu hazilali njaa, yeyote anayemfunga mwingine. Mabao yapo.

LONDON, ENGLAND: UMEONA ule mziki wa usiku wa jana Ijumaa, Brighton ilipoonyeshana ubabe na Chelsea? Vipi mkeka wako umechanika?

Basi usikonde, shughuli nyingine ni leo Jumamosi na kesho Jumapili huko kwenye Ligi Kuu England na simpo tu, chomoka na ishu ya mabao, kwenye mechi hizo, nyavu hazilali njaa, yeyote anayemfunga mwingine. Mabao yapo.

Shughuli itaanzia King Power, wakati Leicester City itakayokuwa mzigoni kuikaribisha Arsenal, ambayo haitakuwa na straika wa asili, lakini ishu ya kufunga halijawali kuwa shida kwa kikosi hicho cha Mikel Arteta. Rekodi zinaonyesha, Leicester na Arsenal zimekutana mara 55 kwenye Ligi Kuu England, sare ni nane, huku Leicester ikishinda tano, nne nyumbani na moja ugenini, wakati The Gunners imeshinda 22, mara 15 nyumbani na saba ugenini. Itakuwaje safari hii?

Mechi nyingine ya mabao itakuwa Villa Park, wakati Aston Villa itakapokuwa na kibarua mbele ya Ipswich Town, huku kasheshe jingine la makipa kuwa bize kuokota mipira kwenye nyavu litakuwa huko Craven Cottage wakati Fulham itakapopepetana na Nottingham Forest. Mechi zote hizo ni za mabao mengi.

Mabingwa watetezi wa Ligi Kuu England, Manchester City watakuwa Etihad kuwakabili Newcastle United katika mechi ya kibabe kabisa, ambayo rekodi zinasoma kwenye mechi 49 walizokutana kwenye ligi, 10 zilimalizika kwa sare, huku Man City ikishinda 31, mara 19 nyumbani na 12 ugenini, huku Newcastle ikishinda nane tu, saba nyumbani na moja ugenini. Kasheshe hilo.

Mechi nyingine za mabao, Southampton itakuwa St Mary’s itakapocheza na Bournemouth, West Ham itacheza na Brentford huku Everton ya David Moyes itakuwa ugenini huko Selhurst Park kukabiliana na Crystal Palace.

Kesho, Jumapili zitapigwa mechi mbili kwenye Ligi Kuu England, Liverpool itakuwa na kibarua kizito kuikabili Wolves, wakati kasheshe zito litakuwa huko London, wakati Tottenham Hotspur itakapocheza na Manchester United.

Rekodi zinaonyesha, Spurs na Man United zimekutana mara 65 kwenye ligi, huku mara 14 zilitoka sare. Spurs imeshinda 12, mara saba nyumbani na tano ugenini, huku Man United imeshinda 39, mara 24 nyumbani na 15 ugenini. Mechi ya Spurs na Man United inavuta hisia kali kutokana na timu hizo mbili kuwa kwenye viwango vya hovyo kwa msimu huu.

Huko Italia, nako kumenoga ambapo leo Atalanta itacheza na Cagliari, Lazio ni moto na Napoli, huku AC Milan itakuwa na shughuli mbele ya Hellas Verona. Kesho, kutakuwa na kazi kubwa, Fiorentina itacheza na Como 1907, Monza na Lecce, Udinese na Empoli, Parma na AS Roma, wakati kasheshe litakuwa huko Turin, ambapo Juventus itakipiga na Inter Milan.

Huko Ufaransa, shughuli ya leo, Marseille itakipiga na Saint-Etienne, huko AS Monaco itakipiga na Nantes na Toulouse itakuwa na kazi mbele ya Paris Saint-Germain.

kesho Montpellier itacheza na Lyon, Le Havre na Nice, Lens na Strasbourg, huku Reims itacheza na Angers na Rennes itakipiga na Lille.